Tuna shindwa wapi wasomi wenzangu?? Nani alaumiwe

Tuna shindwa wapi wasomi wenzangu?? Nani alaumiwe

Labda mtu awe kichaa hadi afanye hivyo aise hapana.

Mimi mama alikomaa kunisomesha kwa shida yaani nilipoingia tu chuo kale kaboom niligawana naye pasupasu.

Nilipomaliza tu na kupata kazi nilikomaa kwenye kachumba ka kupanga uswazi hadi nikamjengea yeye, vutia maji umeme nk ndipo nikaanza kuboresha maisha yangu mjini.

I thank God My Mama yupo japo umri sasa umeenda na magonjwa ya umri mkubwa kama miguu, presure nk yanamsumbua ila bima niliyomkatia inasaidia anapata matibabu sawia.

Sijawahi kumuacha apate shida na namuomba Mungu aniongoze hivi hivi mpaka atakapoamua yeye. Any time akitaka kuja nilipo aja atakavyo, nami huenda mara kwa mara hasa sikukuu zote eg krismasi , pasaka etc.

Tuwajali sana wazazi ndugu zangu tuwajali sana ni Mungu wa pili.
Utafanikiwa sana maishani mwako

Niamini
 
Wapo wanaofanya hivyo mmoja wapo ni mdogoangu hakumbuki chochote kuhusu wazazi wake na hata ikitokea likizo akaamua kuja nyumbani hawa bebei wazazi wake zawadi yoyote ile
Labda kwenye bongo movie ila kweye reality hakuna kitu kama hicho...

Anaefanya hvyo atakua mpuuzi wa kiwango cha juu kabisa
 
Familia nyingi za ki-Africa ndiyo zipo hivyo...

Kwenye jamii mtu anaweza kua na jina kubwa sana na ni mtoaji mzuri sana... ila kwa wazazi wake ni sifuri mpaka huruma...



Cc: mahondaw
 
MAMA NA MWANA
Gozbert ; Mama wamenifukuza shule
Mama : Hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzila kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu. Kazana kusoma
Gozbert; Sawa mama naomba na pesa ya Matumizi, nitashukuru.
Mama; Sawa Mwanangu
Gozbert: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili
Mama; Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelala kwa kunywa uji na wadogo zako. Nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za Parizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima. Jitahidi usome mwanagu nakuombea.
Akamaliza chuo ukafika muda wa kwenda chuo.

Gozbert; Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo mama nimekosa sijui nifanye nini mama

Mama; Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitshindwaje? Namshukuru Mungu kwanza umefanya vizuri mwanangu. Nipo tayari kujaza madeni usome

Baada ya kusoma na kupata kazi nzuri mambo yakageuka

Mama; Gozbert siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini? Hata simu mwanangu!

Gozbert; Yaani mama majukumu ya kazi huwezi amini juzi nilikuwa Zanzibar ndo nimerudi majuzi hapa Dar. Utanisamehe mama

Mama; Kwani Zanzibar kuna mitandao tofauti nay a huku?

Gozbert; Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa namhudumia naporudi nyumbani.

Mama; Mdogo wako amefukuzwa shule ada inasumbua. Nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda kumfukuza tena.

Gozbert; Mama hivi bado unatengeneza pombe? Hivi biblia inasema nini kuhusu pombe mama? Hapana mama hapo unanikwaza kwa kweli

Mama; Sawa mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na yalaiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, kwa kutuma pesa ningekuwa nimeacha

Gozbert; Ningekutumia sasa hivi nakimbizana na ujenzi mama, hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya. Nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata. Nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa

Siku nyingine ikafuata

Mama; Nataka nije nimsalimie mjukuu wangu mwezi huu

Gozbert ; daah yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama mjukuu mwezi mmoja tu zimentoka kama milioni mbili

MSIMU WA SIKUKUU

Mama; msimu wa sikukuu nataka nije nisherehekee na mjukuu wangu huko dar

Gozbert; Daah bahati mbaya likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa uingereza kusherehekea huko. Tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

Tunakwama wapi watoto wa walala hoi
Naked truth ila ni wachache sana watachukulia kwa uzito wake!
 
Halafu mambo yakimwendea kombo kwa mfano kufukuzwa kazi kwa udanganyifu au wizi
Halafu mke nae akarudi kwao kwa maisha magumu hapo wa kulaumiwa nani?
Au kama kawaida atasema karogwa?

Inaweza kuwa ya kutunga lakini uhalisia na maisha ya wengi yapo hivyo na wengine hubadili na namba kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom