nami nagongelea hapo hapo kama mhanga sugu wa transactions/miamala ya ki-elektroniki.
19.10.2017 nimenunua umeme kwaajili ya mashine ya kusaga kupitia MOBISTOCK. nikakatwa 20,000 na meseji yao ikatumwa kwamba salio limetumwa TANESCO na kwamba token zitatumiwa kwenye simu yangu.
nimezoea meseji ya arifa kuwa pesa imekatwa huambatana na ya tokeni (namba zinazojazwa kwenye mita). siku hiyo ikapita hadi zaidi ya dk 30. nikapiga simu. tena hii huduma ya mobistock unapiga simu kwa gharama halisi. sio bure km zilivyo huduma nyingine. nikajibiwa tatizo liko tanesco. kesho yake 20.10.17 nikapiga, 21.10.17 hadi 25.10.17 hadi leo hii sijapokea tokeni na salio halijarejeshwa.
wahudumu sasa wamebaki kunifokea kwamba tufanyeje sasa hali tatizo liko tanesco?
nami nahoji, nimuulize nani sasa endapo ninyi ndio watoa huduma, basi nipeni namba ya tanesco nishughulikie mwenyewe, wao hukata simu.
ebu fikirieni 20,000/= ya kununua lau 56kwh ingeshazunguka mara ngapi. imeshikiliwa kwa siku 12+ sasa.
hii ndiyo Tanzania na maisha yanasogea tu!