Tumfanyeje Lowassa?

Tumfanyeje Lowassa?

We unafikiri alipoenda kule nigeria kwa TB Joshua,alienda kuuza sura? Kazi ndiyo hiyo sasa imeanza mpaka mtavua magwanda muanze kuvaa maovaroli,
 
Kigarama na Wana JF,
Wananchi ndio wenye MAMLAKA aka wenye Uamuzi wa mwisho.
Nawakilisha.

Kwenye mijadala 100 ya kwenye jukwaa hili amini usiamini mijadala 98 ndani yake halikosi kutajwa jina la Edward Lowassa kwa mema, mabaya kwa kuungwa mkono au kwa kupingwa. Lowassa imethibitika kuwa ndiye nguzo ya siasa zetu hapa Tanzania. Ukimshambulia au kumsifia Lowassa ni lazima utavuta hisia (attention) za jamii ziwe chanya au hasi dhidi yako.

Leo hii Lowassa akiacha siasa kitakachofuatia ni mjadala mwingine kama aachwe apumzike au ashitakiwe. Ndani ya CCM makundi yanayotajwa ni ama wanaomuunga mkono Lowassa au wanaompinga, na nje ya CCM mwanasiasa anayetajwa kama atashindwa kirahisi au atawashinda wapinzani wake ni Lowassa. Inavyoonekana kwenye siasa za Tanzania kumuepuka Lowassa haiwezekani.

Lakini kama taifa tunatakiwa tutoke kwenye mkwamo huu wa jinamizi la Lowassa, kwani kwa hali ilivyo sasa inaonekana kama vile Lowassa ni "Control Machine" ya maisha yetu ya kisiasa. Tuamue kushughulika na Lowassa leo na milele (once for all) ili tubakie na kazi ya kuijenga nchi yetu.

Haiwezekani ionekane kama kwa nchi nzima Lowassa anao uwezo wa kufanya chochote halafu sisi kama taifa tunabaki kumwangalia, kulalamika na kuwayawaya kama swala aliyekoswakoswa na simba. Kama analimiki bunge, mahakama, Serikali na chama chake basi asitumiliki na tusiofaidika na mfumo aliouweka.

Kama hatuna cha kumfanya Lowassa basi tujue huko tuendako kama taifa hatuna heri hata kidogo!!
 
lowasa anafaa kabisa kua rais anawafahamu viongozi wote na tamaa zao za kula mali ya uma.
 
Amemfanya nini Mwakyembe?
Lowasa hastahili kuwa raisi japo anajua na ni jasiri kuongoza hii inatokana na kupenda kwake visa na visasi kitendo cha kumfanya vile mwakyembe sidhani iwapo atakua rais mbeya itaendelea kuwa sehemu ya Tanzania!!!Alafu atamshinda nani maana anaogopwa kama ukoma labda apindue nchi
 
Hatupaswi kumchukia EL,tuichukie ccm huku naye akiwa ndani kwani mnategemea kusikia neno UFISADI kutoka kwenye vinywa vya Karamagi,Lowassa,Chenge,Mr.President,Nape,Shiggela n.k
 
kama kweli anautaka uraisi................ aondoke CCM ajiunge na M4C akiwa zigo la lawama kalitupa kwa JK hapo ataaminika tena na wabongo watamsamehe na kumpa umagogoni!!!Komaa lowasa my school mate pale Tabora...."
Laaaaah! Kwa hiyo akienda CHADEMA,uchafu wote anaotuhumiwa,atakuwa amesafishwa?
 
Laaaaah! Kwa hiyo akienda CHADEMA,uchafu wote anaotuhumiwa,atakuwa amesafishwa?
Kwa hoja hii inavyoonekana hakuna cha kumfanya Lowassa. Kama Lowassa leo akisema Richmond na mauzauza mengine ni zao la Kikwete na yeye kutoka CCM na kwenda CHADEMA basi anakuwa msafi basi hakuna tofauti na alivyo sasa. Mimi swali langu ni kwamba ama tukubali kwenda na Lowassa kwenye siasa zetu awe rais au asiwe rais au tumuondoe hivi sasa kabla ya mwaka 2015.

Sote tunaimani kwamba Urais wa Kikwete ni zao la kazi ya Lowassa. Kwa hiyo hapa hoja siyo kama Lowassa agombee Urais au asigombee bali lazima tuione nguvu ya Lowassa kwenye siasa zetu za kila siku. Kwenye Kampeni za Arumeru Lowassa alikuwa anashindana na watu walio ndani ya chama chake na CHADEMA, lakini ukweli wa mambo pamoja na nguvu nyingi zilizotumika kupambana naye mwisho wa siku Mkwewe alishindwa kwa heshima.

Mtu anayetaka tuamini kwamba Lowassa hana nguvu za kisiasa kwenye medani hiyo hapa Tanzania anataka kujifurahisha yeye mwenyewe na kutughilibu sisi. Kama hatuwezi kumshitaki mahakamani na hatuwezi kushitaki kwenye mahakama ya Umma, basi Lowassa ataamua nani awe mshindi mwaka 2015!!
 
Kwenye mijadala 100 ya kwenye jukwaa hili amini usiamini mijadala 98 ndani yake halikosi kutajwa jina la Edward Lowassa kwa mema, mabaya kwa kuungwa mkono au kwa kupingwa. Lowassa imethibitika kuwa ndiye nguzo ya siasa zetu hapa Tanzania. Ukimshambulia au kumsifia Lowassa ni lazima utavuta hisia (attention) za jamii ziwe chanya au hasi dhidi yako.

Leo hii Lowassa akiacha siasa kitakachofuatia ni mjadala mwingine kama aachwe apumzike au ashitakiwe. Ndani ya CCM makundi yanayotajwa ni ama wanaomuunga mkono Lowassa au wanaompinga, na nje ya CCM mwanasiasa anayetajwa kama atashindwa kirahisi au atawashinda wapinzani wake ni Lowassa. Inavyoonekana kwenye siasa za Tanzania kumuepuka Lowassa haiwezekani.

Lakini kama taifa tunatakiwa tutoke kwenye mkwamo huu wa jinamizi la Lowassa, kwani kwa hali ilivyo sasa inaonekana kama vile Lowassa ni "Control Machine" ya maisha yetu ya kisiasa. Tuamue kushughulika na Lowassa leo na milele (once for all) ili tubakie na kazi ya kuijenga nchi yetu.

Haiwezekani ionekane kama kwa nchi nzima Lowassa anao uwezo wa kufanya chochote halafu sisi kama taifa tunabaki kumwangalia, kulalamika na kuwayawaya kama swala aliyekoswakoswa na simba. Kama analimiki bunge, mahakama, Serikali na chama chake basi asitumiliki na tusiofaidika na mfumo aliouweka.

Kama hatuna cha kumfanya Lowassa basi tujue huko tuendako kama taifa hatuna heri hata kidogo!!

Kwanza wewe hujui Maana na uwezo wa DEMOCRACY.

Pili hujui unachotaka kuandika. Kwa upande mmoja unaandika kuwa mtu hatari ni lazima ashughulikiwe, na kwa upande mwingine unaandika mtu hatari tumuache tu abomoe tusimjali, sisi tuendelee kujenga nchi yetu. Sikuelewi.

Sehemu kubwa ya Demokrasia ni uhuru wa kusema. Namshukuru Mungu kuwa uhuru huu Tanzania tunao kupitia njia zote za mawasiliano, toka simu, radio, tv mpaka hapa mtandaoni. Na watanzania tunaitumia vizuri sana nafasi hii ikiwa ni pamoja na kumueleza Mh LOWASA ni nani? Nguvu yake kisiasa iko katika kipimo gani? Uwezo wake wa kipesa uko vipi? Nia yake ya kusonga mbele kushika nafasi za kisiasa ziko vipi? Je ana uwezo katika nafasi hizo? Je ana nia ya kuleta maendeleo kwa Tanzania au kuharibu?

Maswali haya yote ni maswali muhimu sana kwa maisha yetu na vizazi vijavyo. Watanzania wametumia na wataendelea kutumia nafasi hii ya kidemokrasia kujadili, kuyaweka wazi na kuhoji maswali haya katika vyombo vyote vya habari. Hakuna kosa katika hili, na binafsi nawashukuru wote waliopoteza wakati wao kumjadili Mh LOWASA.

Aidha mtoa maada anaandika: "Kama hatuna cha kumfanya Lowassa basi tujue huko tuendako kama taifa hatuna heri hata kidogo!!" Hapa sijamuele, hivi anachohitaji tumpige risasa, tumtie uchizi au tumuweke kizuizini? Naomba maelezo hivi anatarajia watanzania tumfanye nini? Ninachokielewa mimi kueleza mabaya ya LOWASA na watanzania wote wakamuelewa ndio silaha kubwa ya kumuengua LOWASA toka katika uwanja wa siasa kama unaamini kuwa hafai. Ama ukiamini kuwa anafaa ni kueleza mazuri yake ili kumpandisha. Cha msingi ni kuuelimisha Uma, pindi ukielewa ndio kura za masanduku zitaamua.

