Mabibi na mabwana, Mama Samia anahitaji uungwaji mkono katika kuijenga nchi hii. Mama ni muungwana na anayo nia ya dhati ya kuiendesha nchi kwa mujibu wa katiba.
Pamoja na yote anayosema na nia yake njema ya kufanana na JPM, mama ameonyesha kwa vitendo kuwa si katika dhuluma wala katika kuvunja katiba au sheria.
Mwenye macho haambiwi tazama:
1. Leo uamsho wako huru
2. Mdude yuko huru
3. Kesi bambikizi 147 Takukuru zimefutwa
4. Watu hawapotei tena
5. Watu wasiojulikana hawapo tena
6. Nk
Hayati Magufuli alihitaji kupewa muda kuinyorosha nchi. Mama anaomba muda kusimamisha uchumi. Lakini kwani katiba ya nchi inasemaje? Katiba ya nchi itatamalaki. Na hili si hisani. Panga pangua katiba ni lazima kutamamalaki. Na hili ndilo eneo tunalopaswa kumsaidia sana mama katika ujenzi wa nchi hii.
Tusichoke kumsaidia mama katika kuijenga nchi hii kwa kuzingatia matakwa kamili ya katiba iliyopo, tunapojiandaa kwa mwendelezo wa kudai katiba mpya iliyoboreshwa.
Yaliyotutokea kipindi kile hayapaswi kurejelewa.
Ninawasilisha.