Tumejifunza nini kwa haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumejifunza nini kwa haya?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Nov 8, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wakati tukio la polisi kuvamia mkutano wa CDM pale viwanja vya NMC unga Limited likitokea, inadaiwa kuwa Mhe. Mwenyekiti wa CDM Bw. Freeman Mbowe alikuwepo lakini cha ajabu alifanikiwa kuchoropoka (haieleweki) ni kwa staili gani hiyo ambayo iliwaacha baadhi ya wana CDM wenzake akiwemo, Dr. W. Slaa na baadhi ya viongozi na wakereketwa wa CDM (wanyonge) kukamatwa na hatimaye kupandishwa kizimbani. Hata hivyo, kesi ilipokuja mahakamani, viongozi wote wa CDM na washtakiwa 20 wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana , lakini wengine 7 wamepelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Haya yanatokea japokuwa wanachama wenzao wa CDM walikuwepo mahakamani na ni kama wameshindwa kuwadhamini hao 7 walioenda rumande...

  Maswali ya kujiuliza ni je, tupo pamoja au ndio ile ya kila mtu atakufa na mzigo wake??


  Dr. Slaa na Lissu kizimbani Arusha - YouTube

  CHADEMA Wapiga Kambi NMC Arusha - YouTube
   
Loading...