Tumsaidie Rais Samia kuijenga nchi hii

Tumsaidie Rais Samia kuijenga nchi hii

Mama alishasema:

Samia = JPM

Kama hivyo si tungaliishia hapa?

Nani hakujua JPM alitaka nini?

Mbona leo:

1. Sabaya yuko kidogo
2. Uamsho wako huru
3. Mdude yuko nje
4. Shughuli za kisiasa so far hazibughudhiwi?
5. Nk

Tulitaka mama asemeje?

Majibu yetu kwake yanapaswa kuwa wazi. Yaliyokinyume cha katiba hatukubali.

Haipo vita isiyokuwa na casualties.

..hilo neno " vita " limenikwaza.

..tulipata uhuru toka kwa Muingereza kwa njia ya majadiliano.

..lakini chaguzi zetu zimekuwa na umwagaji damu kuliko harakati za kupata uhuru.

..wapinzani kumsihi Mama Samia aruhusu mikutano, jambo ambalo limeruhusiwa kikatiba, ni kumpa heshima kubwa sana. Mama anatakiwa arudishe uungwana ambao vyama vya upinzani vimemuonyesha.
 
Mandela anasema "no easy walk to freedom." Anayetegemea na easy ride hapa yuko in a very wrong place.
🤣🤣Kuongea ni RAHISI Sana.....

Wamisri waliyatafuta hayo na kumuondoa HOSNI MUBARRAK ili wawe na huo "Uhuru".....

Kilichotokea ni HISTORIA....

Wako chini ya FIELD MARSHAL EL SISI.....🤣🤣🤣
 
Kinachoongea ni KITI CHA URAIS....si jinsia ya RAIS....

Mama ni muangalifu mno....ana staha mno......

Ila UAMIRI JESHI WAKE kwa mustakabali wa taifa uko palepale.....

Endeleeni tu kuleta ULIBERALI kwa taifa lililo chini ya WAHAFIDHINA WA CCM.....

#KaziIendelee

..nakubaliana na wewe kuwa mama ni muangalifu.

..lakini kwa kauli alizotoa leo ameteleza.
 
..nakubaliana na wewe kuwa mama ni muangalifu.

..lakini kwa kauli alizotoa leo ameteleza.
Ameteleza wapi ?!!!

Katiba mpya si lengo la CHAMA TAWALA.....

Sawa mtasema huo ni UBABE...ila ndio ukweli wenyewe huo.....

Siku CHADEMA ikiingia madarakani itatuletea hiyo KATIBA MPYA......

#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Mabibi na mabwana, Mama Samia anahitaji uungwaji mkono katika kuijenga nchi hii.

Mama ni muungwana na anayo nia ya dhati ya kuiendesha nchi kwa mujibu wa katiba.

Pamoja na yote anayosema na nia yake njema ya kufanana na JPM, mama ameonyesha kwa vitendo kuwa si katika dhuluma wala katika kuvunja katiba au sheria.

Mwenye macho haambiwi tazama:

View attachment 1833936

1. Leo uamsho wako huru
2. Mdude yuko huru
3. Kesi bambikizi 147 Takukuru zimefutwa
4. Watu hawapotei tena
5. Watu wasiojulikana hawapo tena
6. Nk

Hayati Magufuli alihitaji kupewa muda kuinyorosha nchi. Mama anaomba muda kusimamisha uchumi.

Lakini kwani katiba ya nchi inasemaje? Katiba ya nchi itatamalaki. Na hili si hisani.

Panga pangua katiba ni lazima kutamamalaki. Na hili ndilo eneo tunalopaswa kumsaidia sana mama katika ujenzi wa nchi hii.

Tusichoke kumsaidia mama katika kuijenga nchi hii kwa kuzingatia matakwa kamili ya katiba iliyopo, tunapojiandaa kwa mwendelezo wa kudai katiba mpya iliyoboreshwa.

Yaliyotutokea kipindi kile hayapaswi kurejelewa.

Ninawasilisha.

Yes tuijenge nchi yetu kama watanzania, bila kubaguana wala kuleta upendeleo usio na sababu. Mama asituangushe. Serikali yake ijikite kuwatumikia wananchi. Tumechoka na rushwa na kashfa za kufuja hela za umma. Tumechoka na watu wachache kutumia nafasi za umma kujinufaisha kwa hila wao na familia zao.
Mama ana hekima. Atulee wote tukae kama wamoja na watu wenye nia ya kujenga Taifa imara la Tanzania.
 
..hilo neno " vita " limenikwaza.

..tulipata uhuru toka kwa Muingereza kwa njia ya majadiliano.

..lakini chaguzi zetu zimekuwa na umwagaji damu kuliko harakati za kupata uhuru.

..wapinzani kumsihi Mama Samia aruhusu mikutano, jambo ambalo limeruhusiwa kikatiba, ni kumpa heshima kubwa sana. Mama anatakiwa arudishe uungwana ambao vyama vya upinzani vimemuonyesha.

Mkuu kiswahili kina limitations zake na hasa unapoandika na usingizi ukikunyemelea.

Neno vita nimekuwa nikijitahidi sana kuliepuka hata hivyo lipo hapa ki nahau zaidi. Kukitumika nyani hapa si yule wa porini.

Itambulike mchakato wa katiba mpya hautaridhiwa kwa kuombwa mezani. Ukweli huu utakapotambuliwa na mamlaka tutapata mwanzo wa kupata katiba mpya na si vinginevyo:

Tambua siri ya mafanikio ya jamaa wa uamsho:

IMG_20210628_233643_743.jpg
 
Mkuu kiswahili kina limitations zake na hasa unapoandika na usingizi ukikunyemelea.

Neno vita nimekuwa nikijitahidi sana kuliepuka hata hivyo lipo hapa ki nahau zaidi. Kukitumika nyani hapa si yule wa porini.

Itambulike mchakato wa katiba mpya hautaridhiwa kwa kuombwa mezani. Ukweli utakapotambuliwa na mamlaka tutapata katiba mpya na si vinginevyo:

Tambua siri ya mafanikio ya jamaa wa uamsho:

View attachment 1834081
Kwa hiyo UAMSHO wamefanikiwa?!!!

Kupeleka CHAKULA gerezani kwa miaka hiyo 8 ni mafanikio ?!!!

Hivi umemsikiliza vyema sheikh ul muadhama Ashaikhul Kiraam Mselem bin Alii akisema kuwa "INATOSHA WAKO HURU....MAMLAKA ZIKIWAAMBIA ACHENI KUFANYA HAYA WATAACHA....HUWEZI KUSHINDANA NA WENYE NGUVU..."

Maneno mazito mno hayo.....

AKILI KUMKICHWA.....

Mie Brown niendelee tu kuutafuta "ubwabwa" nitunze vitoto vyangu vidogo ..

#KaziIendelee
 
🤣🤣Kuongea ni RAHISI Sana.....

Wamisri waliyatafuta hayo na kumuondoa HOSNI MUBARRAK ili wawe na huo "Uhuru".....

Kilichotokea ni HISTORIA....

Wako chini ya FIELD MARSHAL EL SISI.....🤣🤣🤣

Misri ni Misri na Tanzania ni Tanzania.

Tunajua kuwa wanufaika nyie mtafanya kila propaganda uchwara kama hizi kufarakanisha watu.

Kulikuwa na uzi hapa utakuwa unakuhusu mkuu:

Hudhani kuwa tunastahili katiba muafaka kama Yanga tu Kikwette kawashauri wapate katiba muafaka?
 
Kwa hiyo UAMSHO wamefanikiwa?!!!

Kupeleka CHAKULA gerezani kwa miaka hiyo 8 ni mafanikio ?!!!

Hivi umemsikiliza vyema sheikh ul muadhama Ashaikhul Kiraam Mselem bin Alii akisema kuwa "INATOSHA WAKO HURU....MAMLAKA ZIKIWAAMBIA ACHENI KUFANYA HAYA WATAACHA....HUWEZI KUSHINDANA NA WENYE NGUVU..."

