Tumia mbinu hii, Kupunguza gharama za ujenzi

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
Baada ya kuona watu wengi wanaumiza kichwa juu ya gharama za ujenzi, kuanzia online hadi offline, nimeona kushare uzoefu wangu nanyi ni jambo muhimu.Kabla ya kukupa mbinu , nitangulize ushauri huu. Jambo la muhimu kuliko yote la kuelewa kabla hujaanza ujenzi ni kuwa, ujenzi ni mradi endelevu kama kumsomesha mtoto kuanzia nursery hadi chuo kikuu. Kama utapiga hesabu hela zinazotumika hadi kupata degree,wengi wangeahirisha.

Mbinu yangu ni hii
Andaa template ya excel, Kama hizi ninazowaandaliaga wenzangu(zinajiupdate automatic kila siku). Kisha muone fundi muamifu akupe materials yanayohitajika kujenga jengo lako, unaweza anza na simple house,mfano vyumba vitatu. Hatua inayofuata , peleka list hii ya materials kwa hardware iliyo jirani zaidi na kiwanja unachotarajia kujenga ili kupunguza gharama za usafiri.

Mtu wa Hardware,akishajaza bei ya materials, mnakubaliana kila mwezi utalipa kiasi fulan cha pesa, mfano laki 5, ambapo utakuwa umedhibiti materials hata yakipanda bei ,wewe mkataba mlisha kubaliana bei ya zamani. Kila Yakitosha materials ya chumba kimoja,unamfuta fundi, mnapitia materials yenu, unasimamia chumba kinaisha. Kwa mtindo huu, miaka kadhaa mbele unakuwa na mradi wako na nyumba kadhaa

Uliza lolote kwa msaada.

mahmoud BOQ.PNG
k
 
Kwa hiyo inamaana unafanya malipo yote kwanza kidogo kidogo kwa kila hatua mfano ya foundation n.k

Hela ikishatimia kwa muuzaji ndiyo unachukua vifaa kupeleka site kwenda kuanza ujenzi?
Au?
 
Huu uzi unapaswa kuingizwa kwenye top 10 threads za Mwaka hata sasa!

Lakini chakushangaza wala watu hawachangii mada wala nini sijui Ndiyo kusema wamesoma na kuelewa na kwamba wanaenda kufanyia kazi au la?!

Anyways mimi nimeupenda na kuupokea kichanya!
 
Back
Top Bottom