Tumia M-Pesa at your own Risk!

Tumia M-Pesa at your own Risk!

Jidu La Mabambasi ,

Niliandika risks za kuanzisha hata biashara za m-pesa hiyo ndiyo moja wapo.

Wafanyakazi wa kampuni wanachakachua pesa za wateja kwa matumizi binafsi kisha wanasingizia kuwa network ina Shida.

Pole sana mkuu.
 
Siwatetei voda ila na wewe umepaniki bro. Soma tena vizuri meseji yako hususan kwenye hiki kipande "kurudishwa mnamo 30/10/17 saa 4.41PM". Huu uzi umeuleta hapa leo Jumanne tarehe 31, ujumbe wako unasema muamala ulifanyika jana tarehe 30 saa 10 na dakika 41 jioni.

Punguza haraka mkuu.
 
Mkuu sidhani km huwa wanasema baada ya masaa 72,huwa wanasema pesa zako zitarudishwa ndani ya saa 72 siyo baada ya masaa 72 ni ndani ya hayo masaa.

Ikumbukwe pia huyo unayeongea nae,kazi yake huwa ni kuchukua taarifa zako,kisha anatuma kwenye kitengo cha miamala. Na kesi km hizo ni nyingi sana! Ndo maana wanaweza kukuambia ndani ya saa 72 lkn ukarudishiwa muda uleule
umesoma ulichokiandika kabla ya kupost?
 
Hawa wezi siku hizi Mimi walinipa deni eti nimekopa nipige tafu wananidai 1,700 wakati hata sijui kuitumia hiyo huduma pambafu kabisa.

Kuna siku nimetoa pesa bank nataka kuzipeleka ktk namba furani ya mpesa nikakosea namba ya mwisho. Nikastuka nikampigia niliyemtumia kimakosa anaonekana ni wa kijijini kabisa nikamwambia anirudishie akasema haelewi kitu na hajaona kitu.

Nikapiga customer care wakaniambia niwatajie Namba ya muamala ya malipo. Nikakata simu nikaiandika namba ya muamala nikapiga tena nikakutana na mtu mwingine nikampa stori akasema Nipe Namba ya muamala nikamsomea baada ya kumsomea nilipomaliza ananiambia pesa zimeshatolewa.

Simu ikakatika nilivyopiga tena naambiwa umeshapiga simu mara tatu kwa siku ya leo hivyo simu yako itapelekwa wapi sijui kisha inakata sikupata tena line.

Nikajiuliza hivi wakati ananiomba Namba za muamala alikuwa haoni kuwa pesa zimeshatolewa mpaka nilipompatia hizo namba?? Hawa jamaa siku wanatia shaka sana.

Ukitaka kujua hawa jamaa sio acha pesa/salio katika simu yaani usinunue bando yaani hata kama hujapiga utakuta zinapungua tu
 
Wanasheria mliomo humu JF, hamuwezi kutushauri jinsi ya kudai damages for non rendering of service.
Mtu kutuma hela kwa mgonjwa isifike in time, akipoteza uhai si lazima iwepo kesi?
Kiongozi, tatizo kama hili likikupata tutafute tukusaidie. Karibu sana
 
mi naona tuendelee amini mabenki... sema tu watu wengi hawapigi gharama za kutoa na kutuma hela....
 
Kutuma pesa M- pesa kwenda mtandao mwingine si salama kabisa
 
umesoma ulichokiandika kabla ya kupost?
Ww ndo hujaelewa nilichoandika na ndo shida ya wengi ktk hili. Kuna tofauti kati ya baada ya masaa 72 na ndani ya saa 72. Ukisema baada ni mpaka masaa 72 yapite,lkn ndani ya saa 72,maana yake tatizo lako litatatuliwa ndani ya hayo masaa yaani hata baada ya saa 1 tu.
 
