kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,300
- 17,577
Ninamfurahia mtu yeyote anaeniambia nijitegee, hata wahenga wetu waliuona ubaya wa mtu kutegemea misaada kutoka kwa ndugu, rafiki au jirani, wakaona waje na misemo mingi ya kiswahili ili kusisitiza na kuonyesha ubaya wa kuwa tegemezi kwa mtu "mtegea cha ndugu hufa angali masikini, cha mtu mavi ukikiona tema mate, na nguo ya mwenyewe haistiri matako". Hata wazee wetu walichukia utegemezi kwa watu wengine.
Tangu nikiwa mdogo Nina tabia ya kumfurahia yeyote anayeniambia nijitegee kwenye mambo yangu, nami nikajenga tabia ya kujitegemea katika mambo yangu mengi na kuona faida yake. Watoto wangu hadi leo wako huru kabisa kwakuwa nimewasomesha hadi vyuoni bila kuitisha vikao vya ndugu, rafiki na majirani zangu kuhusu gharama za kuwasomesha. Sina tabia ya kutoa michango ya harusi, vipairama na kubariki ndoa kwa ndugu, majirani na marafiki zangu. Natumia kwa mujibu wa nilichokuwanacho mfukoni. Najenga nyumba, nanunua gari, nafanya sherehe, nasomesha watoto shule kulingana na uwezo wangu. Sifuati mkumbo.
Hakuna ubishi nchi za kiafrika zimekopa na kutumia misaada bila faida kwa wananchi wao. Wanaomchukia Trump ni watu wasiotaka kuusikia ukweli masikioni mwao, lakini anachosema kuhusu misaada kwa nchi za Afrika ni kweli kabisa, hatustahili kutegemea misaada miaka 60 baada ya uhuru. Ndiyo maana nchi nyingi za dunia hii zinamheshimu sana Rais wetu Magufuli kwa anachokifanya kuelekea kukata umuhimu wa kutegemea misaada kama njia kuu ya ku survive.
Ningekuwa mimi Rais Magufuli ningehangaika tu na kukuza uchumi kwanza na kuachana na habari ya elimu ya bure, afya na elimu. Hata wazungu wamefika pale walipo leo kiuchumi kwa kuhangaika na miundo mbinu (uchukuzi, nishati, maji) ya kukukuzia uchumi tu kwanza na kuacha huduma nyingine za jamii kama Afya na elimu zijihangaikie zenyewe au zifanywe na watu binafsi na mashirika dini. Mpaka leo kule Marekani wako wananchi wengi wasiopata elimu na afya kwakuwa ni ghali mno. Obama Care ilikuja tu hivi karibuni kabisa.
Huwezi kushughulika na huduma za kijamii na kukuza uchumi kwa wakati mmoja.