Mkuu Mchakavumlasana, tuko pamoja hapa ila ofisi haina wajibu wa kumwambia chochote huyo, akamuulize mkewe, ni mtu mzima na ana uwezo wa kujieleza mwenyewe kwa nini atake maelezo kutoka ofisini? Niliisha sema nina wasiwasi na uwezo kiutendaji na huyo HR. Huyu HR eti bila aibu anasema alimuahidi kumjibu kwa maandishi, you must be out of your mind mr/mrs HR.
Tiba
Kama story hii ni ya kweli basi huyo mama ni mpuuzi na hastahili kuonewa huruma ama kufichiwa siri. Kama alijua alichokuwa anakifanya ni kibaya, kwa nini alikubali kufanya hivyo tena ndani ya ofisi? Si basi wangekwenda hata hotelini au guest house?
Halafu huyo mume wake inakuwaje anakuja kutaka kujua kwa maandishi ni kwa nini mmemsimamisha kazi mke wake? Kwani nyie kama ofisi mna uhusiano gani na huyo Bwana mpaka awatake maelezo kiofisi? Mjibu kwa urahisi huyo mume kwamba sababu zilizofanya mke wake asimamishwe ni za kiofisi na anayezijua ni mke wake, hivyo akamuulize mke wake. Huyo mume kwenu ni third party na hana haki ya kujua ni kwa nini mmemchukulia hiyo hatua mke wake. Amuulize mkewe.
Tiba
Iko hivi, hakuna utaratibu unaoruhusu mume kuandika barua akitaka kujua hatma ya mkewe. Hata mke akifa, urithi huwa ni jukumu LA mahakama kutoa tamko/amri baada ya vikao vya kifamilia.
Mjibu huyo mzee kuwa suala la mkewe ni kiofisi na kwamba yeye mkewe ndio amjulishe mumewe kosa, hata akimdanganya. Msimjibu kwa barua itakula kwenu.
Mwambie pia mkewe kuwa mume asiingilie suala ambalo lipo kwenye comm likisubiri maamuzi.
Hatari ya wewe kuongopa kwa mumewe eti hasara utafukuzwa kazi! Hatua ya wewe kumwqmbia mumewe kosa LA mkewe pia utafukuzwa kazi, huna mamlaka juu ya comm na utakuwa umeingilia ndoa ya watu.
Kukaa kimya pia mtaonekana mna njama dhidi ya mkewe na nakuapia babu atazaa na mtu hapo.
Pangu Pakavu.
atanieleza leo nikifika nyumbani,yaani anafanya umalaya ofisini kwake alafu ananidanganya mimi
Tiba naomba kujua hili nalo limekaaje, Mara nyingi wanawake huenda kushtaki ofisini kwa mumewe iwapo huduma stahiki ya matunzo kwa familia haipo, na Mara nyingi husikilizwa unakuta baba atakatwa mshahara wake, sehemu itaenda kwa mkewe, je kwann wakate mshahara,kwani familia au mke ndo kaajiriwa pale? Kwani na wenyewe si third part? Kwanini asiambiwe hili jambo halituhusu kamalizaneni nyumbani?Mkuu sina uhakika na utaalamu wako kwenye mambo ya HR lakini mume wake na huyo Mama hana uhusiano wowote na hiyo kampuni kiasi cha kufikia kutaka maelezo kwa maandishi. Mke ni independent legal entity na mume hana nafasi ya kwenda kuhoji ni kwa nini mke wake alisimamishwa. Kwa nini asimuulize mkewe? Mkewe ni bubu hawezi kuongea? Na wakati anasimamishwa si alipewa barua? Apewe hiyo barua na mkewe asome period.
Tiba
Tiba
Boss, Sina utaalamu na mambo ya HR, na sijaajiriwa bado. Nimejaribu kuongea kulingana na story ilivyo. Naweza kutokuwa sawa.
According to the HR of moment here, huyo mzee ana wajibu/haki ndio maana walikaa kujadili kama wamwambie ukweli ama lah, na ndio maana huyo mama alienda kumlilia huyo boss wake ili asiseme ukweli, na ndio maana pia walimuahidi huyo mzee kwamba watamjibu, na ndio maana yuko hapa kuomba ushauri wa namna ya kumjibu.
Now, i'm sure 'Mr HR' anajua sheria na utaratibu wa ofisi yake better than anyone here, na kama yeye anadhani huyo mzee anastahili kupewa maelezo, then that's it.
Kanuni za utumishi (standing order)zinatambua haki za mume,mke na mtoto kwahiyo mwenza yeyote ana haki ya kwenda kushtaki kwa mwajiri kwa issue yeyote inayoathiri familia kwa namna moja ama nyingine.kwa upande wa suala la huyu mzee na mkewe ni haki kabisa kwa mwajiri kumweleza ukweli mwanaume tatizo lililopelekea mkewe kuachishwa kazi.lakini sisi kama binadamu sometime unatakiwa kutumia busara na kuona side impact endapo utaeleza ukweli wa jambo hilo.Tiba naomba kujua hili nalo limekaaje, Mara nyingi wanawake huenda kushtaki ofisini kwa mumewe iwapo huduma stahiki ya matunzo kwa familia haipo, na Mara nyingi husikilizwa unakuta baba atakatwa mshahara wake, sehemu itaenda kwa mkewe, je kwann wakate mshahara,kwani familia au mke ndo kaajiriwa pale? Kwani na wenyewe si third part? Kwanini asiambiwe hili jambo halituhusu kamalizaneni nyumbani?
Ndugu yangu kama hayo maelezo yako ndivyo ilivyo, huyo HR anapashwa kibarua chake kioteshwe nyasi. Hakuna cha kujadili hapo, huyo Mzee hana haki ya kuuliza ni kwa nini mke wake amesimamishwa kwani kampuni haina mkataba wowote na huyo mzee. Mwenye mkataba ni mke wake. Hayo maswali yake akamuulize mkewe kwani yeye ni mtu mzima na anao uwezo wa kujieleza.
Kazi zina taratibu zake Bwana. Kwa mfano mume wangu hata kama nimemuandikisha ofisini kama mume, nisipotaka kumwambia nalipwa shilingi ngapi kwa mwezi, hawezi kuja ofisini kudai ofisi imwambie nalipwaje. Hata akija ofisi haipashwi kutoa jibu. Ni sawa na hii issue, huyu HR hakupashwa kutoa nafasi ya ili suala kujadiliwa kiofisi wala kutoa ahadi ya kuijibu barua. Kama alifanya hivyo, basi hiyo nafasi haimfai hata kidogo.
Hapa nazungumzia taratibu za kazi zilivyo, huyo mume ni third party hana haki ya kuhoji chochote kinachohusu ajira ya mke wake iwe kwa mdomo au maandishi. Ningekuwa ni boss wa huyo HR, mpaka sasa angekuwa kazi hana kwa kuukaribisha huu ujinga.
Tiba