Huyu mzee mwenangu atakuwa anafail mahali fulani. Makubaliano ya yeye kumwoa mama wa binti yalikuwa makubaliano yao wawili hayakuhusisha binti.
Kuhusu kumlea na kumsomesha pia nimakubaliano yake na mama yake binti, hayakuhusisha binti mwenyewe.
Mahari ni ujira unaotolewa kwa wazazi kama shukurani kwa upane wa pili baada ya kuchukuwa binti yao.
Kuachana kwa mama binti na baba binti hakumaanishi binti naye amchukie babake. Alafu mahari yenyewe kiasi gani hata imtoe roho huyu mlezi, uko kwetu Kanda maalumu tumekuwa tukioa kwa kutoa mahari ya ng'ombe mbuzi, kondoo na majembe, lakini kwa Harusi mjini ni hela hivo sioni sababu ya mlezi kulilia mahari ambayo kimsingi haiwezi kulingana na gharama alizotumia kumtunza huyo binti tangu akiwa na miaka 3 mpaka kumaliza chuo tena kwa kumsomesha utabibu, nani hajui gharama za kozi za afya?
Wenzetu huko Sudani mahari ni ng'ombe 100 -500 tena baada ya kutoa hiyo mahari mwanamke anakaa ndani tu kwa miaka 4 akifanyiwa kila kitu na mawifi huku akitumia muda huo kumsoma mme, baada ya hiyo miaka minne ndo inafanyika tena sherehe ya kupika ambapo ndo siku wanachinjwa kuanzia ng'ombe watatu na kuendelea ili mwanamke awapikie wakwe na familia ya mme.
Na endapo kwa kipindi hiki mwanamke hakukubaliana na tabia za mme basi anaweza kuchagua kuondoka na ng'ombe hawatarudishwa.
Hitimisho mzee mwenzangu achana na hizi stress zisizo za lazima na amabazo zitazalisha stress nyingine. Mzee mwenzangu usijidanganye kuwa mkeo anakupenda kuliko anavyo mpenda mwanae kitakachofuata hautokimdu kabisa.
Acha mahari apewe huyo baba mzazi wa huyo binti