Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,103
- 828,988
Kesho tarehe 10.01.2018 inaweza kuwa siku nyingine mbaya kwa wale wapenda wabadiliko. Kesho kuna kulia ama kucheka kama ni kweli kutakuwa na mkutano Serena hotel.
Mchana wote wa leo mpaka mida hii huku mitandaoni hakufai ni mitifuano na speculations za kila aina kuhusu siku ya kesho na kile kitachasemwa. Kila upande umejiandaa vilivyo na madongo ama vilio ama shangwe za kutosha.
Kama ilivyo kwa mechi ngumu za Simba na Yanga kila upande Unahitaji ushindi. Chochote kitakachotokea kesho kitakuwa na hasara kubwa kwa upande mmojawapo.
Kama hahami furaha shangwe nderemo na vifijo vitakuwa vingi mno... Nchi italipuka kwa kushangilia. Na wale wa upande wa pili watakuwa wamepigwa mweleka mkubwa.
LAKINI ikitokea akasema anahama au hata kusema anastaafu harakati upande wa pili patakuwa hapatoshi japo si kwa kushangilia sana bali vijembe na dhihaka kwa wingi wake.
Huku kwingine kutakuwa ni simanzi kubwa na nchi itakuwa kama iko msibani
Kuna viashiria vya kutisha kidogo.
-Kwanini kaenda peke yake? Pengine ni haki yake
-Kwanini hakushirikisha viongozi wenzake? Kizungumkuti kiko hapa
-Alichoongea mbona kinapingana na uhalisia? Ngoja tutaona...
Itoshe tu kuamini kwamba hatatonesha makovu ya vidonda vinavyopona.. Hatasahau fadhila. Hatawageuka wale wote waliompenda na kumwamini sana.
Hatawavunja moyo na kuwaumiza kihisia wale wote walioumia na kuumizwa kwa ajili yake.
Inawezekana kabisa ukawa ni mwanzo mpya wa kutufanya tusonge mbele pale tulipokwamishwa.