Tumefikaje hapa tulipo?

Hata mimi sina tatizo na watu kama nyie mnaopenda kuzungumzia WATU. Mimi nimekuwa issue yako wewe, while mimi nazungumzia Events na Idea. Hatufanani. Niseme utakavyo hainibadilishi wala haiweki mkate mezani kwangu, Uwe na siku njema..
 
Hakijabadilika kitu, mkuu 'Mkandara'!
Tuyaachie hapa yabaki yalivyo kati yetu.
Lakini nililo hakika nalo, mabadiliko makubwa hayazuiliki tena Tanzania.
 
Hata mimi sina tatizo na watu kama nyie mnaopenda kuzungumzia WATU. Mimi nimekuwa issue yako wewe, while mimi nazungumzia Events na Idea. Hatufanani. Niseme utakavyo hainibadilishi wala haiweki mkate mezani kwangu, Uwe na siku njema..
Hakuna kilichoharibika, maadam tumeelezana na kuelewana.
 
Mtanganyika Magufuli ndio alianzisha huu ushenzi wa kuiba chaguzi nchi nzima, kuteka na kuua wapinzani,huyu mnywa damu wa sasa kaanza kuwageukia wenzake, Nyerere aliongelea haya mambo pamoja na ukabila,solution sio Tanganyika ni katiba mpya ambayo itafanya huu ushenzi unaoendelea impossible
 
Utovu kama huu, .hata mimi nakuvunja miguu tuu 😂😂😂
 

Nashangaa umeandika yote hayo, lakini haujagusia yaliyotokea October 29. Hauoni kuwa hiyo ni moja ya sababu iliyoligawa taifa?
 
Nasisitiza acha upotoshaji, bunge lile lilikwenda hadi mwisho japo kuna waliosusia. Na katiba pendekezwa ilikuwa unasubiri kura ya maoni, ni bahati tu Magufuli aliigomea, na hakuigomea kwasababu wapinzani walitoka, bali alitaka atawale kwa katiba hii hii ambayo rais ni Mungu mtu. Kwa taarifa yako Magufuli angetaka kura ya maoni ingepigwa, na ingepita kwa matakwa ya serekali, na sio lazima wananchi. Hakuna mtu anayekupinga boss, bali ninakutaka uache upotoshaji.

Kama unaongelea uhalisia ni huu niliokumbia, na sio kutaka kujifichia kwenye hisia za uvyama wala nini.
 
Umerukaruka kujificha weee! Mwisho umejiweka hadharani. Hongera kwa Kalamu kumfichua huyu mnafiki.

Umeshindwa kujibu vipi kuhusu Samia?
 
Mkuu wewe unachoongea hapa ni matokeo tu. Ni consequences za mfumo mbovu uliowezesha utawala wa ovyo kukamata uRais wa JMT na kuutumia kufanya mambo ya ovyo sana. Hilo kundi baya halikuzuka tu. Kwa miaka mingi CCM imetengeneza na kulea mazingira yanayowezesha watu wa ovyo kushika madaraka ya nchi. Wote tunatakiwa kupambana kuondoa hayo mazingira ya ovyo. Shida kubwa ni watumainia fursa na wajinga (ignorants) wengi waliojazana kwenye ufuasi wa CCM ngazi zote.

JF ni kielelezo kikubwa. Mifano kadhaa. Kuna wadau hapa waliunga mkono sana hatua za utawala wa 5 za kubana uhuru wa shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani, uhuru wa vyombo vya habari na utoaji maoni, kinyume cha kkatiba na sheria na kutumia vitisho na hit squads (watu wasiojulikana) kutishia, kutesa na kuua wakosoaji wakidai ni "wasaliti" na "wahaini". Walifumbia macho hujuma kubwa iliyofanywa kwenye chaguzi za 2019 na 2020. Leo hii watu hao hao wanaulaani sana utawala wa awamu ya sita kwa kukithiri zaidi katika mambo ya aina ile ile. Kama vile ni kitu kipya na cha kushangaza sana kwao.

Wengi hawaoni tatizo la msingi ndani ya CCM. Bali wanajiaminisha na kutaka kutuaminisha kuwa tatizo kubwa ni uongozi wa awamu hii TU na kumlaani Mabeyo kwa kazi aliyofanya kumwezesha Rais aliyepo kuingia madarakani. Wamesahau kwamba ni wao waliokuwa wakiunga mkono uamuzi wa awamu ya tano kuhusu kupuuzia marekebisho ya katiba na kuminya mifumo na michakato yote ya kidemokrasia. Hata huku mitaani tunawasikia sana. Wanalaani kweli kweli utawala uliopo lakini hawaoni kabisa uozo wa tawala zilizopita. Wanataka tuamini kuwa kabla ya sasa mambo yalikuwa mazuri.

Kuna wengi leo hii ikitokea Rais wa awamu hii akaondoka madarakani (kwa namna yoyote ile) halafu mmoja wa inner circle ya awamu iliyopita akachukua nafasi yake, hawatakuwa na tatizo tena. Hata madai ya kutaka mabadiliko ya katiba na mfumo wa uongozi wa nchi hayatakuwa kipaumbele chao tena. That's really troubling.

This is a systemic problem. Everyone should see it as such. Lakini ni tatizo ambalo limekwamishwa muda mrefu sana na wasaka fursa (opportunists) waliojazana ndani ya CCM na uelewa mdogo wa wananchi wengi.
 
Nashangaa umeandika yote hayo, lakini haujagusia yaliyotokea October 29. Hauoni kuwa hiyo ni moja ya sababu iliyoligawa taifa?
Ukinisoma vizuri ya October 29 ni matokeo Utovu wa UTU na UZALENDO kwa Taifa.
 
Shukran, it goes like this-
Tuna MFUMO mbovu wa Demokrasia Usiozingatia MISINGi ya Demokrasia.
 
100%✔️
 

Wakati wa kampeni tulikuwa tunasema CCM OYEEEEEEEE...MAMA anaupiga mwingi sana hadi unamwagika hadi Magari yetu tukaweka T 2030 SSH.

Hii tuliipenda wenyewe na bado Mama atetewe...leo mtasemaje tumefikaje????

CCM BABA LAO tukutane 2030
 
Sijui ni wapi tunaposigana mkuu 'Drifter'.
"Muundo mbaya ndani ya CCM", ambao ndio umetufikisha hapa leo uliwekwa nyakati zile kwa sababu maalum; za kuepuka yanayotokea leo. Badala yake, ukawa wa kudumu, na hao waliokuwa wadhibitiwe na muundo huo, sasa wamepata fursa ya kuutumia na kushika hatamu ya chama.

"...kulea mazingira yanayowezesha watu wa hovyo kushika madaraka ya nchi." Maneno mazito na sahihi kabisa yanayoendana na kauli zilizozoeleka ndani ya chama, kama :"Huyu ni Mwenzetu"; mwenzetu katika nini katika uongozi wa chama?

Imenilazimu jana kutumia muda kuangalia watu walioko kwenye Kamati Kuu ya Chama na Halmashauri ya Taifa (NEC) ya chama hicho!
Hawa siyo watu waliowekwa huko na hawa wanachama wa kawaida wa CCM tunaowahusisha sasa na ubovu wa chama chao. Na hivi ndio vyombo muhimu vinavyoamua maswala mazito ya chama, na hatimaye ya nchi nzima!

Kwa hiyo, kimsingi tunakubaliana kati yetu juu ya ubovu wa chama kutokana na mfumo mbaya unaowezesha kuingiza viongozi wabovu kwenye uongozi; na kwamba baadhi (kundi kubwa la wana CCM) wamo ndani ya chama kwa sababu tu za kimaslahi yanayotokana na kuwa mwanachama wa chama tawala.

Sehemu ambayo huenda bado kuna tofauti kubwa kati yangu na wewe ni upande wa uhusika wa wanachama wengi wa CCM kukubali matokeo ya uongozi wa chama kama yalivyo sasa.
Ni hoja yangu kwamba, pangetokea fursa ya kuwapa uhuru wa kueleza maoni yao juu ya chama chao leo hii, wengi wa wanachama hawa wasingetofautiana sana na sisi waTanzania wengine tusiokuwemo kwenye chama hicho
 
Hakuna sababu ya uwepo wa Muungano tena. Nafikiri hili ndilo jambo la muhimu zaidi sasa hivi kuliko hata hiyo Katiba Mpya.
Tanganyika irudi, na watu waendelee na shughuli zao badala ya kupoteza muda na Muungano usiokuwa na faida yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…