Hiyo ni dhana yako wewe, waulize watu wa zamani hapa kijiweni hususa Mwanajiji na Rev.Kishoka hata hao viongoI wa Chadema kina Mnyika walikuwa hapa enzi zile za kina Zitto, Maria Sarungi (Woman of substance) Kitila n.k watakwambia mimi ni mtu wa aina gani na ipi misimamo yangu katika mijadala kama hii.Najuwa wewe ni mtu mbishi.
Basi tutajie nchi yoyote yenye vyama pinzani wanaoitana kuwa ni vyama rafiki.
Mkuu 'Mkandara' wewe unajulikana siku zote msimamo wako upo wapi katika haya maswala ya Tanzania. Huna tofauti kubwa sana na 'zealots' wengi humu kama akina Ritz, BIG SHOWW na wengine.
Tofauti yako ni kuwa huwi bayana kama wao. Unajaribu kila uwezavyo kufunika maana ya maandishi yako uonekane upo balanced.; kama utumiaji wa maneno kama "UTU" niliyoyanyanyua hapo mwanzo kabisa.
Kwa ufupi, watu wa aina yako ndio hatari zaidi ya hao wanaojitokeza waziwazi kama hao niliowataja hapo juu.
Sasa wewe nieleze uhasama huu utatatua vipi hali yetu hii inayotukabili, huku watu kama wewe mnafunikafunika uwazi wenu usijulikane.
Halafu unauliza na swali kabisa: Eti "Tumefikafikaje hapa tulipo"?
Kwani hujui?
Hili la "wafuasi wa CCM" tuwe wakweli wenyewe.Endapo, wafuasi wa CCM hawataona hayo kuhusu chama hicho
Watu wa zamani hapa ni akina nani kama hata hujui unayejadili naye na anakueleza hayo hayo aliyoyashuhudia toka huko mwanzo.Hiyo ni dhana yako wewe, waulize watu wa zamani hapa kijiwen
Leo hii nimechukua zaidi ya masaa manne kuwasikiliza viongozi wastaafu, maprofesa na wadau mbali mbali katika mdahalo uloandaliwa na TLS.
Hakika nimejifunza mengi na yanilazimu kuwashukuru sana Mzee wetu Jaji Warioba, Profesa Shivji, Mwanasheria kutoka Kenya, Profesa Tibaijika, viongozi wa vyama vya Siasa na taasisi nyinginezo hususani TLS wenyewe. Wote kwa ujumla wao wamezungumzia mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.
Pamoja na yote yale wameniachia maswali magumu zaidi nimekaa na kujiuliza hivi tatizo hasa lipo wapi? Na tumefika hapa kwa sababu gani?
Kubwa zaidi lilojitokeza kwangu linatokana na hotuba ya Profesa Shivji alipozungumzia Misingi mikuu ya Demokrasia akifafanua juu ya pande mbili yaani upande Wananchi na upande wa Utawala. Na kilichojitokeza wazi kwangu ni Kupotea thamani na heshima ya UTU wetu. UTU ndio kiashiria cha ujenzi na usimamizi wa Uhuru na Usalama.
Taifa letu limepoteza UTU kiasi kwamba Utawala hauthamini wala kuheshimu Wananchi na Wananchi hawawathamini wala kuheshimu Viongozi wake. Haiishi hapo, tumefikia kiasi kwamba Utawala hauheshimu viongozi wenzao na Wananchi hawathamini wala kuheshimu Wananchi wenzao.
Na katika hali hii, Uhuru na Usalama wa wananchi upo hatarini kama ilivyo kwa viongozi wenyewe hawaaminiani wala hawaheshimiani isipokuwa kwa yule mwenye nguvu ya utawala na fedha, hii ndio Tanzania ya leo (status quo)
Swali linakuja tumefikaje hapa? Naamini kila mtu ana mtazamo wake lakini binafsi yangu akili yangu inanambia yote haya yametokana utovu wa nidhamu katika miiko na maadili ya UTU wetu kwa kuiga mifumo ya kigeni ambayo ilidhalilisha mila na tamaduni zetu kama ni misingi ya kale (primitive) ilopitwa na wakati.
Mifumo ya Demokrasia tuloichukua ndio chanzo cha kuharibika kwa misingi ya Demokrasia kupitia mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002. Isipokuwa nitaacha pembeni Katiba ya Zanzibar, hii inahitaji mada nyingine tofauti kabisa.
Najua hoja yangu inahitaji mjadala mpana zaidi lakini niseme kwamba mabadiliko haya ndio mwanzo wa matatizo yote yanayofuatia katika miongo tofauti ya Kiutawala kufikia leo hii.
Katika makosa makubwa yalofanyika ni kuondolewa kwa Miiko na Maadili ya Viongozi hivyo kupoteza Sifa zinazotakiwa za viongozi wetu Kitaifa. Kwa nafasi walizokuwa nazo viongozi serikalini, Wabunge na hata majaji wakaanza kumiliki utajiri pasi kuulizwa wamepataje mali na utajiri huo, hii njia panda ndio ikawa mwanzo wa mmomonyoko wa maadili na chachu ya rushwa kuzaliwa.
Jambo la pili lilikuwa ujio mfumo wa Vyama Vingi ambavyo havikuzingatia misingi ya Demokrasia ( Uhuru, Utu na Usalama) bali ilikuwa ni tiketi ya jicho la Uheshimiwa na kuingia Ikulu kutawala (mfumo wa Vyama vingi). Vyama vingi ndivyo viloweka nadharia ya kina nani watakuwa Waheshimiwa kati ya Wananchi wote na hii ikazaa tamaa ya utukufu wa nyadhifa hizo. Hakuna Chama hata kimoja kinachosimamia itikadi na Sera zake wakati wote ila kulingana na fursa zinazojitokeza.
Katika mukhtadha huo tulipoteza Siasa safi za vyama Kiitakadi, hasada ikachukua nafasi baina ya vyama vya Siasa, viongozi kwa viongozi, Wananchi na vyama pinzani na kibaya zaidi rushwa na upendeleo vikatumiwa kama zana katika teuzi toka chaguzi za ndani ya Vyama vya Kisiasa hadi Viongozi wa Kitaifa – Yakaibuka makundi ya timu za Wana, hasada ikazaa Chuki na Uadui matokeo yake UZALENDO kwa Taifa letu UKAPUKUTIKA.
Kwa hiyo tukiacha hoja ya Katiba Mpya pembeni, sisi Watanzania tuna wivu na chuki za kuhasimiana wenyewe kwa sababu ya fursa za madaraka na utajiri zimeletwa kupitia vyama vingi.
Viongozi waliopo madarakani hujiona wapo katika nafasi adimu sana ya Utajiri wa hadhi na mali na wanajua kuna macho ya wivu dhidi yao hata kama wanayofanya nia njema ama kinyume cha misingi ya demokrasia, bado utachikiwa tu. Siasa zetu zimekuwa ni za Ukinzani ambazo kiitikadi hazifanani kabisa na Upinzani kwa nia, dhamira na malengo ya Demokrasia.
Tujiulize wenyewe mpaka hapa tumefika ni viongozi wangapi wameuawa kwa ajali, risasi au sumu na hakuna watu walotiwa hatiani wala kuchukuliwa hatua. Nini hasa sababu za viongozi hao kuuawa? Bila shaka ni kunatokana na UADUI wa kisiasa walojenga dhidi ya kiongozi ama viongozi wengine iwe kwa nia safi au mbaya.
Wivu na Chuki sii lazima vitumike kwa wale washindani tu bali inaweza toka chini kwa wale wanaotaka kufika pale kiongozi alipofika ama kiongozi kulinda maslahi yake dhidi ya wale wanaotaka nafasi yake.
Kwa hiyo tunapozungumzia leo Maombolezi, Maridhiano na sijui Katiba Mpya ni muhimu kwanza sisi wenyewe tukubali mapungufu yetu kimaadili ili TUBADILIKE - Heshima ya Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa ni utamaduni ulopitwa na wakati.
Hatuwezi fanya maombolezi ambayo baadhi yetu hawaoni umuhimu wala sababu. Hatuwezi fanya Maridhiano kwa kuwekeana masharti yasiyojali Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa hili bali maslahi ya mtu au chama.
Mwisho hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi wenye wivu, chuki na uadui isipokuwa Katiba lazima iwe ni mwongozo wa Wananchi hao bila kujali tofauti zao - Katiba ni ya Wananchi iheshimiwe na wote.
Maasalaam
Nimesoma hayo unayoyaita maoni yako na kikubwa nilichoona ni kwamba yana VIASHIRIA VYA UHAINI.Shukran saana, kwa hoja hii ya msingi kabisa ambayo hata mimi yanipa shida kusema kwa uhakika tunawezaje kutoka hapa.
Hatuwezi kurudisha UTU wetu kwa maandishi kwa sababu hata Katiba hii mnayosema mbovu haifuatwi katika maswala ya msingi kabisa.
Ninewahi tolea mfano HAKI ambayo ipo ndani ya Katika Sura ya kwanza sehemu ya 3 lakini imekiukwa wazi wazi kabisa mpaka tumefikia mauaji ya Watu wasokuwa na hatia na hata walikuwa na hatia utawala ulishindwa kufuata taratibu za Kisheria. Hii yote ni kutokana na kupoteza Heshima na thamani ya UTU wetu badala yake tumeishi kwa Mazoea...
Ukiniuliza mimi nitasema hivi. Hatuwezi kuwa na siku ya maombolezi, siku ya Maridhiano wala Katika Mpya/Mpito pasipo kuwa na - SERIKALI YA MPITO. Tunaipataje?
Sina maana rais apinduliwe au aondolewe kwa nguvu madarakani kwa sababu hatutaki kumwaga zaidi damu za Watanzania na kusababisha uadui mkubwa zaidi isipokuwa dhahiri hatuwezi kifikia muafaka wa aina yeyote Rais akiendelea kuwepo madarakani.
Ataondokaje Madarakani?
- Rais akubali kuwa Bangusilo kwa kulinusuri Taifa hili na manufaa ya wote - AJIUZURU yeye mwenyewe kwa hiari yake akithamini UTU wa Watanzania na Katiba itamlinda. Hakuna njia nyingine salama na yenye baraka kwetu nayoiona mimi.
Tukubali sote hatashtakiwa, atalindwa na mafao yake ataendelea kupata kama marais wengine wastaafu walomtangulia. (It's Win win situation on both sides) Tukumbuke rais ana mamlaka makubwa sana na akikataa hakuna kitakacho fanyika iwe maombolezi, maridhiano wala Katiba Mpya/ya Mpito. Huu ndio Ukweli mchungu.
Kustaafu kwake, Kikatiba kutatupa mwanzo mpya, tutaunda Serikali ya Mpito, tutaweza kuomboleza sote kwa pamoja, tutaweza kufanya maridhiano ya pamoja na sii lazima Uchaguzi Mkuu ufanyike 2030. Ni mpaka pale tumeweza kukamilisha maswala yote ya kutuunganisha Wananchi Upya kama jamii moja ya Watanzania.
Nimeandika haya kama mtazamo na maoni yangu naomba sana isitiafsiriwe vinginevyo.
Maasalaam
Una hoja....sijasoma mada ila tumefika hapa kwa kutembea kwa mguu taratibu taratibu tu
Exactly! Mkapa alutuachia janga.Uchaguzi wa Mwaka 2005 ndio uliopanda siasa mpya za nchi hii. Matokeo mengine yote mbegu ilianzia pale na mnakumbuka pia 2010 JK alivyosaka kura kwa kusaidiwa na familia! Kila uchaguzi umekuwa chanzo cha mipasuko na kuzaa makundi yanayohujumiana. Uchaguzi wa 2025 ilikuwa kilele cha matatizo ya muda mrefu. Kuelekea 2030 kama tusiporudi kwenye misingi tutaingia nchi kwenye matatizo yaliyopo Congo.
Mgawanyiko wa CCM mwaka 2015 ilikuwa ni descendant ya uchaguzi wa mwaka 2005.Hapana Uchaguzi wa 2015 nadhani ndio ulotugawa zaidi makundi. CCM kule wakagawanyika JK na Lowassa! Chadema Dr. Slaa na Lowassa lakini yote kwa pamoja ni Kusaka Uheshimiwa kuingia magogoni.
Kila upande focus kubwa ilikuwa kuingia Ikulu sio kuwatumikia Wananchi. Na hili limekuwa likisemwa na vyama vyote kwamba nia na dhamira ya Vyama vya Siasa ni Kuingia Ikulu. Wee Mwananchi sio priority yao bali ni njia ya kuwafikisha magogoni. Chama kikisha kuwa na dhamira hiyo, mbinu zake lazima hazitakuwa nzuri hata kidogo, kuua, rushwa na wizi vyote vinaingia katika mbinu zake maadam zimefanikiwa.
Ndio kawaida yenu watu wa Chadema, mkipigwa pini tu mnaanza kwenda personal!Watu wa zamani hapa ni akina nani kama hata hujui unayejadili naye na anakueleza hayo hayo aliyoyashuhudia toka huko mwanzo.
Au Alzheimer ilishakuingilia tayari?
Mambo yako yapo vilevile, kama yalivyokuwa huko mwanzo, hujabadilika chochote.
Hata sijui kama Kibara bado unajuwa ipo wapi katika kumbukumbu zako.
