Tumekutana Instagram, amenitumia nauli niende kisiwa cha Malta tuonane

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Wadau kuna binti tumefahamiana kupitia mtandao wa kijamii Instagram ,ana miaka 17 yupo kisiwa cha Malta, tulianzisha mahusiano kupitia huo mtandao na hatimaye tukabadilishana namba za sim tukawa tunachat WhatsApp na kupigiana video call

Ni mwanafunzi wa chuo na wazazi wake ni wafanyabiashara
Binti alishanitambulisha kwa Dada yake ambaye yupo UK ni mwandishi wa habari na shangazi yake ambaye wapo naye chuoni na wananitaka niende

Hivi vihela vidogo vidogo binti na shangazi yake huwa wananitumia na nikiwauliza hela wanatoa wapi na wapo chuo wanasema wazazi wao wanawapa pocket money

Na wananipenda hatari

Tumefahamiana kama miezi 5 imepita juzi kanitumia dola 2720 niende kumtembelea nchini kwake kisiwa cha Malta.

Naomba nisaidiwe yafuatayo

Nauli kwenda Malta ni dola ngapi?

Vipi kuna usalama hapo? Na vipi maisha ya Malta yakoje anayejua

Vipi sheria za Malta kudate na miaka 17
Au nimzime hii hela na niblock

Updates

Nashukuru kwa michango yenu,wengi mmeshauri nisiende ila wengine wanasema niende

Kwa ujumla naheshimu mawazo yenu ila naomba niungane na wale wa kukubali niende ,nimeanza kuandaa harakati za kwenda huko

Nimewasiliana na mamlaka ya vissa Malta wamenipa utaratibu lakini kwa kipindi hiki cha mlipuko wameshauri kwamba nisubiri kidogo kwa sasa wameweka masharti magumu kidogo ya kuingia nchini kwao

Vissa yao wanashughulikia ndani ya mwezi mmoja ,muda huo nifanye maombi ya vissa nikisubiria hali ya covid inaendaje huko ila wakanitahadharisha nisije nikafanye booking ya ndege mpaka wao waje kuniambia

Pia nitakuwa na tahadhari nikifika Malta na kuna mdau mmoja alinishauri nifikie kwenye kanisa ili niangalie hali ipoje ndo niendelee na mambo mengine ila Watanzania mniombee.

Soma Mrejesho:
 
Naomba uage kabisa ndugu jamaa na marafiki; mali zako wagawie kabisa wasije wakazigombania. Usisahau kutuonesha eneo la kaburi, unataka liwe wapi (in case mwili ukifanikiwa kurudishwa). Hizi ni dalili fika za kunyonywa damu mchana kweupe mwishoni mwa mwaka. Weka mbali na watoto!!!

Mabinti wa Bongo milioni 27 huwaoni!??? Kweli mapenzi kipofu!!!
 
Ukizima iyo pesa akifuatilia ubalozi unakamatwa ana picha zako nyingi kuwa na roho ya uaminifu kama uko sirious rudisha tafuta sababu yoyote na inawezekana mara nyingine ukatumiwa zaid ya hizo. Take care

Upande wapili angalia umeonesha ushaanza kufahamu kitu kama mwanafunzi anapata wapi pesa binadamu wana siri kubwa mpaka yakukute ndio utajua.
 
Biashara ya kuuza viungo vya binadamu haipo huko Malta?
🏃🏃🏃
IMG_20211219_093514.jpg
 
Aisee hii mbona inanishtua
.
Usiogope bana, kama mmeongea mtandaoni kwa muda wa kutosha wewe pekee ndio unaweza kujua kama umwamini huyo binti au la...hata Tanzania mbona kuna watu wamepotea kwenye mazingira ya kutatanisha na wengine walikuwa wanaibuka kwenye viroba, kwani unaogopa kukaa Tanzania ?....japo sipendelei sana kuanzisha mahusiano ya kirafiki/kimapenzi kwenye mitandao lakini najaribu kuwa open minded, wewe pekee ndio unaweza kujua kama kuna viashiria vyovyote vinavyoonyesha kwamba unajipeleka kwenye mdomo wa mamba.
 
Why usimshawish aje Tz? Unaenda nae Serengeti, ngorongoro nk. Kma unakwenda malta hakikisha unafikia ubalozini
Nimewahi kumdokezea hili kwamba aje huku akasema baba yake hatakubali coz yupo chuo na vibali hana akashauri labda tukutane UK ,sasa nikajiuliza mtu wa vijijini huku nifikeje UK ,hata mia sina,nikapotezea hiyo ya UK
 
Wadau kuna binti tumefahamiana kupitia mtandao wa kijamii Instagram ,ana miaka 17 yupo kisiwa cha Malta, tulianzisha mahusiano kupitia huo mtandao na hatimaye tukabadilishana namba za sim tukawa tunachat WhatsApp na kupigiana video call

Ni mwanafunzi wa chuo na wazazi wake ni wafanyabiashara
Binti alishanitambulisha kwa Dada yake ambaye yupo UK ni mwandishi wa habari na shangazi yake ambaye wapo naye chuoni na wananitaka niende

Hivi vihela vidogo vidogo binti na shangazi yake huwa wananitumia na nikiwauliza hela wanatoa wapi na wapo chuo wanasema wazazi wao wanawapa pocket money

Na wananipenda hatari

Tumefahamiana kama miezi 5 imepita juzi kanitumia dola 2720 niende kumtembelea nchini kwake kisiwa cha Malta.

Naomba nisaidiwe yafuatayo

Nauli kwenda Malta ni dola ngapi?

Vipi kuna usalama hapo? Na vipi maisha ya Malta yakoje anayejua

Vipi sheria za Malta kudate na miaka 17
Au nimzime hii hela na niblock
Mwambie aje bongo
 
Back
Top Bottom