Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Kwenye nchi hii unaachane kumfuta machozi mtu kama Freeman Mbowe? Hata kama unamchukia kiasi gani ina maana aliyofanya na anayofanya hamuyaoni?
Freeman Mbowe hili ni jina linalopaswa kuwa kwenye kumbukumbu za kudumu nchi hii, huyu ni mpiganaji halisi hakuna vita ambayo hajawahi kushinda.
Freeman amezaliwa kwenye familia tajiri sana na yeye ni tajiri sana ila amekubali kuweka pembeni utajiri wake ili kuwazungumzia watu haki zao kwa gharama yoyote.
Ni tajiri gani angeweza ku-risk kama anavyofanya jabali Freeman? Hakuna.
Freeman amekubali kunyanyaswa, kupigwa, kutukanwa kila tusi na amekubali kupewa kesi zaidi ya 100 na kukaa jela zaidi ya mara 3 yote ili sisi wananchi tufikie nchi ya ahadi.
Hakuna utawala ambao Freeman hajateswa, hakuna ila kakubali yote hayo, tunataka nini tena?
Nawaomba tuungane kukataa mwenyekiti kuachia ngazi 2023. Simaanishi CHADEMA hakuna wa kutupeleka mbali zaidi, ila kwa kipindi hiki bado mwenyekiti Freeman tunamuhitaji sana.
Tumfute machozi Freeman, ana mengi amekubali kuteseka kwa ajili yetu.
Ninaomba wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii tuungane tumfute machozi mwenyekiti hata kwa post yoyote au hashtag inayoonyesha kazi kubwa ambayo mwenyekiti Freeman ameifanya nchi hii.
Tumsaidie Freeman kushinda uchaguzi mkuu wowote utaokuja mbele yetu.
#freeman wewe ni jabali#