Baba Vladmir
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 271
- 447
Bila shaka hamjambo watu wa Mungu! Kwa wale wenye changamoto za kiafya na wanaendelea kuteseka na maumivu juu ya magonjwa waliyonayo, Mungu atawaponya.
Katika dunia ya sasa kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu wanaoishi kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu kila siku iendayo kwa Mungu,mara nyingi dawa hizo ni zile za kumeza kama vile diclopar, diclofenac, piroxam, muscle plus na nyingine nyingi.
Changamoto ya maumivu ya viungo imeongezeka sana kwa sasa ukilinganisha na zama za zamani ambapo iliwakumba sana watu wenye umri mkubwa, lakini siku hizi ni kawaida kukutana na vijana wadogo wenye shida hiyo.
Ikumbukwe kuwa kutumia dawa za maumivu haikupi kupona ugonjwa ulionao, bali ni kuendelea kuugua bila kusikia maumivu. Utumiaji wa dawa za kumeza kila siku unaweza pia kuacha madhara mengi mwilini na wakati mwingine kufanya misuli na neva za mwili kuwa tegemezi wa madawa hayo.
Basi leo ninakufundisha mchanganyo wa kawaida kabisa ambao utautumia wakati wowote utakapokuwa unasumbulia na maumivu katika sehemu ya mwili wako,hususani katika maeneo niliyoyataja hapo juu. Elimu hii ninakupa bure kabisa bila gharama yoyote, hivyo ni wewe tu kuzingatia.
Dawa hii inaandaliwa kwa mchanganyiko wa vitu vofuatavyo;
Dawa hii inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na hupunguza na kuondoa maumivu ndani ya dakika chache baada ya zoezi.Badala ya kumeza vidonge kila siku unaweza kutumia njia hii kama mbadala ili kupunguza madhara huku ukipambana kujitibu zaidi.
Mungu akupe wepesi na akuponye shida hiyo.

- Mafuta ya mzeituni( Olive oil)
- Pilipili kichaa iliyosagwa vizuri
- Ng'watya( unga wa mzizi).Hili ni jina la kibantu kwa mikoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga, Geita na Simiyu wanauelewa vyema huu mmea. Kwa wale wasioulewa ni mmea mkali ukinuswa puani, unaponusa unga wake unaweza kupiga chafya mfululizo mara kadhaa na unatumika katika tiba ya magonjwa mengi.