Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Bakhti Lamine Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Vijana na Michezo ya nchini Algeria

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Bakhti Lamine Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Vijana na Michezo ya nchini Algeria, Septemba 7, 2023 Jijini Algiers.

Mazungumzo hayo yalikua na lengo la kuwa na ushirikiano baina ya Tanzania na Algeria katika sekta ya Michezo hususan katika mafunzo ya uongozi wa miundombinu ya michezo na uendelezaji wa vipaji.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu yupo nchini Algeria kuungana na Watanzania kuishangilia Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) katika mchezo wake dhidi ya Timu ya Taifa ya Algeria utakaochezwa leo majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania kuwania kufuzu fainali ya AFCON mwaka 2024 nchini Ivory Coast.View attachment 2742072
IMG-20230907-WA0046.jpg
 
Back
Top Bottom