Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Serikali imesema imepanga kufanya maboresho makubwa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni juhudi za kupambana na athari za majanga pindi zitokeapo ajali mbalimbali ikiwemo ajali ya moto ili kuweza kuokoa mali na maisha ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania itanunuliwa Helikopta ya kusaidia uokoaji.
Maboresho hayo yanajumuisha ununuzi wa magari ya kuzimia moto yasiyopungua 150, magari 20 ya kubebea Wagonjwa, boti za kisasa 25 za uokozi na Helikopta moja maalum ya uokozi.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema hayo Kibaha Mkoani Pwani wakati akiongea katika mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara na Makatibu Tawala ulioandaliwa na TAMISEMI.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi hii, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakwenda kufanya uwekezaji mkubwa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, nawaomba Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kunakuwepo vituo vya kuchotea maji ambayo yatatumika pindi yatokeapo majanga ya moto”