Tumekutana Instagram, amenitumia nauli niende kisiwa cha Malta tuonane

Sasa Mr huyu kijana kapata bint wa 17yrs na yuko chuo. Na ukingalia kwa undani huyu bint n mdogo, yupo chini ya wazaz. Sasa huu uwezo anautoa wapi?

Angekua mwanamke ndo anatakiwa na mwanaume huko ni sawa tyuuh.
Nilimuuliza kitu hicho akasema huwa anampiga fix wazazi wake kila mara wanamtumia pocket money anakusanya
 
Nakushauri tafuta Mtanzania aliyepo malta wasiliana nae huyo mtanzania ndio akutumie Mwaliko wa kwenda huko bila yule binti kujua ukishafika mtafute huyo binti kutana nae sehemu ya wazi au Restaurant sehemu utakayofikia msome mtu kama ana nia mbaya utajua tu siku ya pili hama Hotel kwa sababu tayali utakuwa umestudy Mazingira hakikisha sehemu zote unazoenda huyo Mtanzania anajua kama una app ya kutrace location kwenye simu yako weka off kabisa na kama utapata chakula au kinywaji na huyo binti usimpe chance ya kubaki peke yake na kinywaji au chakula usikurupuke kupiga Papuchi ikiwezekana kwa kuwa lengo ni kuonana rudi TZ bila kupiga papuchi kama ana nia kweli mtaendelea kuwasiliana kama alitaka kukufanyia mchezo atakata mawasiliano Tiketi kata kabisa Go and Return
 
Mkuu Hongera Sana Huo ni Ujasiri Wa Kiume. Una Roho Kama Yangu, Nimeenda Nchi Nyingi sana Bila Hata kujua Naenda Kufanya Nini, Ila Huwa najisemea Ngoja Niende Nione itakuwaje. Na Hizi Trip Hazihitaji Pesa Nyingi Sana.

Twende Kwenye Issue Yako

1. Kupata Visa Ya Malta.

Ukitaka kupata Visa Ya Malta Kwa Tanzania kwanza Unatakiwa uwe Dar Es Salaam, Ukiwa Pale Dar Es Salaam unaenda Ubalozi Wa ITALY pale Utaomba Visa Yako. Sina Hakika na Charges Lakini Haizidi Tsh 100,000/= ya kupata Visa. Na kwasababu Yako Chagua Kwenda Kwaajiri ya Tourism baasi Inatosha. Mahitaji ya kupata Visa Ni Yale Yale Ya Siku zote, Bank Statement, Medical Aid Cover, passport Yako, Kama Una Mwenyeji kule ambaye ndio Huyo Demu wako( Akuandikie Barua Ya Kuku Invite, Atakupa Home address yake na Vingine) usiseme ni Demu wako Kwasababu Hakuna Nchi Inayo Ruhusu kudate na Mtu ambaye ni Under 18 So hiyo ni Illegal, Kikubwa Wewe Unaenda Kwa Utalii Inatosha. Kuhusu Medical Aid Sahizi Mashirika Ya Ndege Yanakupatia Medical Aid au Hata Ubalozini Wanaweza Kukupatia Kutegemea Unakaa Muda Gani Kule. Medical Aid Haiwezi Kuzidi Tsh 500,000/= kama Unakaa Chini Ya Miezi 3. Bank Statement hiyo Dollar 2720 ni Nyingi sana Inatosha, Kwanza Wa Italy wanajua Kuwa Tanzania Tunaweka sana Hela Kwenye Tigo Pesa, Mpesa na Zingine kuliko Bank So Relax kuhusu Bank Statement hata kama haina Mpunga Wa Kutosha

2. Unakuwa Na Yellow Fever Certificate, hii Just In Case wakihitaji, Hii unaipata ndani ya Siku Moja Kwa Gharama Ya Tz Sh 30,000/=, Bila Shaka Passport Ya Kieletronic Unayo. Kama Huna Ukiwa Dar Es Salaama Gharama ni Tsh 170,000/= kupata Passport Na Unaipata Ndania Ya Wiki 6 ( Huu Ni muda wa Kiserikali) Ila Muda Wa WAHUNI ni Siku 1 hadi Siku 2 umepata Passport yako Safii, Ila Kama Unapenda Kulipa Kodi basi Kuna Express/VIP gharama yake ni Millioni 1 ya kitanzania Unapata Less than Week 1, Najua National ID unayo au ile ID number tuu inatosha.

3. Ticket ya Ndege, Kwa Shirika Bora Kabisa La Ndege Lenye hadhi Ya Kimataifa Yaani Emirates RETURN Tickets Ni Tsh, 2,220,000/= hii inaweza kupungua kulingana na Muda Utakao Kata Ticket, Unaanzia Dar Es Salaam, Una Stop Zanzibar Dakika Kadhaa, Then Unatua Dubai, Pale Dubai Mtazuga Masaa 2 Then Kimoja Kwenda MALTA. Ni Kama Safari Ya Masaa 23-26 kutegemea na Connection Ya Flights, Ila Dar To Dubai Ni 5 hrs and 25 minutes, Then Dubai To Malta ni 8hrs and 40minutes so utajumlisha na Muda wa StopOver Mara nyingi Dubaid Connecting ya Kwenda Malta huwa ni 9 hrs. Ukiamua kwenda Na KLM ni USD 1,230 hii Ni Return Ticket Inaweza Kushuka Kutegemea na Muda.

4. Hotel Za Malta.

Hotel Kali Kabisaaa Sio Ya Kihuni Huni, Ambayo unaweza hata kupost Status Kwa 7 nights Huwa ni Tsh 2M, 1.5M au 1M una Enjoy Maisha, Unaweza Kulipa Kabla Hujaondoka Kabisa. Chukua Hotel Kupitia BOOKING.COM hawana Mizingua Hizo hotel unapata Breakfast Ya Nguvu. Lakini Mimi Hupenda Kutumia AirBnB.com hii Unachukua Apartment kwa Bei rahisi kabisa, Unaweza kujipikia na kuwa Huru zaidi Kuliko Hotel na Ni Cheap, Unaweza Kulipa Kabla Ya Kuondoka Dar kutegemea utakaa muda Gani.

5. COVID-19 RULES.

Unapima Covid Yako unapata majibu yawe ndani Ya 72 hrs hadi Unafika Malta, kupima Covid ni kama Tsh 115,000/= na Ukiwa Unarudi Utapima Tena Malta ni Kama Dollar 100 ukiwa Malta, Na Ile Ya wizi wizi ya Bongo ukiwa Airport ni Tsh 23,000/=. Unawahi Kabla Tanzania Hawajatangaza OMICRON Wakitangaza Tuu Malta Itazuia Wasafiri Toka Tanzania. Lakini So Far Tanzania Kwa Malta tupo kwenye Dark Red Countries Kwa Issue Ya COVID-19, Unajiweka Quarantine Siku Kadhaa Tuu au Unaweza Usijiwekee.

6. OTHERS.

-Unakuwa Na Visa Au Mastercard ATM card, Unaweza Kutoka Mpunga Popote, Unakuwa na Internet banking Just Incase, Unaruhusu Card yako kufanya Online Purchases na Vingine Unakuwa uko Full Mkoko.
  • Sheria Ni Moja Usitembee Na Cash Wala Usifanye Malipo Kwa Cash, popote pale Omba Kulipa Kwa Card.
  • Hotel Unaweza Kuomba Wakufuate Airport ila huwa ni Gharama, Download Application Yako Ya BOLT weka Kulipia Kwa Card weka Card yako Ukifika Airport Request Bolt kwenda Hotelini. Au Malta Wan application yao ni kama Uber inaitwa eCABS una request Gari, Uber Kule Haijafika. Bolt usalama Wake ni mdogo ila angalia Driver Status yake Ka Complete Safari ngapi na Nini kama Ratings zake.

