Tumfute machozi Freeman Mbowe, tusikubali aachie uenyekiti 2023. Ametupigania sana

Kwenye nchi hii unaachane kumfuta machozi mtu kama Freeman Mbowe? Hata kama unamchukia kiasi gani ina maana aliyofanya na anayofanya hamuyaoni?

Freeman Mbowe hili ni jina linalopaswa kuwa kwenye kumbukumbu za kudumu nchi hii, huyu ni mpiganaji halisi hakuna vita ambayo hajawahi kushinda.

Freeman amezaliwa kwenye familia tajiri sana na yeye ni tajiri sana ila amekubali kuweka pembeni utajiri wake ili kuwazungumzia watu haki zao kwa gharama yoyote.

Ni tajiri gani angeweza ku-risk kama anavyofanya jabali Freeman? Hakuna.

Freeman amekubali kunyanyaswa, kupigwa, kutukanwa kila tusi na amekubali kupewa kesi zaidi ya 100 na kukaa jela zaidi ya mara 3 yote ili sisi wananchi tufikie nchi ya ahadi.

Hakuna utawala ambao Freeman hajateswa, hakuna ila kakubali yote hayo, tunataka nini tena?

Nawaomba tuungane kukataa mwenyekiti kuachia ngazi 2023. Simaanishi CHADEMA hakuna wa kutupeleka mbali zaidi, ila kwa kipindi hiki bado mwenyekiti Freeman tunamuhitaji sana.

Tumfute machozi Freeman, ana mengi amekubali kuteseka kwa ajili yetu.

Ninaomba wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii tuungane tumfute machozi mwenyekiti hata kwa post yoyote au hashtag inayoonyesha kazi kubwa ambayo mwenyekiti Freeman ameifanya nchi hii.

Tumsaidie Freeman kushinda uchaguzi mkuu wowote utaokuja mbele yetu.

#freeman wewe ni jabali#
Napata tabu Sana kuona watu hawamuelewi huyu Mjasiriamali was KISIASA.
Huyu ndiye anayekidai chama mabilion kila uchaguzi kwa kupokea na kutoa michango na Kisha kufanya matumizi bila vielelezo.
Huyu ndiye anayeuza majimbo kwa kutosimika wagombea kwenye baadhi ya maeneo mfano kule kwa nimrod mkono.
Huyu ndiye anayekula michango ya kina sabodo na matajiri wengine, anakula hela za wafadhili toka vyama washirika kule ulaya, anaweka dada zake mahawara na Ndugu zake na wa jamaa zake kuwa Wabunge wa viti maalum kwa upendeleo(nilisikia wale covid-19 waliamua kujiteua kwa sababu hii), anachangisha Wabunge na baadae kusepa na hela zote mfano mzuri zile 4bln za mwaka jana wakati viti maalum walichangishwa 1.5mlper month na wa majimbo 0.5ml per month na mwisho wa siku baada ya kuzikusanya kwa miaka 5 yaani miezi 60 zikayeyuka.
Huyu ndiye anaetoa kafara waandamizi wake kila mwaka kuanzia kwa Aman Walid Kabourou, Chacha Wangwe, Zitto Kabwe, Said Arf. Prof Safari, Dr. Slaa,kina Kitila, kafulila na wengine kibao.
Mimi namfananisha Mbowe na Mwl. Nyerere aliyeijenga nchi na ikamfia akiwa bado madarakani hata alipoamua kung'atuka kila kitu kilikuwa kimeisha. Ndio huyu Mbowe wako... mafanikio yote aliyopata kutoka kupata Kura 5%-39% za Urais mpaka Sasa anaporomoka, Lisu aliambulia 12 sijui...!!! Nafikiri next election itakuwa Kura za Membe. Upande wa ubunde ndio balaa kutoka 35 mpka 1. Na Sasa anaogopa hata kukiingiza chama kwenye uchaguzi ili udhaifu usionekane. Au Kuna mtu kasahau kwamba Wabunge 16 hivi walihama na madiwani zaisi ya 200.
Keyboard warriors waliimbishwa eti tumeibiwa juzi kati katoa majibu kwamba walishindwa uchaguzi kwa kuwa;
1. Hawakuwa na POTENTIAL CANDIDATES
2. CDM haina mtandao mpaka vjjn Kama CCM Sasa(suluhisho ni kwenda kijijini kusajili wanachama kidigitali kwa watu ambao bado wanaishi kianalojia).. Yale Yale ya Lowasa kushindwa kunadi sera jukwaani akasema watu wakaisome kwenye website ya Chama..
Nacheka Sana kwa kweli tumuongeze miaka mingine 20 haina shida
Makamanda eeeeeh
Peeeeeeeeeeople'ssssssssssss
 
Kwenye nchi hii unaachane kumfuta machozi mtu kama Freeman Mbowe? Hata kama unamchukia kiasi gani ina maana aliyofanya na anayofanya hamuyaoni?

Freeman Mbowe hili ni jina linalopaswa kuwa kwenye kumbukumbu za kudumu nchi hii, huyu ni mpiganaji halisi hakuna vita ambayo hajawahi kushinda.

Freeman amezaliwa kwenye familia tajiri sana na yeye ni tajiri sana ila amekubali kuweka pembeni utajiri wake ili kuwazungumzia watu haki zao kwa gharama yoyote.

Ni tajiri gani angeweza ku-risk kama anavyofanya jabali Freeman? Hakuna.

Freeman amekubali kunyanyaswa, kupigwa, kutukanwa kila tusi na amekubali kupewa kesi zaidi ya 100 na kukaa jela zaidi ya mara 3 yote ili sisi wananchi tufikie nchi ya ahadi.

Hakuna utawala ambao Freeman hajateswa, hakuna ila kakubali yote hayo, tunataka nini tena?

Nawaomba tuungane kukataa mwenyekiti kuachia ngazi 2023. Simaanishi CHADEMA hakuna wa kutupeleka mbali zaidi, ila kwa kipindi hiki bado mwenyekiti Freeman tunamuhitaji sana.

Tumfute machozi Freeman, ana mengi amekubali kuteseka kwa ajili yetu.

Ninaomba wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii tuungane tumfute machozi mwenyekiti hata kwa post yoyote au hashtag inayoonyesha kazi kubwa ambayo mwenyekiti Freeman ameifanya nchi hii.

Tumsaidie Freeman kushinda uchaguzi mkuu wowote utaokuja mbele yetu.

#freeman wewe ni jabali#
Freeman Mbowe ana kitu chake pale mbele Paradiso
 
Hapana, kama ni kufutwa machozi itafutwe njia nyingine ya kumfuta hayo machozi, lakini kuhusu kupumzika, nashauri aachwe apumzike, yeye ndie ameamua kufanya hivyo japo anajua bado anaungwa sana mkono na wapenda mabadiliko, msiogope, iacheni Chadema iende phase nyingine, hakuna chenye mwanzo kikakosa mwisho, kama tunaogopa mabadiliko hivi basi bora CCM iendelee kututawala.

hizi znaitwa WISDOM!!!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom