Tuna shindwa wapi wasomi wenzangu?? Nani alaumiwe

K-wire

JF-Expert Member
Dec 6, 2017
278
285
MAMA NA MWANA
Gozbert ; Mama wamenifukuza shule
Mama : Hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzila kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu. Kazana kusoma
Gozbert; Sawa mama naomba na pesa ya Matumizi, nitashukuru.
Mama; Sawa Mwanangu
Gozbert: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili
Mama; Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelala kwa kunywa uji na wadogo zako. Nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za Parizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima. Jitahidi usome mwanagu nakuombea.
Akamaliza chuo ukafika muda wa kwenda chuo.

Gozbert; Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo mama nimekosa sijui nifanye nini mama

Mama; Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitshindwaje? Namshukuru Mungu kwanza umefanya vizuri mwanangu. Nipo tayari kujaza madeni usome

Baada ya kusoma na kupata kazi nzuri mambo yakageuka

Mama; Gozbert siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini? Hata simu mwanangu!

Gozbert; Yaani mama majukumu ya kazi huwezi amini juzi nilikuwa Zanzibar ndo nimerudi majuzi hapa Dar. Utanisamehe mama

Mama; Kwani Zanzibar kuna mitandao tofauti nay a huku?

Gozbert; Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa namhudumia naporudi nyumbani.

Mama; Mdogo wako amefukuzwa shule ada inasumbua. Nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda kumfukuza tena.

Gozbert; Mama hivi bado unatengeneza pombe? Hivi biblia inasema nini kuhusu pombe mama? Hapana mama hapo unanikwaza kwa kweli

Mama; Sawa mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na yalaiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, kwa kutuma pesa ningekuwa nimeacha

Gozbert; Ningekutumia sasa hivi nakimbizana na ujenzi mama, hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya. Nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata. Nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa

Siku nyingine ikafuata

Mama; Nataka nije nimsalimie mjukuu wangu mwezi huu

Gozbert ; daah yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama mjukuu mwezi mmoja tu zimentoka kama milioni mbili

MSIMU WA SIKUKUU

Mama; msimu wa sikukuu nataka nije nisherehekee na mjukuu wangu huko dar

Gozbert; Daah bahati mbaya likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa uingereza kusherehekea huko. Tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

Tunakwama wapi watoto wa walala hoi
 
Labda kwenye bongo movie ila kweye reality hakuna kitu kama hicho...

Anaefanya hvyo atakua mpuuzi wa kiwango cha juu kabisa
 
Usichanganye wasomi na watu wasiojitambua. Lakini kumbuka ustaarabu na utu hausomewi. Unaweza ukaelimika bila kwenda kusoma.
 
Haya mambo yapo kabisa na yako yanaendelea amini usiamin yapo kwenye jamii labda Kama hujakutana nayo
 
hapo ni zaidi ya kukwama mkuu. na usipopata mke muelewa utajizolea laana maana kila mara atakuwa anaweka vikwazo mama yako asile mema ya inchi.
 
Labda kwenye bongo movie ila kweye reality hakuna kitu kama hicho...

Anaefanya hvyo atakua mpuuzi wa kiwango cha juu kabisa
Labda mtu awe kichaa hadi afanye hivyo aise hapana.

Mimi mama alikomaa kunisomesha kwa shida yaani nilipoingia tu chuo kale kaboom niligawana naye pasupasu.

Nilipomaliza tu na kupata kazi nilikomaa kwenye kachumba ka kupanga uswazi hadi nikamjengea yeye, vutia maji umeme nk ndipo nikaanza kuboresha maisha yangu mjini.

I thank God My Mama yupo japo umri sasa umeenda na magonjwa ya umri mkubwa kama miguu, presure nk yanamsumbua ila bima niliyomkatia inasaidia anapata matibabu sawia.

Sijawahi kumuacha apate shida na namuomba Mungu aniongoze hivi hivi mpaka atakapoamua yeye. Any time akitaka kuja nilipo aja atakavyo, nami huenda mara kwa mara hasa sikukuu zote eg krismasi , pasaka etc.

Tuwajali sana wazazi ndugu zangu tuwajali sana ni Mungu wa pili.
 
