Tumheshimu Rais wetu Kikwete

Tumheshimu Rais wetu Kikwete

Sidhani kama ni jambo la busara sana kumvunjia heshima rais JK hadharan na kumwita majina ya ajabu

Kila mamlaka iliyowekwa imewekwa kwa makusudi ya Mungu hivyo kutoitii ni km kutomtii Mungu.

Rais Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi anahitaji heshima yetu hata kama haturidhiki na utendaji kazi wake.

Zipo njia nyingi za kumfikishia ujumbe but not going beyond na kumwita dhaifu!

Siku zote jina hutokana na matendo ya mtu. Sasa kwa matukio kama haya yafuatayo kiuanguka Jangwani mara mbili, kuanguka Mwanza, Kushindwa kuwawajibisha watendaji wake, kuwatoroka walinzi na kuingia mitaani kusaka ving'amuzi, kupenda ving'amuzi vya wenzie, kutorosha wanyama hai, safari za nje ya nchi zisizo na tija, kupenda ngoma kuliko kazi n.k. Kwa hizi sifa chache jina lipi linalo mfaa?

Sidhani kama ni jambo la busara sana kumvunjia heshima rais JK hadharan na kumwita majina ya ajabu
... kama kiongozi mkuu wa nchi anahitaji heshima...but not going beyond na kumwita dhaifu!
Siungi mkono tabia ya kumpachika majina ya ajabu Rais. Lkn ni vema tujiulize why is this? Mbona waliotangulia hawakuwa na majina ya ajabu? Nyererere aliitwa Mchonga aka Musa, Mwinyi aka Ruksa, Mkapa aka Ukapa. Kwa nini huyu yamezidi? Majina haya yanamtambulisha mtu alivyo.

ahahahhahahha kwa kipi!
kwa kiiiipi!
kiiipi nauliza!
kipi ?

aah, Kirangaaa! Umemjibu vema Bikira yeye, once you become a politician, you are exposed in every way.
Ukitenda vema utaheshimiwa, ukivuruga utadharauliwa. Mbona Dk Magufuli, pamoja na ukatili wake wa kubomoa vibanda vya walalahoi watu wanamuheshimu?

sidhani kama ni jambo la busara sana kumvunjia heshima rais jk hadharan na kumwita majina ya ajabu

kila mamlaka iliyowekwa imewekwa kwa makusudi ya mungu hivyo kutoitii ni km kutomtii mungu.

Rais kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi anahitaji heshima yetu hata kama haturidhiki na utendaji kazi wake.

Zipo njia nyingi za kumfikishia ujumbe but not going beyond na kumwita dhaifu!
mtu mzima hoooovyo!

Mwenyewe hata nguvu ya kuomba hiyo heshima hana.
Vijana wetu wanachora mazombie kwe mtihani wao wa mwisho 7 years tangu aingie madarakan af mnamuombea heshima?

Naamini kila binadamu anatakiwa kuheshimiwa!

Nchi yetu inaangamia mchana kweupe. Kama wewe ni mtanzania utakuwa unaelea kwenye behewa baharini kuleta mada kama hii hapa. Wewe mwanao akilipuliwa kama Mwangosi utasema hujaridhika hivyo unaheshimu mwuaji? Hivi ndugu yako akafanyiwa aliyofanyiwa Dr. Ulimboka utaleta upuuzi huu hapa? Vaa viata vya watoto ambao mama/baba zao wanaozea mahabusu kwa kubambikiziwa makesi. Va viatu vya mjane wa Mwangosi na wanae. Vaa viatu vya wazazi na ndugu za Dr. Ulimboka. Jiweke kwenye nafasi ya baba na mama wa Padre Evaristi Mushi. Angalia na wengine wengi tukitaja hapa jamii forum itafurika. Jamani acheni unafiki. Watanzania tufikiri mara mbilimbli udhalimu huu unaotukumba kiasi nchi yetu imepoteza kabisa heshima, utaifa, na utu wake. Kisha Kiwete mtu mzima. Loo!

Ni kweli mkuu...
"USIMSEME/USIMTUKANE VIBAYA MKUU WA WATU WAKO MBELE YA WATU ANAOWAONGOZA" ni maneno ya biblia....

Mi nadhani JK hana washauri makini, may be there is a force behind him.

Pendekeza jina unaloona wewe linamfaa kwa udhaifu wake,sisi tumempa dhaifu ww unataka aitwe nani?

Sidhani kama ni jambo la busara sana kumvunjia heshima rais JK hadharan na kumwita majina ya ajabu

Kila mamlaka iliyowekwa imewekwa kwa makusudi ya Mungu hivyo kutoitii ni km kutomtii Mungu.

Rais Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi anahitaji heshima yetu hata kama haturidhiki na utendaji kazi wake.

Zipo njia nyingi za kumfikishia ujumbe but not going beyond na kumwita dhaifu!

Wala huhitaji certificate yoyote kujua kama viongozi tulionao (Rais na Serikali yake) kwamba ni dhaifu.

Umesema kweli mkuu.Mara nyingi hata kama mtu kakosea (hata kama sio rais) njia bora ya kumkosoa ni kwa kutumia busara. Hapo ndipo anapoweza kuiona hoja yako na hata kuitafakari na ikibidi kuchukua hatua.Lakini mtu unapotumia lugha za matusi, dhihaka na kejeli; si tu kwamba unakuwa unajidhalilisha, kumdhalilisha kiongozi wako hivyo kulidhalilisha taifa lako lakini pia unasababisha hoja yako ambayo inakuwa imejificha ndani ya lugha chafu uliyoitumia kuyeyuka kama barafu.

Hii haiwezi kutokea kwa huyu raisi dhaifu, ye mwenyewe hana hata chembe busara ana maneno ya dharau na mipasho tu aheshimiwe kwa kuwa anavaa suti au?????

Sidhani kama ni jambo la busara sana kumvunjia heshima rais JK hadharan na kumwita majina ya ajabu

Kila mamlaka iliyowekwa imewekwa kwa makusudi ya Mungu hivyo kutoitii ni km kutomtii Mungu.

Rais Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi anahitaji heshima yetu hata kama haturidhiki na utendaji kazi wake.

Zipo njia nyingi za kumfikishia ujumbe but not going beyond na kumwita dhaifu!

Kumwita mbwa jina lake si kumtukana hata kidogo!!
Sasa kama JK ni dhaifu na mpuuzi kumwita hivyo si kumvunjia heshima hata kidogo!!
Ila naona kumwita kabila lake kumekuwa restricted humu jamvini kwa kuwekewa dash dash!!
JK ajiheshimu kwanza na kutimiza wajibu wake aone kama hataitwa majina ayapendayo!

Dr. Ndalichako amekuta na majibu yanayo dhihilisha hayo ya udhaifu.

Umenikumbusha mbali sana niliwahi kusoma kijitabu cha Kiswahili kinaitwa Heshima Yangu sasa nadhani na wewe ndio unakuja na the same same phrase.....

Back
Top Bottom