Tumekwama barabarani usiku huu kwa matukio haya mawili

Aliemwambia asafiri usiku wa manane nani?
Unapoamua kusafiri usiku wa manane lazima uwe na tahadhari,halafu asilimia 80 ya wanaopenda kusafiri usiku ni wafanya biashara ya magendo na mihadharati kwa kua wakti huo polisi sio wengi
Dhibitisha au itakuwa uzushi usio na mashiko. Kwa mtu anayejali kupangilia muda wake wa uzalishaji, kusafiri usiku ndo muda bora zaidi wa kusafiri ili akifika anakoenda aanza kufanya shughuli zake mara moja. Napenda kuihimiza serikali iruhusu magari kusafiri usiku ili kuokoa nguvukazi inayopotea kwa watu kusafiri mchana, kutilia maanani udhibiti wa spidi ya mabasi uliopo sasa hivi. Piga hesabu idadi ya mabasi yanayosafiri safari kwa siku Tanzania nzima, zidisha na abiria kwa kila basi. Kuweka sheria ya kusafiri mchana tu ni kukubali kushindwa na majambazi wachache wanaoteka magari, na ni aibu kwa nchi.
 
Ila watanzania kwa kulalamika hatujambo. Mshaambiwa usafiri wa usiku ni hatari bado mnalazimisha kusafiri kisingizio mbona kenya wanasafiri usiku. Hizo mamlaka husika nao ni binadamu,kama bara bara haipitiki watapita wapi kuja kuwapa msaada?
Mkuu, nikumbushe ni lini hili tangazo la "kusafiri usiku ni hatari" lilitoka lini!?
 
Lawama kila kitu,
Umesafiri wewe tena usiku ufike porini uanze kulalamika kuwa hakuna msaada wa polisi?
Hali yenyewe ya mvua kubwa!!

Kuweni na mioyo ya kiutu polisi sio malaika wa kuota matukio, toa taarifa!!

Halafu kutwa kucha mnawatukana hao polisi kuwa sio watu na hawana msaada wowote eti kazi yao kutesa wapinzani, mkitekwa mnaanza kuwalilia wawasaidie,

Nanga wakubwa nyie mlitakiwa kuliwa viboga kwanza.
 
Habari za usiku

Wanajf wenye mamlaka husika ya barabara ya kuanzia korogwe hadi arusha usiku huu mvua ni kubwa barabara sehem nyingi hazipitiki mimi nimekwama hapa karibia na hedaru tumeambiwa mbele barabara imeziba shauri ya maji kupita juu lakini mbaya zaidi tunaambiwa hapo mbele yetu maeneo ya mgagao gari nyingi zimetekwa huku mvua kubwa inaendelea kupiga eneo hili hadi sasa saa 9 kamili usiku huu hapa porini. la kusikitisha kuliko yote hadi sasa a hatujaona mamlaka yoyote inayohusika na dharula hizi ikipita kutoa msaada wa aina yeyote raia tumebaki kama vifaranga japokuwa ziko gari zaidi ya 160. tumeamua kujilinda na bastola zetu tunazozimiliki kihalali kama mkombozi pekee aliyebakia View attachment 734778
Kujilinda ni jukumu la kila raia
 
Ukisoma uzi huo hasa hiyo barua ya huyo mkuu wa police anazungumzia zaidi mabasi na sio private cars and again issue ya hilo katazo sio suala la security, ni suala la uvunjaji wa sharia wa madereva hasa speed kwenye maeneo yanayo katazwa; mleta uzi kazungumzia usafiri wake but again, huonagi malori hiyo mida ya usiku ndio mida yao!? Makampuni baadhi yameweka utaratibu wao wa kusafiri mida ya mchana tu, wao wameenda mbali zaidi kwamba mida ya jua kuzama tu, then park lori lao hapo hapo (eneo ambalo walau ni makazi ya watu ) na dereva alale hapo, again issue sio security, issue ni safety but again kwao sio kwasababu ya katazo la kisheria buli ni utaratibu wao kama owners
 
Mleta mada kasema walipata msaada wa askari wenye silaha baadae na wakapita salama......hiyo hakuna alieona wala kuchangia.ni kama kuna watu wanatafuta mabaya tu ndio wayaseme
 
Back
Top Bottom