Je baba unamuhudumia?kwa sababu na wewe unakuja kuwa baba...
 
Educated Fools.

Schooling to them was about passing exams and getting jobs.

Not becoming intellectuals with the ability to fully utilize their brains.
 
Sio wasomi tu ni asilimia kubwa ya me wanaokumbuka wazazi wao especially baada ya kuanzisha miji yao
 
Je baba unamuhudumia?kwa sababu na wewe unakuja kuwa baba...
Wakati mama anateseka kulima vibarua hadi akanisomesha mzee alikuwa kasepa kaenda zake mkoa mwingine kaanzisha makazi mapya na kuoa mdada nesi , ila naye mzee hatukuwahi kumuonyesha chuki yoyote, aliumwa tukaenda kumjulia hali nakumbuka by then nilikuwa ndo nina kama mwaka hivi tu kazini. Bahati mbaya alifariki,mwili ukaletwa kuzikwa, Mungu amrehemu. Angekuwepo naye nadhani ningemjali ila siyo kwa kiasi sawa na mama ,siyo kabisa na ningemuuliza a few questions....😔
 
Kafunguka khs mama sana hadi sisi wazee hatuoni umuhimu wa kulea
😂😂Hapana ndugu yangu simaanishi baba atengwe ila ushuhuda wangu umekaa hivyo 'contextually' , kwa mimi mama tu ndo alihasle (mzee aliingia mitini) na naamini bila mama nisingefika nilipo, kwa hiyo kwa kweli I adore her!! Kama unajali wanao mkuu wana wajibu wa kukujali sana tena sana.
 
Wakati mama anateseka kulima vibarua hadi akanisomesha mzee alikuwa kasepa kaenda zake mkoa mwingine kaanzisha makazi mapya na kuoa mdada nesi , ila naye mzee hatukuwahi kumuonyesha chuki yoyote, aliumwa tukaenda kumjulia hali nakumbuka by then nilikuwa ndo nina kama mwaka hivi tu kazini. Bahati mbaya alifariki,mwili ukaletwa kuzikwa, Mungu amrehemu. Angekuwepo naye nadhani ningemjali ila siyo kwa kiasi sawa na mama ,siyo kabisa na ningemuuliza a few questions....😔
Pole mkuu,ila ukiona mwanaume anamuacha mwanamke jua kuna siri nzito ndani,na mama hata siku moja hatakuambia zaidi ya kumwaga sumu.Mfano, we mkeo anaweza kukukwaza ikakulazima kumtelekeza...mwisho wa siku mtoto anamezeshwa sumu kuhusu wewe....na wewe unaishia kuzeeka huku ukitaabika.Ndio maana tunaambiwa tuishi na wanawake kwa akili.
 
Labda kwenye bongo movie ila kweye reality hakuna kitu kama hicho...

Anaefanya hvyo atakua mpuuzi wa kiwango cha juu kabisa
wapo mkuu, maana hizo bongo movie story wanazitoa kwenye real life mkuu
 
Labda mtu awe kichaa hadi afanye hivyo aise hapana.

Mimi mama alikomaa kunisomesha kwa shida yaani nilipoingia tu chuo kale kaboom niligawana naye pasupasu.

Nilipomaliza tu na kupata kazi nilikomaa kwenye kachumba ka kupanga uswazi hadi nikamjengea yeye, vutia maji umeme nk ndipo nikaanza kuboresha maisha yangu mjini.

I thank God My Mama yupo japo umri sasa umeenda na magonjwa ya umri mkubwa kama miguu, presure nk yanamsumbua ila bima niliyomkatia inasaidia anapata matibabu sawia.

Sijawahi kumuacha apate shida na namuomba Mungu aniongoze hivi hivi mpaka atakapoamua yeye. Any time akitaka kuja nilipo aja atakavyo, nami huenda mara kwa mara hasa sikukuu zote eg krismasi , pasaka etc.

Tuwajali sana wazazi ndugu zangu tuwajali sana ni Mungu wa pili.
Huyo ni wewe mkuu, ila amini wapo wanaoshindwa mkuu, wakati mwingine maisha ya uzunguzungu yanachangia na kuwa na marafiki wenye maisha ya kuigiza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom