Tumwapa dhamana mmeshindwa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumwapa dhamana mmeshindwa.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Topical, Jan 4, 2011.

 1. T

  Topical JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  1. David Mattaka (ATC):

  Hakuna ndege, hakuna safari za ndege ndani na nje zinazoeleweka, hatuoni kama una program sahihi kufufua shirika letu. kuna ugumu gani kusema nimeshindwa ideas zimeniishia na uachie wengine watanzania watafute solution kwenye hili shirika?

  2. Justin Mwandu (NIC):

  Shirika lenye mtandao mkubwa kuliko zote Tanzania, imeshindwa kulipa wadeni wake wakiwemo walimu wa shule za msingi, umeshindwa kubuni mkakati wa kuokoa, umekuwa mwoga kupita kiasi kufanya chochote. Kuna ugumu gani kusema creativity yangu imeiishia hapo watafutwe watu wengine kutoa solution kwa shirika hili? kwanini wasijumuishiwe kule kwa Emanuel Humba (NHIF) walau kila mtanzania awe na bima ya afya ya lazima?

  3. Mustafa Mkullo (MoF):

  Wizara yenye dhamana ya kutoa mwelekeo wa uchumi na ukusanyaji wa pato la serikali pamoja na kuthibiti mapato imekuwa chanzo cha upotevu wa pesa za serikali, tumeishiwa na mawaziri yenye uwezo hadi uendelee kubakia wewe?

  4. William Mhando (TANESCO):

  Ulipoiingia tu kitu cha kwanza kufanya ni kuwaudhi wateja eti unaomba kupandisha bei ya umeme badala ya kupunguza, umeongeza gharama za kuunganisha umeme, umeshindwa kudhibiti wafanyakazi wabadirifu na wezi kwenye shirika. Hicho ndicho tulichokutuma sisi wananchi? badala ya kutoa huduma mnatukomoa? hivi unajua kwamba ukitaka kuunganisha umeme lazima ununue nguzo mwenyewe? halafu hizo nguzo mnaziita za Tanesco bila aibu? watu wote waliounganisha umeme kwa kununua nguzo wakizitoa wanapohama mtabakiwa na nini? hii aina gani ya huduma mkuu?

  5. William Ngeleja (Madini na Nishati):

  Umekuwa mwongo, wizara yako haijasaidia wananchi ku sera wala kiutendaji bado tunanyongwa kwenye madini hakuna udhibiti wa mapato na pia kwenye umeme kila mtu ni shahidi. Kwani lazima uongoze wewe kama huna maarifa si uache? unatutesa wananchi?

  6. William Urio (PPF):

  Ulitakiwa kusaidia wastaafu waliochangia sio wastaafu (bodi members). Kila mwaka wanachama rejea mikutano kule Arusha, wanakuomba ujitahidi kuwasiliana na serikali ili sheria za kukokotoa pension irekebishwe lakini wapi? husikie wahadhiri wa chuo kikuu wamekuandikia barua na mchanganuo wao hujawasikiliza. tumekupa dhamana umeshindwa..

  Mmepewa dhamana na wananchi badilikeni au mjitoe?
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  At least david mattaka ameondoka ..tunasubiri na hao wengine muondoke ikiwezekana
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  At least wameondoka wengi wao; Bado kichwa ngumu Erio wa PPF na Justin Mwandu
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,774
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280

  Mkuu Waongeze Kikwete na Pinda katika list yako.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  tatizo siyo watu; ni sera mbovu za CCM; sera ambazo baadhi ya watu wanaamini "zinatekelezeka" wakati ni rahisi kuona "hazitekelezi". Tatizo ni utawala wa CCM. Ukishalijua hili utajua kwanini Said Mwema hawezi kusimamia jeshi la polisi, au Rashid Othman usalama wa taifa; utaona ni tatizo lile lile kwenye kila kona.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hao hado 2015 kwenye kura..sasa hivi tudeal na hao ambao wanatuumiza kwa karibu zaidi

  CEO ni cheo kikubwa unaweza kuleta mabadiliko mbona NHC wameweza?
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wewe una interest zako na ccm..ambazo hutaki ku-declare

  Tatizo ni watu si CCM
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mwjj

  Ile campign yako ya Idrisa must Go, Mkullo Must go, Haji Mponda must go..ilikuwa inalenga watu au ccm..
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,070
  Trophy Points: 280
  ..nadhani wakwanza aliyeshindwa ni Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  JK mophia
   
 11. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Inasababishwa na serikal dhaifu kuanzia raisi mpaka mwenyekiti wote wezi
   
 12. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kichwa ngumu ni Erio William Mkapa, ameliibia shirika (PPF) kwa kushirikiana na Martin Mmari (DF), Hosea Kashimba (Chief Internal Auditor-Chief Thief), na Julius KAM Mganga(Utawala-Chief witch Doctor)

  Kama Mkulo, Ngereja, na Dr. Kaparata (wa TUCTA kwa Mgaya) aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya PPF wameondoka na hawa wahesabu masaa tu wataondoka kwa aibu.


  Sasa hivi DG Erio ni billionea kuliko hata mama yake mlezi Anna Bejamin Mkapa(Kibaka wa Kiwira). Amua mradi wa nyumba Mwanza amepeleka kijijini kwa Rais Mstaafu ambaye ni mjomba wake Umachingani Mtwara. Na ili kufanikisha kafungua na kanda ya Mtwara yenye wanachama wasiozidi 2000
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndio maana tunamshauri atumie mamlaka yake ya kikatiba awatimue hawa ma CEO

  Maana wameshindwa kukidhi matarajio ya wananchi na madhumuni ya mashirika waliyopewa

  Wameshindwa kuwa wabunifu, na kutumia dhamana walizopewa vizuri

  Tushiriki katika kuwafichua ili watimuliwe..au wajiondoe wenyewe..

  Taifa litajengwa na wewe.
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yeye ni bilionea lakini ameshindwa hata kupambana ili kubadili sheria za kukutoa pension za wastaafu.

  Sijui anajisikiaje pensioner PPF kupewa 21,000/- kwa mwezi???

  Pensioners ndio clients wake..ameshindwa kukidhi matarajio ya clients wake.
   
 15. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Akipandisha pension ya wastaafu PPF inakufa maaana mihela wamegawana yote. Kama kila miaka mitatu toka 2008, wakurugenzi hulipwa group endowment an gratuity ya zaidi ya shs. 220M kila mmoja na wapo 9. Mishahara yao ni Tshs 12M kwa mwezi na DG Erio ni Tshs 15M kabla hujaweka marupurupu ya mafuta, simu, umeme, maji na pia hawatulii ofisini kila siku safari.

  DG akiwa Bagamoyo analipwa Tshs 450,000 kwa kutwa na nje ya nchi ni Usd1012 (Tshs. 1,600,000 kwa kutwa moja)

  Sasa apandishe pension yeye akale wapi?
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pesa za PPF wamezifanya kuwa ni viongozi wa PPF na si za wanachama?? pathetic

  JK fanya vitu ondoa hawa viumbe wawili waliobakia
   
 17. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mafuruki kaondoka, bado William Mkapa Erio kwa kukingiwa kifua na Mzee Mkapa.
   
 18. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2014
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu Bw. bado yupo PPF pamoja na ubadhirifu alioufanya. Mkataba wake uliisha mwaka jana, kakauka kimya akipeta ndani ya mkataba wa tatu bila ridhaa ya Rais
   
Loading...