JosephNyaga
JF-Expert Member
- Apr 28, 2014
- 291
- 232
Kwa wakazi wa mkoa wa Daresalama, Ni sehemu gani tulivu naweza kumpeleka huyu mtoto mzuri ambaye nina ndoto za kuja kumuoa awe mama watoto wangu nyumbani. Kesho tumepanga kuonana nae RASMI kwa ajili ya mazungumzo ya awali kabisa ya urafiki wetu, sasa najifikiria nimpeleke sehemu gani ambayo ni nzuri kwa mazingira na utulivu mkubwa ambapo tutaweza kuwa huru kuzungumza mambo yetu safi kabisa na kupata chakula na vinywaji kwa bei ya kawaida tu. Ninakumbushia tu kwamba iwe sehemu nzuri ya kuvutia na gharama za mkutano wetu ziwe za kawaida.
Nawasilisha wadau..
Nawasilisha wadau..