Tumfanyaje huyu dogo?

Tumfanyaje huyu dogo?

MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2014
Posts
2,118
Reaction score
2,198
Undugu wa damu ungekuwa unakatizwa nadhani ningekuwa wa kwanza kuomba huduma hiyo. Wadau huyu dogo nahisi ni adhabu tuliyoachiwa na marehemu wazazi (sijui tulikosa nini).

Naomba mjaribu kunisaidia mawazo aisee.

Huyu dogo alipomaliza form 4 (kwa mbinde) hakufanya vizuri sana akajiunga na jeshi la polisi, hakumaliza akatimuliwa huko CCP.

Kuna mzee mmoja rafiki wa marehemu mzee akatufanyia mpango dogo akaingia jwtz, dogo akaenda akakimbia depo aftr several weeks.

Akaja home, akatafutiwa kazi tanesco akafanya kazi siku mbili. Tukashauriana kwamba aende veta nako akafukuzwa vile vile kwa vurugu.

Hakuna ambacho hatujajaribu kwa huyu kiumbe na kuna bro kawahi kumuweka asimamie mradi mmoja hivi kaharibu.

Akiachwa hivi hivi anakuwa ni kero tupu, hapo home kashauza kila chenye maana.

Akija kwa kaka zake ndio ugomvi kila siku cheni, simu na vipochi vya shemeji zake haviponi.

Kesi za kutapeli kila siku.

Tumewaza hadi tunakaribia kukufuru waungwana.
 
achana naye...time will tell!kuna umri utafikia atashituka na kujua kachezea...hapo atatulia mwenyewe!japo asipokuwa makini akishapata uzoefu wa kuchukua vya nyumbani atahamia mtaani hapo ndo atakapojua kuwa anayo yafanya hayakubaliki
 
Mnamwendekeza mnamwendekeza ndiio maana anawasumbua.
 
Halafu inavyoonekana hamjawahi kumuadhibu hata kidogo huyo, siku nyingne akifanya vikosa vidogo vidogo vyenye kifungo kidogo mnamuacha tu akale kozi ya uraia wema gerezani.
 
Huyo dogo mwacheni kwanza life impige ban mwenyewe atapata akili, mara nyingi madogo wenye uhakika wa kula milo mitatu na kulala bila masimango huwa wana matatizo sana. Alivyo haribu CCP militakiwa muachane nae kabisa mpaka pale atakapopata akili na kuja na wazo lake mwenyewe la anataka nini na tena akija msiwe wepesi wa kutoa support mpaka pale mtakaporidhika na ikiwezekana muulizeni yeye ana nini katika hicho kitu anachofanya.

Msiogope hawezi kufa kwa shida kama mkimtosa maana mbona wengi tu wameishi maisha ya dhiki wakatoka (SHIDA NI KIPIMO CHA AKILI)
 
Huyo dogo mnamwendekeza mwacheni dunia imfundishe
 
Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi,yaani kachezea nafasi zote hizo mwacheni walimwengu wamfunze.
 
Wahenga walikua sio wajinga kusema "Penye mitu hapana wajenzi" nafasi ambazo watu wanalilia na kusubutu hadi kuhonga fedha yeye kazichezea! Kama ajapigwa kiberiti huyo kwa wizi basi ataweza olewa kwa kupenda mtelemko pumbav kabisa. Mimi huwa natoa kipigo tu kwa watu kama hao.
 
Huyo dogo muacheni kama alivyo kwani dunia itamfundisha, hii issue ni kama copy and paste ya mdogo wangu mmoja hivi ila nae kwa sasa yupo jela huu ni kama mwezi wa saba sasa na ameshaanza pata ufahamu na kujuta!
Muacheni dunia itamfundisha!

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tafuta kituo cha polisi karibu peleka ale kiboko week nzima
 
Kabla hajachomwa moto ni vizuri mkafanya hiv:
mpelekeni kwa wataalam wa saikolojia ili wamchunguze na kumpa ushauri unaofaa.
mkiona hakuna mabadiliko, msiwe na huruma naye, hakikisheni mnamuweka ndani (jela) kwa muda wa kutosha.
mwelezen huyo dada yenu kuwa anachokifanya kumtoa jela kila mara hamsaidii bali anamjengea mazingira hatarishi ya kuuwawa. tambuen kama nyiny mtamuonea huruma lkn ipo jamii ambayo haitamhurumia.
mchague akatulie jela sehemu ambayo atakuwa hai huku akirekebishwa au mumchekelee na kumuona akifanya fujo mitaan mkisubiria achomwe moto.
 
Na huo ndio ushauri wangu. Watamkosa huyo dogo soon
 
achana naye...time will tell!kuna umri utafikia atashituka na kujua kachezea...hapo atatulia mwenyewe!japo asipokuwa makini akishapata uzoefu wa kuchukua vya nyumbani atahamia mtaani hapo ndo atakapojua kuwa anayo yafanya hayakubaliki

mwacheni jamii itamgawana sio muda mrefu. chezea wananchi wenye hasira kali wewe.
 
Back
Top Bottom