Nicodemas Tambo Mwikozi
JF-Expert Member
- Aug 13, 2016
- 663
- 1,047
Mwaka 2014 nikiwa katibu wa Umoja wa vijana Chama Chama Cha Mapindizi UVCCM-Mkoa wa Morogoro Tulipokea Wageni Vijana kutoka Africa Kusini.
Lengo la Vijana hao ilikua ni kutembelea Eneo la Mazimbu ambalo wapigania Uhuru wa Taifa hilo lililopo kusini mwa Africa waliweka kambi na kuchukua mafunzo ya kumuondoa Kaburu na sera zake za ubaguzi wa Rangi ili waweze kujitawala.
Vijana hao walifika kuona na kujifunza Historia ya wapigania Uhuru wa Taifa lao na kuziona nyayo walizopitia, Historia inatukumbusha tulipotoka ili Tujue Tulipo na Wapi Tunakwenda. vijana hao walitaka kujua yaliopita.
Katika Mazungumzo yetu walionekana Kutoridhishwa na hatua za Maendeleo tulizofikia Kama taifa, Katika fikra zao picha ya jiji waliokua nayo kichwani Mwao ilikua ni jiji la aina Capetown, Johannesburg au Pretoria waliyayozoea kwao.
Hivyo walipotua dar na kuona jijini hakuna flyover,hakuna barabara sita sita zinazopishana, hakuna train za umeme , hakuna Mataa barababarani, na maudambwiudambwi Mengi waliyoyaona ni ishara za maendeleo katika jiji kutokuwepo jiji la Dar es Salaam walionekana kushanga.
Wakaanza kunihoji kwa utani ambao kwangu niliuchukulia kama dharau kwa taifa langu, mbona hamna hiki mbona hatujaona hiki mbona hakuna kile. Muda mwingi nilijibu hicho tunatarajia kujenga muda sio mrefu , hicho bado kabisa, hilo lipo kwenye Mchakato.
Baada ya kuona maswali yamekua Mengi niliamua kufipisha maswali yote kwa jibu Moja Fupi.
Sikilizeni Tungeweza Kua na vyote hivyo mnavyoulizia lakini fedha ambayo tungejengea miradi yote hiyo mnayoulizia Mlikula nyie wakati tunawasaidia mpate uhuru . Tuliwapa fedha zetu na nguvu kazi yetu kubwa, kuja kumwaga damu zetu kwa ajili yenu. Ukimya ukatawala Nidhamu ikarudi. Nikasema Dozi imeingia moyoni nikatabasamu.
Leo Tunaadhimisha Miaka kadhaa Tangu Baba wa taifa letu afariki lakini kiuhalisia Baba wa taifa hajafa bado anaishi nasi katika matendo mema na fikra zake njema ambazo zinadumu mpaka kesho.
Zipo namna zaidi ya milioni ambavyo Mtu anaweza kumuelezea na kumsimulia mwalimu, Mwalimu hakinai wala hachoshi Kumuelezea kwa namna yoyote ile.
Binafsi leo Namkumbuka kwa Falsafa yake ya "sisi Tanzania hatupo huru kama nchi jirani wenzetu hawapo huru"
Kauli hii iliamsha harakati za ukombozi kusini mwa Jangwa la sahara ambapo sera zetu za nje ilikua ni kuhakikisha nchi za kiafrica zinapata uhuru.
Kupitia sera hiyo Taifa letu lilipoteza fedha nyingi na damu nyingi za askari wetu kuhakikisha majirani wanakua huru. Uhuru ambao sasa wote tunafrahia.
Zipo ndoto zake kadhaa wa kadhaa ambazo Alitamani kuzitimiza lakini hakuzitimiza Alitamani kuona taifa letu likiwa na miradi mikubwa ya Umeme kama kama ule wa Stiglers Gorge, alihifadhi madini yetu akiamini vijana watasoma na kuyachimba kwa faida ya watanzania wote, alihifadhi mazingira na aliamini mtu anaeharibu mazingira anaharibu urithi bora wa kizazi kinachofwata baada Yake, kifupi alizilinda Rasilimali za taifa letu akiamini ni za kwa manufaa ya wote.
Imani yake hiyo na Falsafa za Baba wa taifa zinaishi na kutekelezwa kwa kiwango kikubwa Na Raisi wetu wa sasa Mh. John Pombe Joseph Magufuri ametimiza ndoto za Muasisi wa Taifa Letu, Mradi wa Stiglers Gorge ameutekeleza, Dodoma Kua Makuu Ya nchii Ametekeleza, ndoto ya Mwalimu kuona Madini yanawanufaisha Watanzania wote Mh. JPM Ametekeleza kwa kiwango kikubwa.
Tunapomuenzi MWALIMU siku ya Leo Tumuenzi Mwalimu nyerere kwa Kumpa kura John Pombe Magufuri Tarehe 28.10. Pamoja na na wabunge na madiwani watokanao na Chama chake Chama cha Mapinduzi ili Aendelee kutimiza Ndoto za Muasisi wa Taifa Letu.