Ww ndo hujaelewa nilichoandika na ndo shida ya wengi ktk hili. Kuna tofauti kati ya baada ya masaa 72 na ndani ya saa 72. Ukisema baada ni mpaka masaa 72 yapite,lkn ndani ya saa 72,maana yake tatizo lako litatatuliwa ndani ya hayo masaa yaani hata baada ya saa 1 tu.
kwa hiyo kwa akili yako ilivyo uko tayari kuifanya shida yako isubiri hiyo saa 1 ama 72 kama unavyosema? Muda mwingine ni bora kukaa kimya kuliko kujifanya kimbelembele katika mambo ambayo yanagusa maisha ya watu.
 
Tanzania ni nchi inayoongoza Afrika kwa kutumia simu kufanya miamala..hiii Ni kwasababu wabongo wengi hawana uelewa mpna ktk hili..mitandao ya simu ktk money storage,na transactions(miamala) ni fedha nyingi sana inakatwa..so kuna unyonyaji mkubwa sanaa ktk hii mitandao ya simu,it's better to use mabank ktk miamala....
In case ukifeli kabisaa tumia simu kwa miamala...
Kuna hiii mifumo ya simu bank,hapo mabank ndo wanapiga vibaya mnooooo...makato Ni makubwa balaa,ila ndo wabongo wanaipapatikia hatar
 
M pesa ni wezi hua wanakula pesa alafu wanarudisha hizo siku nne. Kwahiyo mimi binafsi waliishanizungusha kama week hivi, na kuanzia hapo nikavunja na line Yao kabisa. Na Kwa sifa nikakopa kama 6500 , alafu nikakopa M PAWA nkavunja line
 
Ni kwa nini unasema 4:41 PM haipo?
Soma vizuri logic ninayoelezea.
Kwanza message imeingia saa8.04 mchana, ikikutaarifu kuwa saa 4.41 wamerudisha muamala.
Kiu ambacho hakipo mmana nusu saa tu kabla ya hapo niliwapigia kulalamika kwa nini muamala haujarudshwa , na wakasema wataurudisha ndani ya siku nne!!
Which means ile message ya ksema muamala umerudishwa saa 4.41 was fake!
 
Soma vizuri logic ninayoelezea.
Kwanza message imeingia saa8.04 mchana, ikikutaarifu kuwa saa 4.41 wamerudisha muamala.
Kiu ambacho hakipo mmana nusu saa tu kabla ya hapo niliwapigia kulalamika kwa nini muamala haujarudshwa , na wakasema wataurudisha ndani ya siku nne!!
Which means ile message ya ksema muamala umerudishwa saa 4.41 was fake!
Sawa ila hata system huwa zinakosea nilitaka nielewe tu hapo uliposema 4:41 PM haipo
 
Sawa ila hata system huwa zinakosea nilitaka nielewe tu hapo uliposema 4:41 PM haipo
Mkuu system haiwezi kukosea maana messaging huwa ni automatic.
Vodacom wanafikiri hizi system watu hatuzifahamu zinavyofunction.

Logic inasema hivi:
  • Nimewapigia saa 12.45( saa saba kasoro robo) mchana-kwenye screens zao bado hela hazijarudishwa, na wakanijulisha kuwa muamala utarudishwa within 4 days!
  • Napata ujumbe saa 14.04 kuwa ATI muamala umerudishwa (jana yake 30/10/2017 saa 4.41!!), kitu ambacho si kweli!!
  • Hata hivyo muamala umerudishwa muda huo wa 14.04 mchana
Nia yangu ni kuonyesha contradiction katika message hizo na actual follow up kwa simu nilizopiga namba 100, huduma kwa wateja. Na maana halisi ni kwamba kuna mfanyakazi aliyekuwa ana temper na flow ya information kuonyesha kuwa tatzo limeshughulikiwa toka jana yake wakati si kweli.
Kwa mimi mteja hi inanipa hisia kuwa kweli fedha zetu huko Mpesa haziko salam sana, pamoja na ukweli kuwa baada ya kulalamika sana ndio imeridishwa kimagumashi.
 
Wanasheria mliomo humu JF, hamuwezi kutushauri jinsi ya kudai damages for non rendering of service.
Mtu kutuma hela kwa mgonjwa isifike in time, akipoteza uhai si lazima iwepo kesi?
Mselewa anahusika hapa, mtu amtag !
 
Back
Top Bottom