Mazungumzo Kati ya mama na mtoto wake jifunze kitu

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
MAMA NA MWANA

Gozbert: Mama wamenifukuza shule.

Mama: Hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzila kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu, kazana kusoma.

Gozbert: Sawa mama naomba na pesa ya Matumizi, nitashukuru.

Mama: Sawa Mwanangu.

*Gozbert: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili

Mama: Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelalia uji na wadogo zako, Nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za Parizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima, Jitahidi usome mwanagu nakuombea, akamaliza chuo ukafika muda wa kwenda chuo.

Gozbert: Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo mama nimekosa sijui nifanye nini mama.

Mama: Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitashindwaje? Nipo tayari kujaza madeni usome.

Baada ya kusoma na kupata kazi nzuri.

Mama: Gozbert siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini? Hata simu mwanangu!

Gozbert: Yaani mama majukumu ya kazi huwezi amini juzi nilikuwa Zanzibar ndo nimerudi majuzi hapa Dar, tanisamehe mama.

Mama: Kwani Zanzibar kuna mitandao tofauti nay! huku?

Gozbert: Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa na mhudumia naporudi nyumbani.

Mama: Mdogo wako amefukuzwa shule ada inasumbua, nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda kumfukuza tena.

Gozbert: Mama hivi bado unatengeneza pombe? Hivi biblia inasema nini kuhusu pombe Mama? Hapana Mama hapo unanikwaza kwa kweli.

Mama: Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na laiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, kwa kutuma pesa ningekuwa nimeacha.

Gozbert: Ningekutumia sasa hivi nakimbizana na ujenzi mama, hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya, nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata, nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa.

Siku nyingine ikafuata

Mama: Nataka nije nimsalimie mjukuu wangu mwezi huu.

Gozbert: daah yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama mjukuu mwezi mmoja tu zimenitoka kama Milioni mbili.

Gozbert: Daah bahati mbaya likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa uingereza kusherehekea birthday ya mtoto huko, tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

Tunakwama wapi watoto wa walala hoi???

Wee! niambie tuna akina Gozbert wangapi leo hii..?

 
Kizazi cha sasa kina hii tabia ila huko tuendako sidhani kama kuna mzazi atamtegemea mtoto.

Mimi napigana vita yangu, natimiza wajibu wangu kwa mtoto akifika umri wa kujitegemea aende zake na mimi nitapumzika nikisubiri siku yangu ifike
 
Back
Top Bottom