Kwa maana hiyo siungani mkono nawe. Isitoshe unasahau kuwa huyu mtu ameshawahi kuchukua fomu ya kugombea urais huko nyuma, ameshashika nafasi nzito za kisiasa mbali mbali ikiwemo pamoja na uwaziri mkuu. Hivyo kumjadili kisiasa ni jambo la muhimu. Zaidi ya hayo katika uwanja wa siasa si yeye tu anayejadiliwa kuna akina Mh Slaa, Mh Zitto Kabwe, Mh Sumaye n.k

Mwisho natoa PONGEZI KWA
WOTE wanaomjadili na endeleeni kutumia nafasi hii ya kidemokrasia na wapuuzeni wote wanaofikiri eti kumjadili LOWASA ni kosa.
 
Lowasa ndiye mwanaccm aliyebaki mwenye uwezo wa kuipeleka tanzania kwenye maendeleo ya kweli wengne ni funika kombe mwanaharamu apte...lowasa ni jasri,ni mtendaji na anapenda maendeleo
 
Lowasa hauski na magonjwa ya watu acheni kuhukumu mtalaaniwa..sita kashazeeka msisklize
 
Misaada ya mamilioni ya pesa kwa makanisa anayatoa wapi yeye kama mtumishi wa umma?

Fuatilia kwa makini mamilioni hayo huwa yanatoka wapi. EL ni fundraiser mzuri, hela hazitoki mfukoni mwake, hizi ni harambee. Tofauti, lets say na JK aliechota EPA au Sumaye aliechota NSSF.
 
He will be the best president ever for Tanzania
 
Tususie kuandika taarifa zake zote nzuri ila tumuandame kwa kufichua maovu yake yote ikiwamo kutumiwa na usa ili akiingia madarakani aaendelee kuhujum nchi kwa kuwafavour wamarekan
 
Kwaheri mafisadi!!!!!!!!!!!!!!Never discuss about people for cheap popularity
 
Kwanza wewe hujui Maana na uwezo wa DEMOCRACY.
Sikuelewi.

Demokrasia haina ukiritimba wa uelewa ukiona unadhani tafsiri ya Demkrasia unayo wewe wenzio hawana, jua wewe una chembechembe za udikteta ambao tafsiri ya mambo hutoka kwao pekee na wao tu ndiyo wajuao. Tafsiri ya Demokrasia haina hatimiliki.

Na ukijiona huelewi ujue kwamba hauko mbali sana na kuelewa!!
 
Lowasa ndiye mwanaccm aliyebaki mwenye uwezo wa kuipeleka tanzania kwenye maendeleo ya kweli wengne ni funika kombe mwanaharamu apte...lowasa ni jasri,ni mtendaji na anapenda maendeleo

..............mlipokuwa mnampigia debe Kikwete 'maisha bora kwa kila mtanzania' ilikuwa ni uongo ambao mnaujua kuwa ni uongo !?
Je, huo wa Lawasa sio uongo mwingine ?
 
EPA,richmond na zingine zote ilikua kwa kazi ya uchaguzi, hakula lowasa. Amebeba mzigo kwa makubaliano.

Alafu yeye toka aachie ngazi hajapiga madili kama wenzake walivoziendeleza na mzee mzima bado anapiga michongo hadi leo
 
Kimya kingi kina mshindo mkuu na ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria mh. Lowassa katika siasa ya nchi hii rekodi yake ni mzuri sana hasa katika uwajibikaji na hii ilijionesha dhahili alipojiuzu wadhafa wake kwa maslai ya nchi kwa wakati ule ambao serikali hii ya awamu ya nne ilikuwa bado changa.Katika hilo alionesha ujasiri wa hali ya juu sana,actually is very intelligent katika hili tusibishe kabisa maana angelikuwa mpumbavu angelopokalopoka tu hovyo ama kulaumulaumu tu huku na kule lakini wapi.Tukiachilia masuala ya ukanda,dini,kabila na rangi Mh.Lowassa he may be a good leader for future Tanzania we need,kwani aliyeumwa na nyoka akiguswa na jani tu lazima astuke so kwa yote wanayodhania kumtuhumu Mh.Lowassa katika awamu yake no body can corrupt public funds na hata wale watumishi wezi wote watakimbia ama kuogopa kufanya kazi za umma.Nia hayo tu.
Katka kfungua kampein za CDM, Marando alisema wezi wa EPA wakuu ni RA, JK na EL. Aliwataka wampeleke mahakamani. Mpaka leo hakuna aliyekwenda mahakamani. Hiyo inaonyesha kuwa hawa jamaa ni wezi wa kutupwa. Walikubaliana na madai ya Marando ndio maana wakanyamaza.
 
Back
Top Bottom