Tumeridhika masuala ya vijana kuhamishiwa wizara ya habari na michezo?

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo linalokua kwa kasi sana ambapo kila mwaka takribani vijana 700,000 huingia katika soko la ajira ilihali kati ya mwaka 2005 hadi 2008 nafasi za ajira zilizotengenzwa zilikuwa ni Milioni 1.1 tu.

Katika Bara za la Mawaziri lilopita masuala ya Vina yalikuwa chini ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana. Lakini katika Baraza jipya masuala ya vijana yamehamishiwa katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kana kwamba shughuli pekee ya kumuendeleza kijana wa Tanzania ni mambo ya michezo na utamaduni tu?

Nini maoni yako?
 
naomba kwanza kufahamishwa kijana ni mtu wa umri gani mwisho?
 
Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo linalokua kwa kasi sana ambapo kila mwaka takribani vijana 700,000 huingia katika soko la ajira ilihali kati ya mwaka 2005 hadi 2008 nafasi za ajira zilizotengenzwa zilikuwa ni Milioni 1.1 tu...............................Kwanza kabisa kitendo cha kucheza cheza na Muundo wa serikali kinaonyesha kuwa tuna serius critical problem.Hatuna Stable Governmen strucure japo kwa miaka 10. 40 yrs after independece inaonekana bado hata structure ni issue.

Pili kitendo cha kubadilisha badilisha kita consume time. Time ya kuhamisha resources( Finance, bajeti wafanyakazi, etc ) za vijana zilizokuwa chini ya wizara ya kazi na sasaa kuzihamisha Wizara nyingine. Hata kama ni wazo sahii kitendo cha kuhamisha hamisha kinapunguza efficiency ya serikali japo kwa miezi kadhaa. Tena mbaya zaidi imefanyika katikati ya mwaka wa bajeti. Kwa Nini asisubiri kufanya hivi kwenye bajeti ijayo?

Hii inaonyesha wanasiasa wengi hawataki kufikiri beyond politics na washauri wao hawawambii ukweli matatatizo ya kucheza cheza na structure

Kwa hili naona we need a stable government structure.

Gaijin said:
Kwa mtazamo wangu kitanzania au kiafrika nadhani kijanani ni yule ambaye yuko below 45
 
naomba kwanza kufahamishwa kijana ni mtu wa umri gani mwisho?

Umoja wa Mataifa (UN) unawatambua watu walioko katika rika la kati ya miaka 15-24 kuwa ni vijana, lakini Tanzania inatambua watu walioko katika rika la kati ya miaka 15-35 kuwa ni vijana.
 
Umoja wa Mataifa (UN) unawatambua watu walioko katika rika la kati ya miaka 15-24 kuwa ni vijana, lakini Tanzania inatambua watu walioko katika rika la kati ya miaka 15-35 kuwa ni vijana.

iwapo vijana ni hadi miaka 35 basi haiingii akili kuwa vijana wawekwe chini ya wizara ya michezo.

Vijana wanamaliza chuo kikuu wakiwa na miaka 23-25. Wanaajiriwa au kujiajiri na kuajiri wengine, wanakuwa na responsibilitie na kuliingizia taifa mapato. Hao ndio wenye nguvu ya kuleta mabadiliko nchini.

Sielewi rais anaposema vijana shughuli zao zinahusiana na michezo......
 
Naam ..! huo ni upeo wa Rais .....AKILI MUKICHWA! POLENI MLIOMCHAGUA .!mzee hajui masuala mengine ya vijana zaidi ya Bongo flava na mbio za mwenge au Green Guard na masuala ya urembo!
Kama alishasema hajui chanzo cha umaskini wa Tz unategemea nini!
HAWEZI KUANGANISHA DHANA NZIMA YA AJIRA KUWA KWA SEHEMU KUBWA UNAWAHUSU VIJANA,...KIUWA VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA ....HAJUI ,VIJANA WENYE AKILI ENDELEZENI MAPAMBANO ,NCHI HII YAHITAJI UKOMBOZI ...HAKUNA KULALA......!HATUWEZI KUONGOZWA KWA AINA HII HATUMTENDEI HAKI MUNGU ALIYETUUMBA NAAKATUPA AKLI!
 
Kwanza kabisa kitendo cha kucheza cheza na Muundo wa serikali kinaonyesha kuwa tuna serius critical problem.Hatuna Stable Governmen strucure japo kwa miaka 10. 40 yrs after independece inaonekana bado hata structure ni issue.

Pili kitendo cha kubadilisha badilisha kita consume time. Time ya kuhamisha resources( Finance, bajeti wafanyakazi, etc ) za vijana zilizokuwa chini ya wizara ya kazi na sasaa kuzihamisha Wizara nyingine. Hata kama ni wazo sahii kitendo cha kuhamisha hamisha kinapunguza efficiency ya serikali japo kwa miezi kadhaa. Tena mbaya zaidi imefanyika katikati ya mwaka wa bajeti. Kwa Nini asisubiri kufanya hivi kwenye bajeti ijayo?

Hii inaonyesha wanasiasa wengi hawataki kufikiri beyond politics na washauri wao hawawambii ukweli matatatizo ya kucheza cheza na structure

Kwa hili naona we need a stable government structure.

hapo umenena the only option ni kurarua katiba iliyopo na kuja na mpya mtu hawezi akawa anacheza na mambo nyeti kama vijana ambao ni zaidi ya nusu ya wakazi wa nchii hii jamani what a hell
 
Tuna tatizo ya kutojua tatizo na kulitafutia mzizi (root course) kabla ya kutoa solution. vijana kweli wanahitaji ajira lakini kuweka wizara moja yenye maneno Vijana na Ajira au michezo haujatatua shida.

Ajira million moja hazitengenezwi na wizara bali mkakati wa kweli wa kutengeneza ajira (viwanda, kilimo cha kisayansi etc)
Vilevile kuweka wizara yenye maneno kama maji, umwagiliaji, kilimo...mifugo nk kutabakia kuwa mkusanyiko wa maneno tu kama hatutaweka mikakati ya kweli.
 
Back
Top Bottom