Tunachojifunza ni tofauti na tunachokiishi

Tunachojifunza ni tofauti na tunachokiishi

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,619
Niende moja kwa moja kwenye kile nilichokilenga,

Shuleni kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo tunakatazwa kabisa kutazamia. Mwanafunzi anayetazamia huwa anapewa adhabu. Huu ndo ukweli kwa elimu ya Tanzania.

Katika maisha ya kawaida, msingi wetu ni kutazamia. Anzia kwako mwenyewe, mambo mengi unayofanya ni kwa kutazamia kwa wengine, uvaaji, ulaji, imani n.k. Njoo kwenye familia yako – mwangalie jirani yako hapo mtaani, hadi kwa kiongozi wako wa jimbo (naishia hapa jimboni kwa sababu mwingine juu ya jimbo hairuhusiwi kumwongelea). Yote yanayotendeka ni kwa kutazamia tu. Ni wachache sana wanaofanya mambo kwa kutumia misingi ya akili zao.

Ushauri: Taasisi zinazohusika na elimu hapa nchini jaribuni kuliangalia hili. Kutazamia sio dhambi hadi kufikia hatua ya kumfutia mwanafunzi matokeo yake ya mwisho.

Una mtazamo upi katika hili?
 
Kama ni doctor aliyetazamia si atauwa watu? Au ataua kwa kutazamia !
 
Kama ni doctor aliyetazamia si atauwa watu? Au ataua kwa kutazamia !
Hakuna Daktari asiyetazamia, kama sio kutazamia basi wasingekuwa wanaenda kwenye mafunzo ya vitendo. Huko ndo kutazamia.
 
Wengi hawatakuelewa ila unahoja ya msingi!
Mkuu, ipo siku wataelewa ninachokimaanisha ... ila ninachokiamini ni kwamba wenye kuelewa kilichojificha kwenye maandishi huwa ni wachache sana. Wewe ni mmojawao; tuendelee kuwajuza hata kwa lugha za kimalaika.
 
Mie mwenyewe huwa najiuliza hivi kweli mitihani ni kipimo sahihi cha uelewa? unakuta mwanafunzi anasoma zaidi kipindi cha karibu na mitihani.
 
Mie mwenyewe huwa najiuliza hivi kweli mitihani ni kipimo sahihi cha uelewa? unakuta mwanafunzi anasoma zaidi kipindi cha karibu na mitihani.
Hapo kwenye bold; big-up!
Kwanza yanayofundishwa ni kama historia tu hayana maana yoyote.
Majuzi nilitembelewa na wataalam toka kituo kimoja cha ufugaji. Walipofika wakamkuta kijana wangu akawa anawaonesha namna tunavyootesha hydroponic fodder; pamoja na kwamba wao kuwa wataalam wa kilimo na mifugo lakini wanadai hawakuwahi kuona kitu kama hicho.
Hiyo ni picha tosha kwamba kinachofundishwa kwenye vyuo ni nje ya kinachoendelea kwenye real life.
Utendaji kazi wa mwanafunzi wa VETA ni wa tija kuliko Graduates wa vyuo vikuu tulivyo navyo.
 
Mkuu hydroponic fodder ni uoteshaji wa nini?
 
Back
Top Bottom