SoC03 Tumejifunza nini katika majanga yaliyotupata?

Stories of Change - 2023 Competition

Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
313
271
Nchi yetu inakumbwa na majanga mbalimbali kila mwaka. Majanga haya yanaweza kuwa ya asili au yasiyo ya asili (artificial). Ukipitia vyombo mbalimbali vya habari kama televisheni, redio au magazeti si ajabu ukakutana na vichwa vya habari vinavyosomeka hivi:

“.. watano wamefariki kutokana na ajali ya moto….’’, “ nyumba imeungua na kuteketeza familia yote’’, “ ajali yaua 20 na kujeruhi 40’’, ajali ya meli, ajali ya ndege na kadharika.

Madhara yatokanayo na majanga haya ni pamoja na kupoteza uhai wa watu, kupoteza uwezo wa kufanya kazi tena kwa majeruhi, uharibifu na upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu mbalimbali ambayo imeghalimu serikali fedha nyingi kuitengeneza.

Takwimu zinaonesha kuwa kuna vifo na majeruhi 1,010 vilivyotokana na ajali mgodini, mashimo ya vyoo, ajali barabarani, mafuriko, mito mabwawa na baharini haya hapa nchini kwa mwaka jana kuanzia january hadi disemba

Majanga haya husababishwa na sababu mbalimbalimbali kama vile nguvu za asili kama maporomoko ya udongo, mawe, matetemeko ya ardhi, kimbunga na dhoruba kali baharini na ziwani. Vilevile, majanga yanaweza kusababishwa na uzembe katika kuendesha/kuongoza mitambo, matumizi mabaya ya gesi/petroli, mafunzo dhaifu kwa madereva, rushwa kwa wasimamizi wa kanuni na sheria, na jamii kutokua na elimu ya kujikinga na majanga.

Hata hivyo, jamii ya watanzania imekua na kasumba ya kutochukua hatua Madhubuti mara baada ya haya majanga kutokea. Jamii na serikali kwa ujumla imekua ikisahau na kutoweka namna bora ya kuzuia majanga haya yasitokee tena au kupunguza athari kwa jamii endapo majanga haya yatatokea tena. Leo ningependa tuangalie majanga ya moto.

Taarifa ya utekelezani ya jeshi la zimamoto kwa vyombo vya Habari ya mwezi wa kwanza, 2023 imeelezea kuwepo kwa matukio ya moto 1854 nchini katika kipindi cha kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa kumi na mbili 2022. Katika ajali hizo kuna Jumla ya vifo vya watu 32 na majeruhi 66 (Jeshi la Zimamoto na Uokoaji – Kuokoa Maisha na Mali). Matukio hayo ya moto yametokea katika maeneo ya umma kama vile shule (Bwiru, Buhangija), viwanda (GSM, BORA, JAMBO), masoko( Sido, Karume, Kariakoo) na kusababisha hasara kubwa kwa mali kama ilivyoelezwa na mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi bwana Lukaza; “Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa kuungua moto kwa Soko la Karume, Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na kuungua kwa soko hilo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 7.2 ambapo idadi ya Wafanyabiashara waliokumbwa na janga hilo ni 3,090” ( Unaambiwa Hasara iliyotokana na Kuungua Solo la Karume ni Zaidi ya Shilingi Bilion 7)

Chanzo cha matukio hayo ya moto imebainishwa kuwa ni hitilafu za umeme, matumizi ya mishumaa na vyanzo vingine visivyojulikana kama inavyoelezwa baada ya matukio haya. Hata hivyo, tumeshuhudia jeshi la zima moto kuchelewa kufika katika eneo la tukio kwa kile inachosemekana ubovu wa miundombinu, upungufu na uchakavu wa vifaa vya kazi, Magali kufika bila maji/povu ya kuzimia moto na wakati mwingine upungufu wa weledi unaopelekea mali kuteketea hadi kuisha huku jeshi la zimamoto wakiwa eneo la tukio.

Je nini kifanyike ili kupunguza majanga ya moto na madhara yake?

Pamoja na matukio haya ya moto yaliyoteketeza Maisha ya raia na mali zao, bado juhudi za kudhibiti majanga haya hazitoshi na kufanya ajali za moto kuendelea kutokea hapa nchini.
  1. Elimu kwa umma : Jitihada mbalimbali zimekua zikifanywa katika kukabiliana na majanga ya moto hapa nchini ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na majanga haya kama ilivyoelezwa na Jeshi la zimamoto (mafunzo kwa maeneo 7511 na kufikia watu 421,656 kwa mwaka 2022). Takwimu hizi zinamaanisha kwamba asilimia 0.68 ya watanzania zaidi ya milioni 61 (61,741,120; National Bureau of Statistics - Home) pekee ndoyo ilifikiwa na mafunzo na elimu hii kwa mwaka jana, pia itachukua miaka 146 kufikia wanzania wote. Hii inaonesha kwamba kasi ya kusambaza elimu kwa jamii juu ya majanga ya moto ni ndogo kuliko inavyotakiwa. Nashauri jeshi liongeze kasi kwa kutumia mitandao ya kijamii na watu wenye ushawishi ili waweze kufikia watu wengi Zaidi.
  2. Jeshi Madhubuti la zimamoto: Jeshi la zimamoto linakabiliwa na upungufu mkubwa wa watendaji, hili linadhihirishwa na kauli ya kamishna jenerali aliposema Idadi yao haitoshi kuhudumia nchi hii kubwa. “Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye amesema wanakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi ikilinganishwa na ukubwa wa nchi na idadi ya wananchi”( Zimamoto kuajiri wafanyakazi 1,500). Hivyo, ni vyema serikali ikachukua hatua za Madhubuti katika kuajili wafanyakazi wa kutosha na wenye weledi mkubwa katika jeshi hili na vifaa vya kutosha . Sambamba na hilo, serikali iendelee kuwapa mafunzo ya kutosha wakiwa kazini hasa yanayoendana na madiliko ya technolojia kama matumizi ya ndege nyuki katika kuzima moto kwenye majengo marefu yanayozidi kushamiri hapa nchini.
  3. Uwekaji wa vidhibiti moto kwenye majengo ya umma na binafsi: Sheria namba 14 ya mwaka 2007na kanuni zake za mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 yanatoa jukumu la ukaguzi wa vifaa vya kinga na tahadhari kwenye maeneneo ya huduma za umma na vyombo vya Usafiri. Lakini, ni dhahiri kuwa bado kuna shule, masoko na sehemu nyingine za umma hazina vifaa hivi muhimu kukinga janga la moto. Uzembe huu utakomeshwa kwa kufanya ukaguzi stahiki na kuchukua hatua kwa wote watakao kiuka agizo hili.
  4. Mpango bora wa ardhi na kuweka miundombinu bora ya barabara: Mpango bora wa ardhi utaweka barabara zinazowezesha magari ya dharura kama zimamoto na magari ya wagonjwa kufika kwa wakati.Waziri Kangi Lugola (2018) alisema ““Tunatakiwa kuachana na ujenzi holela kwa sababu unasababisha vikosi vya zimamoto kushindwa kufika eneo la tukio kwa wakati,” amesema.“Jambo hilo linawafanya waonekane hawafiki maeneo husika kumbe chanzo ni sisi wenyewe. Lazima tubadilike na viongozi wasimamie hili.”

Hivyo Hatuna budi kuhakikisha kuwa makazi, shule, hospitali na viwanda vinafikika kwa urahisi ili kuokoa mali na uhai endapo majanga ya moto yatatokea.

Mwisho.
 
Back
Top Bottom