Freeman Mbowe ndiye Mwanasiasa aliyejadiliwa zaidi kwenye Eneo la Maziwa Makuu 2023 , Umaarufu wake waongezeka mara dufu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,770
218,389
JamiiForums1267461471_387x387.jpeg

Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , Yule Mwamba wa siasa za Kisasa kwenye eneo la Maziwa Makuu , Freeman Mbowe , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa zaidi na kinachoungwa mkono na wananchi wengi zaidi Nchini Tanzania , anatajwa kuwa ndiye Kiongozi wa Kisiasa aliyejadiliwa zaidi kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu kwa Mwaka 2023 , akiwaacha Mbali wanaomfuatia , Rais wa DRC Tshishekedi na Dikteta Paul Kagame wa Rwanda

Magwiji wa siasa kwenye eneo hilo wanataja sababu kuu ya mtu huyu ambaye pia anajulikana kama Ustaadh Aboubakar Mbowe kujizolea umaarufu huu , ni pamoja na Karama ya Ushawishi aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu , huku jambo kubwa lingine likiwa ni kukisimika chama chake Nchi nzima , vikiwemo vijiji vya Dodoma na Ruvuma, ambavyo kwa miaka mingi viliamini kwamba CCM ni kama dini na kwamba ukiiacha ni sawa na kutenda dhambi

Msimamo wake katika Kupigania haki kwenye Nchi yake , ndio nguzo kuu ya Imani ya Wananchi kwake binafsi na kwa Chama chake , Matajiri wengi wa Tanzania na nchi nyingi za kiafrica hujiambatanisha na Watawala kwenye ukandamizaji wa Raia , Wananchi wanashangaa imekuwaje Bilionea Mbowe yeye yuko na Wananchi tu badala ya kushirikiana na watawala kunyonya rasilimali za Taifa .
 
Warumi 10
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
 
Kuna hili suala la nusu mkate ndugu Erythrocyte . Ni kweli kwamba kwenye maridhiano chadema wamekubali kuachiwa baadhi ya majimbo kwenye uchaguzi mkuu ujao?
Hakuna maridhiano kati ya Chadema na ccm , maridhiano yalishavunjika , hata hivyo kwa kadri ninavyofahamu kwenye karatatasi ya ajenda zilizojadiliwa sikuliona la nusu mkate
 
Chawa kazini 🤣🤣🤣

Naona Lucas Mwashambwa umerudi katika ID yako ya kawaida.

Kwa hali ilivyo sasa hivi, haishangazi mtu kujaribu kutumia jiwa moja kuua ndege wawili, ili familia ipate mboga ya kulia ugali 🤣🤣
 
Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    11.9 KB · Views: 3
View attachment 2862650

Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , Yule Mwamba wa siasa za Kisasa kwenye eneo la Maziwa Makuu , Freeman Mbowe , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa zaidi na kinachoungwa mkono na wananchi wengi zaidi Nchini Tanzania , anatajwa kuwa ndiye Kiongozi wa Kisiasa aliyejadiliwa zaidi kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu kwa Mwaka 2023 , akiwaacha Mbali wanaomfuatia , Rais wa DRC Tshishekedi na Dikteta Paul Kagame wa Rwanda

Magwiji wa siasa kwenye eneo hilo wanataja sababu kuu ya mtu huyu ambaye pia anajulikana kama Ustaadh Aboubakar Mbowe kujizolea umaarufu huu , ni pamoja na Karama ya Ushawishi aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu , huku jambo kubwa lingine likiwa ni kukisimika chama chake Nchi nzima , vikiwemo vijiji vya Dodoma na Ruvuma, ambavyo kwa miaka mingi viliamini kwamba CCM ni kama dini na kwamba ukiiacha ni sawa na kutenda dhambi

Msimamo wake katika Kupigania haki kwenye Nchi yake , ndio nguzo kuu ya Imani ya Wananchi kwake binafsi na kwa Chama chake , Matajiri wengi wa Tanzania na nchi nyingi za kiafrica hujiambatanisha na Watawala kwenye ukandamizaji wa Rais , Wananchi wanashangaa imekuwaje Bilionea Mbowe yeye yuko na Wananchi tu badala ya kushirikiana na watawala kunyonya rasilimali za Taifa .
Usitudanganye wewe, mtu ambaye hapa nchini hata watoto hawamjui ndo ajadiliwe maziwa makuu, kwenda zako bana, imagine enzi za Magufuli, kitoto Cha miaka mi4 ukikionyesha picha kinakwambia Magufuli, Mbowe nani anamjua, ungesema angalau Julius Malema basi... Mnalipwaga shingapi aisee? Au we ni kijana wake, au ndo Mbowe mwenyewe
 
Kunifananisha mimi na Mwashambwa ni sawa na kunitukana matusi ya nguoni , ni bora utafute matusi mengine tu mkuu
Sifa zenu zinafanana. Wote mnasifu na kuabudu watu.

Wewe kwa mwaka unamsifu mwenyekiti Mbowe zaidi mara kibao, halikadhalika na yeye anamsifu raisi Samia mara kibao. So kwa sisi wafuatiliaji wa thread zenu hapa jukwaani tunaona kuwa there's no different between you and him mkuu.
 
Usitudanganye wewe, mtu ambaye hapa nchini hata watoto hawamjui ndo ajadiliwe maziwa makuu, kwenda zako bana, imagine enzi za Magufuli, kitoto Cha miaka mi4 ukikionyesha picha kinakwambia Magufuli, Mbowe nani anamju, ungesema angalau Julius Malema basi... Mnalipwaga shingapi aisee? Au we ni kijana wake, au ndo Mbowe mwenyewe
Magufuli alishakufa na malema hayuko kwenye eneo la maziwa makuu
 
labda kama umeng'olewa ubongo , Mwashambwa ni mwandishi wa Tulia na Samia tu , si mwandishi wa ccm , mimi ni mchambuzi wa siasa na mwandishi wa habari zote za kisiasa
Endelea kujisahaulisha mkuu, lkn nina imani moyo unakusuta kwa kuukwepa ukweli.
 
Uliposema eneo la "maziwa" makuu nikahisi mjadala huo aliongoza Joyce Mukya faraghani
 
Back
Top Bottom