Tumuenzi Hayata Wolfgang Dourado | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumuenzi Hayata Wolfgang Dourado

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Mar 21, 2012.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tumeanzi vipi jaji Dourado aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar akiongoza Mahakama ya Kazi ya Zanzibar aliyefariki hivi karibuni?

  Dourado aliwahi pia kuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Zanzibar mara baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 na baadaye kuzaliwa kwa taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hata hivyo katika kipindi cha uhai wake Dourado alikuwa miongoni wakosoaji wa mkataba wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ulioasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Nyerere.
  Aiendelea na wadhifa wake hadi kifo cha hayati Karume mwaka 1972 ambapo mabadiliko mbali mbali yalifanyika na kuja kwa wanasheria mbali mbali wakuu katika kipindi cha rais mstaafu Alhaji Aboud Jumbe akiwemo Bashir Swanzi kutoka Ghana pamoja na Damian Lubuva ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
  Mara baada ya kifo cha hayati Karume, Dourado alikuwa mwendesha mashtaka mkuu wa kesi ya kifo cha hayati Karume ambapo watu kadhaa walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifo wakiwemo wanasiasa maarufu.

  Dourado katika uhai wake aliwahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na Idara ya Mahakama Kuu ya Zanzibar akiwemo mjumbe wa kamati mbali mbali na tume za kurekebisha muundo wa Mahakama ya Zanzibar.

  Kufuatia kuundwa kwa Mahakama ya kazi ambayo lengo lake kubwa kusikiliza malalamiko yanayotokana na ajira katika utumishi wa Serikali na sekta binafsi Dourado aliteuliwa na rais mstaafu Amani Abeid Karume kuongoza mahakama ya kazi.

  Dourado alizaliwa Septembar 20 mwaka 1929 na kusoma katika shule mbali mbali za Unguja ikiwemo St. Joseph ya Zanzibar katika mwaka 1939-1946.
  Na baadaye kwenda Uingereza katika shule ya Royal London School of Economic katika mwaka 1962-1963.
  Baada ha hapo alipata kazi katika serikali ya Kikoloni tangu mwaka 1947 hadi alipostaafu mwaka 1985 ambapo pia alipitia katika ngazi mbali mbali za uongozi akiwemo katibu mkuu katika wizara tofauti.

  Nyadhifa nyengine alizoshika katika serikali ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mnamo Febuari mwaka 1964.

  Aidha katika mwaka 1977 aliteuliwa kuongoza Shirika la Bima la Zanzibar, na kuwa meneja mkuu wa kwanza, na baadaye kuongoza taasisi ya kuangalia muundo wa sheria mbali mbali za nchi, ikiwemo za mahakama kuu.
  Nyadhifa nyengine alizoshika wakati wa uhai wake ni kuwa mjumbe katika kamati mbali mbali katika sekta ya sheria ikiwemo kuwa mjumbe wa tume ya rais iliyokuwa ikitazama suala la mfumo wa chama kimoja au mfumo wa vyama vingi mwaka 1991.

  Mwili wa Dourado anatazamiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar kabla ya kufanyiwa misa katika Kanisa la Minara Miwili Shangani. Marehemu amewacha mke mmoja na hakujaaliwa kupata mtoto
   
 2. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Bakhti mbaya huyo Hayata Wolfang Dourado hatumjui huku bara. Pole sana yakhe!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwanza ni furaha iliyoje kukuona hapa JF. Nilidhani na wewe ulijiunga na wale waliokimbilia Somalia:-
   
 4. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mambo ya Al-Shabab yakhe!
   
 5. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sasa huyo Wolfang si atakuwa Kafir. What is so special about him?
   
Loading...