Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii Aprili 20, 2023, Dkt Slaa amesema akipata nafasi ya kukutana na mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe atamshauri aachane na maridhiano kwa kuwa hayafai.
“Nikipata nafasi ya kukutana nitamwambia kwamba fuata principle za siasa safi, simamia, kwa sababu kwa sasa unatakiwa kuwapatia watanzania katiba mpya. Maridhiano hayafai” amesema
Amesisitiza, “Maridhiano hayafai kwasababu yanakaa zaidi ya mwaka, hakuna taarifa kwa wananchi. Maridhiano si mali ya Samia na ya Mbowe. Katiba inayodaiwa ni ya watanzania. Katiba si mali ya watu wawili, wala sio ya CCM na CHADEMA, ni ya watanzania. Watanzania lazima wajue wanataka katiba ya aina gani”
Dkt Slaa amesema amemsikia mara kadhaa Rais Samia akisema kuwa wataangalia katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa Rasimu ya Warioba imepitwa na wakati, yeye anasema haya ni makosa makubwa sana.
“Someni preamble pale kwenye katiba mwanzoni imeandikwa nini, imeandikwa sisi watanzania tumeamua, kwenye katiba”
Kuhusu kusubiria uteuzi, amesema kwa umri wake hasubirii tena fursa hiyo, pia amemsfia Freeman Mbowe kuwa mwanasiasa mzuri, mkonge na mpambanaji wa siku nyingi.
Chanzo: East Africa Radio