Tunatambua Juhudi zenu. Mnayo dhamira ya kweli, mnayo dhamira ya Dhati na Mna Uchungu sana na Ukombozi wa Taifa hili kutoka mikononi na mifukoni mwa Wasio waadilifu. Mungu anajua. Hata kama Mtapigwa, hata kama mtadhalilishwa kwa kiasi gani sisi hatutawasaliti. Tunajisikia vibaya sana tunapoona mnadhalilishwa, mnanyimwa haki Bungeni na Kukaripiwa kama watoto wadogo. Lakini tunatambua kwamba haya yote yatapita. Ipo siku na si mbali, hawa wanaowatendea haya watapiga magoti mbele zenu. Msikate tamaa kwa haya yanayotokea, maana kila jambo jema na mafanikio makubwa hupatikana kwa jasho jingi sana au hata wakati mwingine kwa maumivu makali sana. Sisi tuko pamoja nanyi katika kila hatua. Kumbukeni YESU alidhalilishwa, akapigwa mijaledi, akatemewa mate, wakamdhihaki, lakini mwishowe akawa mshindi na sasa kila goti hupigwa mbele zake. Hata Mtume S.A.W naye bila shaka alipitia mazingira magumu ili watu waweze kumweelewa, wapo walio mpinga lakini leo wanaheshimu harakati zake. Mhe. Joseph Mbilinyi alidhalilishwa sana na polisi wa Bungeni, Mhe. Mbowe alidhalilishwa sana kwa kauli za Ndugai. Kwa ujumla wabunge wote wa upinzani walidhalilishwa sana. Wabunge wa CCM walionekana kufurahi sana. Nataka niwambie, Wabunge wa CCM achaneni na akili za kufikiri na kuishia ndani ya ukumbi wa Bunge. Hao mnaowadharau leo kesho wanaweza kuwa viongozi wenu. Tatizo lenu hamjitambui. Hawa mnaowaona wabaya wanapigania haki yenu, watoto wenu na wajukuu wenu. Jitambueni, acheni ushaabiki wa kijinga. Fikirieni mstakabali wa Taifa hili kwa ajili ya watoto wenu. Mungu ibariki Tanzania. Mungu wasaidie Wabunge wa CCM wawe na ufahamu, kwani wamepoteza fahamu, busara na hekima kwa sababu ya kulewa na madaraka.