Maneno mazito mno hayo.....

AKILI KUMKICHWA.....

Mie Brown niendelee tu kuutafuta "ubwabwa" nitunze vitoto vyangu vidogo ..

#KaziIendelee

Unarukia rukia tu? Soma nyuzi.
 
Kama ambavyo sitishi bali nasema ukweli pia.
Sawa Komredi brazaj....

Endelea kuipigania katiba mpya kwa NGUVU ZOTE ULIZONAZO.....

TO EVERY ACTION THERE IS AN EQUAL AND OPPOSITE REACTION

#KaziIendelee
 
Kwani COVID 19 haipo ?!!
Kwani hakuna wanaopumulia mashine?!!!

Hivi umeshawahi kuwafikiria vyema MADAKTARI NA MANESI wetu wanaotoa huduma kwa hao wagonjwa wa COVID-19?!!!

Yaani hata hawa wataalam wetu wasichomwe hizo CHANJO ili waendelee kutupatia huduma?!!!

Hivi hao wataalam wetu wakitoka humo mawodini kwa wagonjwa wa UVIKO huwa hatukai nao BAA NA VIJIWE VYA KAHAWA?!!!

Hivi hao wataalam huwa hawarudi majumbani mwao kujiunga na wanafamilia wao ?!!!

FIKIRIENI NJE YA BOX....

#KaziIendelee
Acha ujinga ww! Ni daktari yupi huyo anayetaka kuchomwa maujinga hayo!? Aliyekudanganya yanakinga ni nani!?
 
Misri ni Misri na Tanzania ni Tanzania.

Tunajua kuwa wanufaika nyie mtafanya kila propaganda uchwara kama hizi kufarakanisha watu.

Kulikuwa na uzi hapa utakuwa unakuhusu mkuu:

Hudhani kuwa tunastahili katiba muafaka kama Yanga tu Kikwette kawashauri wapate katiba muafaka?
Sawa.....

Ila harakati za wananchi wa MISRI hazitofautiani sana na nchi nyingine barani Afrika....

Endelea kupambana MLIBERALI....
 
Acha ujinga ww! Ni daktari yupi huyo anayetaka kuchomwa maujinga hayo!? Aliyekudanganya yanakinga ni nani!?
😲😲🤣🤣
Baadhi ya watanzania waliifuata nje ya nchi hiyo CHANJO....sembuse MADOKTA wetu ambao wanaletewa hawa nyumbani ?!!!!

Mkuu KINGA NI BORA KULIKO TIBA.....

#KaziIendelee
 
Chanjo ni hiari. Sielewi kwa nini kitu cha hiari jiwe issue kwa yeyote.

Binafsi nitachanjwa on day 1.
Tutachanjwa wote mkuu.....

Mimi nitapiga picha niipost humuhumu ndani pale BEGA langu litakapopokea hiyo SINDANO....

#ChanjoYaUvikoNiHiyari
 
😲😲🤣🤣
Baadhi ya watanzania waliifuata nje ya nchi hiyo CHANJO....sembuse MADOKTA wetu ambao wanaletewa hawa nyumbani ?!!!!

Mkuu KINGA NI BORA KULIKO TIBA.....

#KaziIendelee
Mkuu hiyo ingekuwa haina agenda nyingine na inakinga kweli hata mie ningeifuata nje! Hii ya sasa si kitu kihivyo! Na inamadhara sana!
 
Tutachanjwa wote mkuu.....

Mimi nitapiga picha niipost humuhumu ndani pale BEGA langu litakapopokea hiyo SINDANO....

#ChanjoYaUvikoNiHiyari

Haki, uhuru na usawa ndiyo msingi wa katiba iliyopo ambao sote bila exception tunapaswa kuizingatia.

1. Chanjo hiari tusipangiane
2. Kujumuika hiari tusipangiane
3. Kudai haki hiari tusipangiane

Ni katika mwendelezo huo Mama ajenge uchumi na sisi tufanye yetu na tutampa support yote ndani ya katiba.

Au nasema uongo jombi.
 
Back
Top Bottom