Tumejiandaa kupokea matokeo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumejiandaa kupokea matokeo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Good, Sep 23, 2010.

 1. The Good

  The Good Senior Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Pilikapilika za uchaguzi zipo kwenye kilele. CCM na CHADEMA wanakabana koo huku CUF wakichukua kasi. Kila mmoja ana matumaini ya ushindi kwa chama chake.. Lakini tusisahau ni mmoja tu atashinda (hasa tukizungumzia nafasi ya urais).

  Sasa swali, Je kweli watu wamejiandaa kupokea matokeo? Kama tayari Mola ashukuriwe lakini kama bado na hasa ya kushindwa naona tatizo mbele.

  Matayarisho ya kisaikolojia ni muhimu na wana JF tunapaswa kuongoza hili. Tujiulize,
  Je tupo tayari kupokea matokeo ya kushindwa kwa Wagombea/Mgombea wetu?
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180  Wanaharakati tupo tayari kwa sababu kuu hizi hapa;
  1. Tuna uhakika wa kupata wabunge wengi wa kuingia bungeni, hiyo inatutosha kutupa moyo(motivation) hata tusipovuka nusu itaturiwaza kwani hatujawahi kufikia hapo for the past 15 yrs
  2. Tuna uhakika Dr.Slaa ataendelea kuwepo bungeni hata kama hatachaguliwa kwani kuna wagombea mambumbu wa sheria wa SISIEMU watakaochemsha kufuta taratibu hivyo chaguzi ndogo zitakuwepo ha hivyo Dr.Slaa kurudi bungeni, sababu hii itatupa moyo(motivation)
  3. Tuna uhakika kwa matokeo namba 1 na 2 hapo juu SISIEM wataongoza kwa shida sana kwani mbinu za kitaalam hawana hivyo bado upinzani utaiendesha serikali kama anavyofanya Dr.slaa kwa serikali kufanyia kazi maelekezo yake
  4. Nje ya namba 1,2 na 3 tunajiandaa kusherekea na kuwaacha SISIEM kwa huzuni kama jANNIFER wa BBA stars.
  Mtajijuuu
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Mkuu, the Good!

  Una akili sana broda!

  Hakika sijasikia mtu hapa ndani akiongelea jambo la busara hivi katika siku za karibuni!

  Kwa kuangalia tu, utaona kwamba wengi sana tuko OPTIMISTIC juu ya matokeo, and we just sound as if we hope only for the fovourable results!
  Lakini shilingi ina pande mbili wakuu!...Kushindwa ni likely result, hope you know probabilities!

  Mimi binafsi napenda kuchukua nafasi hii kuwaasa wenzangu kwamba jukumu letu si kulalamikia tu tutakapoona mtu tusiyetegemea ameshinda, lakini tunawajibika kusimamia kura zetu mara baada ya kupiga kura ili kuondoa grounds za malalamiko yasiyokuwa na ulazima!..

  Kama mtu atajiridhisha kuwa hakuna faulo iliyofanyika basi ana kila sababu ya kupokea matokeo kwa jinsi yatakavyokuja!

  Nawasilisha!
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani wanachadema tusije kimbiana humu jf, baada ya uchaguzi. kwani nakumbuka moja ya chaguzi ndogo zilipokwisha gazeti la tz daima lilipotea online. tuvumilie kwa machungu yatakayowapata lakini hiyo ndo politics, kuwa kuna kushindwa pia. nasema hiyo kwa sababu mnajipa matumaini kupita hata uhalisia wa hali ilivyo.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa kwa taarifa yako,
  Unapokuwa vitani lazima ujipe moyo utashinda tu hiyo ndiyo siraha ya kupambana vitani Hukupita JKT nini????ukapata mafunzo ya uchakaa????
  Hata msemaji wa SADAMU Hussein(waziri wa habari wa Iraq wakati ule) aliendelea kutoa taarifa za kujulisha dunia uimara wa jeshii tiifu la sadam. Iweje wana jf wasifanye hivyo??? ndizo mbinu za kumtia hofu adui, halafu unpiga Kichwa kiulaini.Kwa sasa CCM wamepagawa no confidence at all, can you imagine???!!!! Ni kubonda bila jasho
   
 6. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  sasa nadhani tunaweza kuongea lugha moja kwani kukubali matokeo ndio kukuwa kisiasa na kama hukuridhika na matokeo basi hatua za kisheria zifuatwe tuna mahakama huru nchini mwetu na tunao wanasheria kibao waliobobea na ifike mahali watanzania tuweke maslahi ya nchi yetu mbele kwanza halafu vyama vya kisiasa nyuma!!! Tusiruhusu mtu yoyote atuletee fujo na vurugu kwasababu kiongozi fulani wa chama fulani kaukosa urais!

  utulivu wa kisiasa tulionao nchini mwetu ndio tunu kubwa kuliko tunu zingine zote zinazopigiwa kelele na wana siasa wetu!!! Hivyo bila kujali wewe ni shabiki wa chama gani hatuna budi kulinda utulivu tulionao kwa nguvu zetu zote!!! Kiongozi anaekuambia mwaga damu yako ili yeye aingie ikulu, mwambie amwage yake kwanza, kwani yeye sio bora kuliko yesu!!!! Maana yesu alikubali kumwaga damu yake ili wengine waokoke!!! Kwa mujibu wa imani ya kikristo!

  wenzetu wa zenji wamelitambua hilo la maslahi ya nchi kwanza halafu vyama vya kisiasa baadae!!! Ndio maana kampeni zao zinaendelea bila fujo wala husikii kuna janjaweed au sijui nini utafikiri hawako ktk uchaguzi!!!
   
 7. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nadhani heading ya thread ingekuwa "Tumejiandaa kupokea matokeo YASIYOCHAKACHULIWA?" opposite to this I reserve my comments
   
 8. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimejiandaa kupokea matokeo yoyote ambayo hayana harufu ya aina yoyote ile ya wizi wa kura, lakini chama filisi cha mafisadi kimeshatuma waraka kwa watendaji wake mbali mbali wakiwemo wakuu wa wila, wa mikoa na wengineo kwamba "wafanye kila wawezalo" ili kuhakikisha ushindi kwa CCM. Sasa kwangu mimi "Kila wawezalo" ina maana hata mbinu haramu za kutoa rushwa na kuiba kura na huko nyuma haya yote yameshatokea. CHADEMA isiyakubali matokeo yoyote ambayo yataonyesha uchaguzi na uhesabuji wa kura utagubikwa na utata wa aina moja au nyingine katika eneo kubwa la nchi yetu.
   
 9. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  CCM wao wako tayari kuyapokea matokeo kwa sababu wana kila sababu ya kuyapokea

  hofu wapinzani wasije kusema kura zao zimeibiwa uchaguzi haujawa huru na wa haki
   
 10. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Je kutakuwa na asasi mbalimbali za kimataifa kama AU,UN, EU kusimamia uchaguzi?????
   
Loading...