- Internet- Hotelini Utapata Free Wifi, Aiport Utapata Free Wifi, Mwenyeji Wako Atakupa Free Wifi, ukawa unaingia Jamii Forum Na Kutusimlia Yanayo Jiri , Lakini Unaweza Kupata SimCard. Afu kile ni kisiwa cha Kitalii, Ni Wazungu So Wazungu Hawana Ubabaishaji Kama Afrika. Uta Enjoy Maisha.

Mwisho, Hiyo Dollar 2720 ni NAULI tuu Na Vitu Vidogo vidogo sana, So kama ukifika Kule Akupete mpunga zaidi Au adeposit tena kwenye Account Yako, Au Wewe Uwe na Mpunga Na Wewe hata Millioni 2 tuuu Za Emergency Sio Unamtgemea Demu Wako Tuuuu Mwanafunzi, Malta ni Kisiwa cha Kitalii Hizo Dollar 2720 Ukiwa Malta Si Chochote Si Lolote, Angalia Hesabu hizo Hapo Juu Utaona Inaisha Kabla Hujaondoka Bongo , Bado kwenye Hizo Aiports Utakula na Nini. Na Wewe Jiongeze. Basi Ukiwa na Akili Malta Utatoboa, Nenda Umeweka Rasta utapata sana Hela, Mpe Demu wako Show Ya Nguvu Rough Moja Mbaya sanaa, Uta Enjoy maisha Siku Za Mbeleni. Ulaya Ni Ulaya Tuuu na Afrika ni Afrika Tuuu…

Kuwa Kuna Ukristo sana, Wanatumia Euro kama Pesa Yao ila hata Dollar Unatumia, Ni Kaeneo Kadogo sana Yaani Dar Kubwa Sana, Kitu ambacho Muhuni Hakiwezi kukushinda . Wazungu wako Straight Sanaa Uje uje kweli, Akisema Usije Amemaanisha

Nilifika MALTA nikiwa Simjui Yeyote nili Enjoy Nikatengeneza Na Marafiki Kibao, Baada Ya Hizi Sikukuu, Nitarudi Tena MALTA kwa Mwaliko wa Marafiki zangu Kuna Sehemu Nataka Kwenda Kutalii Sijawahi Fika, Pande Za Italy, So Kutokea Malta Kwenda Italy ni Rahisi Sana, Tunachukua Kivuko Tuu pale Chap Tupo Italy… So Tumepanga na Wahuni wangu wa kule kwenda Kutembelea eneo Fulani Italy ni Rahisi Ukitokea Malta. Blazaaa USIOGOPEEEE
 
Hii habari nilijua ni mwanamke kaandika kumbe mwanaume hakika kizazi chetu kinaangamia tufiche wapi watoto wetu wa kiume jamani yaani uko serious kabisa unataka kumfuata,nenda ndugu Ila wape taarifa ndugu zako litakalokukuta uwe tayari
 
Kufa kupo tuu …chukuwa risk iyo ila jiridhishe mambo kadhaa wa kadhaa muhimu
Picha zake unazo waachie baadhi ya ndugu na details za mwanamama zote kwa ajili ya taathari
Wazungu wanakuja daily Arusha kuona pisi zao walizikutana nazo online…
 
Mnanitisha jamani
Haya ndo matokeo ya kuweka hadharani privacy zako za mahaba.

Kuna vitu unapaswa kufahamu na kufuatilia.

Chukua tiketi nenda lakini hakikisha unajikonnect na mtandao salama huko.

Kuhusu bei ya nauli, ingia google angalia gharama au nenda traveler agency au tembelea ATCL website wana kila kitu mule hadi gharama ya kusafirisha nyoya za kuku
 
Najua watanzania hampendi kupangiwa maisha
Ila mimi naona bro malta usiende

Tafuta vitz yako safi uwe unagandishwa na AC hapa dar safi kabisa hapo ushatafuna line na umezika simu

Namnukuu proffesor wa language hapo juu

But still is you're judgement and decision ....but take care ohooo

Mrejesho utupe kama utaagana na nyonga ukienda ukarudi utuletee

Aloo ila nilijuaga malta ni ile tamutamu kumbe kuna nchi zinaota kama uyoga
Uletepo ukirudi.....kama utarudi
 
Back
Top Bottom