Tuwakumbuke wazazi waliotusaidia kufika hatua tuliyopo leo

Lucas philipo

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,034
2,656
MAMA NA MWANA

Clement komba: Mama wamenifukuza shule.

Mama: Hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzila kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu, kazana kusoma.

Clement Komba: Sawa mama naomba na pesa ya Matumizi, nitashukuru.

Mama: Sawa Mwanangu.

Clement Komba: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili.

Mama: Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelalia uji na wadogo zako, Nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za Parizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima, Jitahidi usome mwanagu nakuombea, akamaliza chuo ukafika muda wa kwenda chuo.

Clement Komba: Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo mama nimekosa sijui nifanye nini mama.

Mama: Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitashindwaje? Nipo tayari kujaza madeni usome.

[Baada ya kusoma na kupata kazi nzuri]

Mama:
Clement siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini? Hata simu mwanangu!

Clement Komba: Yaani mama majukumu ya kazi huwezi amini juzi nilikuwa Zanzibar ndo nimerudi majuzi hapa Dar, tanisamehe mama.

Mama: Kwani Zanzibar kuna mitandao tofauti nay! huku?

Clement Komba: Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa na mhudumia naporudi nyumbani.

Mama: Mdogo wako amefukuzwa shule ada inasumbua, nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda kumfukuza tena.

Clement Komba: Mama hivi bado unatengeneza pombe? Hivi biblia inasema nini kuhusu pombe Mama? Hapana Mama hapo unanikwaza kwa kweli.

Mama: Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na laiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, kwa kutuma pesa ningekuwa nimeacha.

Clement Komba: Ningekutumia sasa hivi nakimbizana na ujenzi mama, hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya, nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata, nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa.

Siku nyingine ikafuata

Mama: Nataka nije nimsalimie mjukuu wangu mwezi huu.

Clement Komba: Daah yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama mjukuu mwezi mmoja tu zimenitoka kama Milioni mbili.

Clement Komba; Daah bahati mbaya likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa uingereza kusherehekea birthday ya mtoto huko, tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

#My Take

Watoto tujitahidi sana kuwakumbuka wale waliotusaidia na kutufikisha tulipo leo. Usijione umetoboa, maisha ni mzunguko unaowadharau leo huenda kesho ikawa msaada wako.

Tuwatunze wazazi wetu ili tuishi miaka mingi hapa duniani. Ni aibu kuwadharau na kuwasahau wazazi wako waliopigania maisha yako hadi leo upo hapo ulipo. Ikumbukwe huenda leo ukawaona si kitu lakini hizo mali nakuambia hutadumu nazo, utajiri ulionao unaweza usikufikishe mahali popote kwani Ni suala la muda tu.

Yawezekana wazazi wasishuhudie kuanguka kwako lakini ndugu, jamaa, marafiki na hata watoto ambao walishuhudia pindi unawatupa wazazi wako watakuwepo na kudhihirisha fedheha na laana ya wazazi wako.

COPY & PASTE kutoka mitandaoni.
 
Nmeichukua nzima nzima

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom