Tumkumbushe Sirro: Mkubwa akijamba hatakiwi kusingizia watoto

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
KUJAMBA ni tendo jema kiafya. Ni upumuaji. Linakuondolea gesi mwilini. Ukibanwa na haja, choo kikiwa mbali, ukijamba unapata unafuu. Haja inalegea.

Hata hivyo, kujamba ni tendo lenye kuhitaji faragha. Kujamba mbele za watu ni dalili za kutojiheshimu. Umakini huhitajika unapojamba kipindi umebanwa na haja, harufu yake haivumiliki. Uangalifu huhitajika zaidi ukiwa na tumbo la kuhara. Unaweza kudhani unajamba kumbe unaharisha.

Hutokea ukajamba bila kupangilia. Hewa inakutoka yenyewe. Kanuni ni moja; ujambe bahati mbaya au kupanga, iwe kuzidiwa na gesi au kupunguza makali ya haja, ukijamba hakikisha humsingizii mtoto. Bora unyamaze. Mtoto atakuumbua.

Mtoto atapayuka tu: "Unanisingizia nimejamba wakati wewe ndiyo umejamba." Hata ambao hawakuusikia ushuzi, watajua. Waza ndio sasa unaleta ufundi wa kujamba kumbe unaharisha, halafu unamsingizia mtoto. Aibu yake hutaisimulia.

NI ANGALIZO KATIKA MFANO

Huo ulikuwa mfano. Nilichotaka kukijengea maudhui ni hiki; Oktoba 19, mwaka huu, siku ambayo IGP Simon Sirro alitokeza kwenye vyombo vya habari na kuuonesha umma gari linalodaiwa kutumiwa kumtorosha Mo Dewji baada ya kumteka, Colosseum Hotel, Oysterbay, watu wengi walikosoa. Walishambulia.

Niliandika tweet yenye maneno: "Tujifanye tumekubali kudanganywa. Tujifanye hatujashtukia kitu. Tuwapongeze kwa hizo findings za upelelezi wao. Tuwajaze upepo ili wafanikishe kutuletea Mo Dewji. Baada ya Mo kupatikana ndio tuanze kuwasuta. Tukiwasuta sasa tunaweza kuharibu. Mimi naanza; Hongera sana polisi."

Tweet yangu ilimaanisha kukumbusha wakosoaji kuwa lengo namba moja ni Mo Dewji kupatikana, siyo namna gani angepatikana. Baada ya kupatikana ndiyo tunapaswa kurejea kwenye mjadala wa namna ambavyo Sirro alivyotulisha matango pori.

Si kwamba hoja za wakosoaji hazikuwa na maana, la! Tena zilikuwa za msingi hasa. Ila kwa aliyeona mkutano wa Sirro na vyombo vya habari, angejua kwamba Mo alikuwa karibu kupatikana au kuachiwa. Kubisha na kumzodoa Sirro ingesababisha ionekane kuwa 'muvi' haijapatiwa. Tungechelewa kumpata Mo.

Ni jambo la heri kuwa Mo amepatikana. Watanzania wakawa na furaha. Si kwamba alivyopatikana ilijibu maswali na kuondoa utata, la! Maswali yaliongezeka zaidi. Viulizo vilitawala kwenye kila kichwa cha Mtanzania mwenye akili na anayeipenda nchi yake. Mazingira ya jumla yalionesha kuna sinema imechezwa.

Hiyo sinema iliibuliwa na polisi wenyewe. Mkutano wa Sirro kwenye vyombo vya habari uliwapa mshangao wengi. Wanaoipenda nchi yao walimwaga machozi. Waliona wanachezewa. Nchi yao inachezewa. Daima kuna hasara kubwa katika kuichezea nchi.

Akichokisema Sirro kilitofautiana na maelezo ya aliyekuwa Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kuhusu picha zenye kunaswa na kamera za usalama (CCTV Camera). Mambosasa alisema kamera hazikunasa picha za waliomteka Mo wala gari lililotumika kumtorosha. Sirro akaibuka na picha ya gari, akasema CCTV Camera zilisaidia kupata picha ya gari na uelekeo wa gari baada ya utekaji.

Picha iliyooneshwa siyo ya CCTV. Hapohapo polisi wanataka wananchi waelewe bila kuhoji. Wanapohoji wanaitwa maadui wa polisi. Vema kumkumbusha Sirro wamba mkubwa akijamba, akisingizia watoto lazima ataumbuka.

POLISI WETU HAWAJUI SINEMA

IGP Sirro alisema kuna watu wanataka kulifundisha jeshi la polisi jinsi ya kufanya kazi. Ametoa vitisho! Sirro anajisahaulisha kwamba anaowatisha ndiyo wamiliki wa jeshi. Unamzuia mwenye mali asikosoe uendeshwaji wa mali yake.

Sirro alipaswa kutambua hili; utoaji wa taarifa kuhusu gari na namna Mo alivyopatikana, unaibua wasiwasi mkubwa kwamba kuna kitu zaidi ya kilichoelezwa. Ama mtekaji walishamjua, kwa hiyo kuna namna ilifanywa kumlinda, au mtekaji ni mtu hatari, kwa hiyo ilibidi kumzunguka.

Tujenge hoja; Sirro ile picha ya gari aliitoa wapi? Haikuwa picha ya CCTV na walisema CCTV hazikunasa gari. Walijuaje kama lile ndiyo gari lenyewe?

Colosseum Hotel alipotekwa Mo ni eneo nyeti na lina ulinzi mkubwa. Kuna majengo nyeti yenye ulinzi wa kutosha. Inakadiriwa kuna CCTV Cameras takriban 30. Zote hizo zisinase gari likipita?

Mtu atekwe jirani na Makao Makuu ya Usalama wa Taifa. Jirani na Nyumba ya Makamu wa Rais. Ubalozi wa Marekani panaposifika kwa vifaa vikali vya kiusalama, hapako mbali. Kweli zikosekane picha za kiusalama kote huko? Halafu inakuja picha ya kupigwa na kamera ya simu, gari likiwa limepaki.

Swali linakuja; walilijuaje? Walilikuta wapi? Kwa nini hawakulikamata? Je, picha ilipigwa kabla ya tukio? Kama ni ya kabla ya kabla ya tukio, maana yake waliipata baada ya upelelezi wa kipolisi. Ni kwa nini hawakuwa na majibu ya mmiliki? Wakaishia tu kusema wanamjua dereva.

Sirro alisema gari lilipotoka Colosseum lilielekea Kawe. Walijuaje? Barabara ambazo gari lilipita, kuna CCTV Cameras nyingi. Kwa nini polisi hawakuomba ushirikiano na wamiliki wa nyumba zenye CCTV ili kupata picha inayoondoa utata?

Imeelezwa gari limesajiliwa Msumbiji. Ikaelezwa pia kwamba gari hilo liliingia nchini kupitia Kenya. Hivi Sirro haoni huu mkanganyiko? Mara watekaji ni Wazungu, mara ni watu wenye kuongea lafudhi za Kusini ya Afrika. Mkanganyiko huu hauonekani kwa Sirro?

Mchana polisi wanaonesha gari la watekaji. Kwa vyovyote vile watekaji walikuwa wakifuatilia vyombo vya habari, maana waliyemteka ni mtu mzito. Wanaona gari lao limewekwa wazi, halafu usiku wanaliendesha mpaka Gymkhana, Dar na kumtelekeza Mo pamoja na gari. Hawa watekaji wana akili kweli?

Gari limeshajulikana, polisi wanalijua. Gari ambalo limeoneshwa na televisheni zote za ndani, na nyingi za nje. Gari litoke lilipokuwa mpaka Gymkhana bila kikamatwa na polisi wa doria. Lilipitia barabara zipi? Usalama wetu upoje?

Maswali haya ni mengi na polisi wameshindwa kuyajibu. Badala ya kuyajibu polisi wanatoa vitisho. Vitisho hivyo si lolote, ni sawa na kujamba kisha unamsingizia mtoto.

TUSEME UKWELI

Ni kweli Mo Dewji alitekwa. Na imemuuma sana. Kuhusu nani aliyemteka, hilo ni doa kubwa kwa Serikali. Watanzania wanayo tafsiri yao mbaya kuhusu sanaa nzima ya tukio la kutekwa Mo hadi kuachiwa kwake.

Suala la gari kutelekezwa na bunduki zilizokutwa, ni doa kubwa kwa Serikali. Watanzania wana akili. Walihitaji majibu sahihi na siyo majibu ya kufumbafumba na mlolongo wa longolongo.

Hivi polisi wetu wanafuatia habari za mwandishi wa habari wa Washington Post, Jamal Khashoggi aliyeuawa Oktoba 2, mwaka huu, ubalozi wa Saudi Arabia, nchini Uturuki?

Wameona picha za CCTV zilivyowaumbua majasusi wa Saudia? Jinsi jasusi anayeitwa Mustafa al-Madani, alivyovaa nguo za Kashoggi, miwani, ndevu bandia, ili aonekane ni Kashoggi. Kusudi picha za CCTV zioneshe Kashoggi alitoka salama ubalozi wa Saudia.

Mtiririko wa picha za CCTV unaonesha kila kitu. Muda ambao mashushushu waliingia, akiwemo al-Madani ambaye ni 'body double' aliyevaa mwonekano wa Kashoggi. Muda ambao Kashoggi aliingia ubalozini. Na muda ambao al-Madani alivyotoka akiwa amevaa nguo alizoingia amevaa Kashoggi, kasoro viatu. Alipovua na kwenda kuzitupa nguo za Kashoggi. Matukio na muda wote umerekodiwa.

Hivyo ndivyo CCTV hufanya kazi. Sirro na picha yake ya kupiga kwa simu, halafu anataka ikubalike, kisha anatoa vitisho. Yote hayo hayamsaidii. Ni sawa na mtu mzima kumtisha mtoto aliyejaribu kumsingizia kuwa amejamba, na mtoto mwenyewe akakataa.

Tuliseme hili kwa msisitizo; sinema ya Mo kutekwa, kutokueleweka kwa polisi na kuibuka na picha ya "Simu-Kamera" badala ya CCTV Camera, kunawafanya Watanzania waone pichapicha tu. Hawajaelewa chochote. Wanaona polisi wanajifunza sanaa kwenye jumba la sanaa.

Wangemshirikisha japo Dude wa Bongo Dar es Salaam au Ray Kigosi wangeweza kutoa muvi yenye kupunguza viulizo. Sirro aondoe vitisho. Kwa nafasi yake, anatakiwa kuisaidia nchi, kuwaunganisha wananchi na polisi, vilevile kuwafanya wananchi waliamini jeshi lao. Vitisho havitasaidia. Vitisho ni kujidhalilisha.

HII TABIA IKOME

Kumekuwa na tabia inayoshika kasi ya walio kwenye mamlaka kutotaka watu wasitoe maoni, hasa kukosoa. Sirro pia baada ya picha yake ya "Simu-Kamera" kuhusu gari lililotumika kumteka Mo kukataliwa, ametoa vitisho.

Vema kumkumbusha kwamba mwananchi ndiyo mmiliki wa nchi. Jeshi la polisi ni mali ya nchi. Sasa huwezi kumzuia mtu kutoa maoni kuhusu mali yake, au kukosoa uendeshaji wa mali yake.

Mwananchi anamchagua Rais na kumpa mamlaka ya kuiongoza nchi. Mwananchi anachagua mbunge ili aende akamsimamie na akamdhibiti Rais. Naye Rais ili atende kazi kwa mujibu wa matakwa ya mwananchi, amepewa vyombo vya kijeshi. Ndiyo maana Rais ndiye pia Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa ufafanuzi huo, maana yake majeshi yote ni mali ya mwananchi. Rais anapopewa mamlaka ya kuyasimamia majeshi, anaajiri askari ambao wanafanya kazi kuhakikisha mwenye jeshi lake (mwananchi), anaridhika.

Sasa kama mwenye jeshi (mwananchi), haridhiki kuhusu jinsi jeshi lake linavyotenda kazi, inabidi asikilizwe. Au jeshi lenyewe lijifanyie masahihisho. Kumtisha mwananchi kwenye nchi yake ni sawa na menejimenti ya kampuni kumtishia mwanahisa. Unamtisha mwenye mali?

Haya mambo ya vitisho yaachwe. Hoja ijibiwe kwa hoja. Mo alitekwa na kuachiwa. Hilo ni jambo la heri. Hata hivyo, mazingira ya kupatikana kwake yamesababisha wananchi waanze kuhisi polisi wanajifanya wameshafika Hollywood, lakini sinema zao hazifui dafu hata kwa Bongo Movie.

Inasikitisha zaidi kwa sababu nchi inasomesha watu, wamo ndani ya polisi. Lakini polisi wanaibuka na maelezo ambayo hata watoto wa chekechea wananusa harufu ya matango pori. Kisha vitisho vinafuata. Hili siyo sawa kabisa.

Vitisho vikome. Nchi ni ya mwananchi. Polisi jukumu lao ni kuratibu amani, ulinzi na usalama ndani ya mwananchi. Kama mwananchi haridhiki na uratibu, jisahihishe, siyo kumtisha. Mwananchi mwenye kujitambua hawezi kukubali kutishwa kwenye nchi yake, hasa kama hajavunja sheria. Kukataa matango pori ya polisi siyo uhalifu, ni umakini wa mwananchi.

Mo alivyoachiwa, sinema ya gari na bunduki, ni matango pori. Tunaonesha umakini wetu kuyakataa.
 
Kama kuna ' Sakata ' ambalo limemuaibisha, kumshushia Heshima IGP Simon Sirro na kuliwekea Doa ' takatifu ' na la ' kudumu ' Jeshi la Polisi Tanzania basi ni hili la ' Kutekwa ' kwa Mfanyabiashara na Bilionea Mohammed Dewji. Ni ' Sakata ' ambalo limemdhalilisha na kulidhalilisha hadi Jeshi lenyewe na Polisi / Ndata Tanzania.
 
Familia ya mo imeridhika na chai wamekunywa nyie msio na uhusiano na mbona mnahoji au kwa vile hamkukaribishwa chai
Siro yuko imara
WEWE NDIE MTEKAJI ULIETUMWA NA BABA UBAYA KAMA SIYO BURSHEETY NA SASA UMESHINDWA NA AIBU KUBWA MNAFIKIRI WATZ WA SASA NI MWAKA 1940 MNALETA PICHA ZA TECNO Y2 HALAFU MNATUDANGANYA KUWA NI ZA CCTV CAMERA LABDA HIZO CCTV ZIMETENGENEZWA KOLOMIJE
 
DHAMBI YA KUMTEKA MO HATA SHETANI AMESHINDWA KUIREKODI AMEIRUDISHA KWA WAZEE WA KOLOMIJE
 
Umesema amejamba? au amekunya?
 
Hawa wamesomea kazi zao; hata kama ni kutengeneza muvi basi wangetengeneza lenye ubora wa hali ya juu ili hata kina sisi tusiweze kunusa harufu mbaya.

Nina imani kwamba mwenyezi MUNGU akitaka kumuumbua mwanadamu anaweza kabisa; ni kukuondolea ufahamu wa fani yako kwa muda; nafikiri hiki ndicho kilichofanyika.
 
Basi tu hatuna namna tena ukitekwa ndiyo basi tena hauna Msaada.
1 police watajidai wanakutafuta kumbe kimya.
2 waziri atasema umeenda kutafuta maisha.
3 ccm watasema umejiteka tu
4 viongozi wetu watakuwa kimya wanakula kodi zetu tu.
5 ndugu zako watakuwa dhoofuli bin taabani kukutafuta na vitisho juu.
6 watanzania wenzio wataishia kusikitika tu.

Watekaji wataandika ubao wa THE END kama movie vile you are silenced
 
Ukiondoa ubavicha wewe ni waandishi bora sana.
 
Nimecheka sana hiyo Gari picha inaonyeshwa mchana vituo vyote vya tv halafu usiku inaendeshwa mpaka posta Yaani hao watekaji wa kigeni kiboko
Halafu mambo sasa anasisitiza ile alfajiri eti ni gari ile ile igp aliyoonesha Ndo imemleta watu walikuwa wanapuuza intelijensia kumbe Ndo anazidi kujamba haya majamaaaa yaende futui aisee
 
Back
Top Bottom