Unapointi haswa!Uchaguzi wa Mwaka 2005 ndio uliopanda siasa mpya za nchi hii. Matokeo mengine yote mbegu ilianzia pale na mnakumbuka pia 2010 JK alivyosaka kura kwa kusaidiwa na familia! Kila uchaguzi umekuwa chanzo cha mipasuko na kuzaa makundi yanayohujumiana. Uchaguzi wa 2025 ilikuwa kilele cha matatizo ya muda mrefu. Kuelekea 2030 kama tusiporudi kwenye misingi tutaingia nchi kwenye matatizo yaliyopo Congo.
sijui ni mara ngapi wewe umenihusisha na CHADEMA.Ndio kawaida yenu watu wa Chadema, mkipigwa pini tu mnaanza kwenda personal!
Lugha yako mkuu pekee inakuacha Uchi. Mtu yeyote anaye wachambua wafuasi wa Chama kingine cha Siasa kwa imani zao tayari inamweka yeye upande wa pili. Isitoshe kauli zako kwangu zinaashiria wazi unadhani mimi CCM na hata kama niwe CCM sidhani kama ni kosa au hoja ya msingi kwa sababu sote KIKATIBA tuna HAKI sawa ya kujiunga na chama chochote cha Siasa. Mzee Warioba mpaka kesho ni CCM unamuonaje?sijui ni mara ngapi wewe umenihusisha na CHADEMA.
Ulikwishaona mahali popote nikidai kuwa nipo CHADEMA?
Kwani siwezi kuzungumzia maswala ya Tanzania bila kuwa ndani ya chama chochote?
Nijuavyo, wewe hata huko CCM hupo; bali unatetea huko kwa sababu zinazojulikana
Mimi nawatetea CHADEMA sasa hivi, kwa sababu ni tofauti kabisa na hiyo CCM unayoitetea wewe; na huipendi CHADEMA kwa sababu ndiyo inayotishia maslahi yanayokufanya uambatane na CCM bandia inayovuruga utulivu wa taifa hili.
Achana na unafiki, kuuliza maswali ambayo unajuwa majibu yake.
Unayo matatizo 'Mkandara'.Nilimkosoa Mkapa enzi za #Jambofurums, tukahamia #Bcstimes wakati wa JK na tukamkoma nyani vizuri sana zile scandal za Richmond, Tanesco na Dowans.
KIongozi pekee ambaye mimi binafsi nakiri nilikuwa upande wake muda wote ni Magufuli kwa sababu simkubali Lowassa na hata Tundu Lissu maana sio viongozi wanao nivutia kwa sifa, iitikadi wala kimaadili.
Hilo halina Ubishi kabisa lakini siwezi kukidharau chama chochote au Wanachama wake kwa sababu ya misimamo ya Kiongozi wake. Labda niseme ACT Wazalendo pekee ndio chama nachoshindwa kabisa kuelewa mwelekeo wake.
Daaah, sababu gani hizo? ebu nijulishe maana miye sijui kama nawatetea CCM. Na sijui kama nayoyasema hapa yataniacha salama jambo ni imani yangu kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.sijui ni mara ngapi wewe umenihusisha na CHADEMA.
Ulikwishaona mahali popote nikidai kuwa nipo CHADEMA?
Kwani siwezi kuzungumzia maswala ya Tanzania bila kuwa ndani ya chama chochote?
Nijuavyo, wewe hata huko CCM hupo; bali unatetea huko kwa sababu zinazojulikana
Mimi nawatetea CHADEMA sasa hivi, kwa sababu ni tofauti kabisa na hiyo CCM unayoitetea wewe; na huipendi CHADEMA kwa sababu ndiyo inayotishia maslahi yanayokufanya uambatane na CCM bandia inayovuruga utulivu wa taifa hili.
Achana na unafiki, kuuliza maswali ambayo unajuwa majibu yake.
Hii siyo mbinu mpya hata kidogo kwa watu wa mlengo wako.Lugha yako mkuu pekee inakuacha Uchi. Mtu yeyote anaye wachambua wafuasi wa Chama kingine cha Siasa kwa imani zao tayari inamweka yeye upande wa pili
Najuwa hata CHADEMA walitamani sana "aachie" kama ulivyosema wewe; sasa sijui tatizo lako na CHADEMA ni lipi; kwa sababu ya Tundu Lissu pekee?Hivi kweli kuna mtu hapa (at that time and day tarehe 31 October 2025) aliweza kusema hadharani kumtaka rais Samia ajiuzuru kulinusuri Taifa? I did that...
Kifupi Mkuu wewe unamkubali Tundu Lissu kwa sababu zako nami nilimkubali Magufuli kwa sababu alifanya exactly Chadema walivyojitangaza kabla ya Uchaguzi wa 2010 - 2015 baada ya kuona nchi hii haitawaliki pasipo kumpata rais DIKTETA. Rais anayeweza kufanya maamuzi magumu na sera zikaandaliwa ambazo Magufuli alizifuata.Unayo matatizo 'Mkandara'.
Sasa eleza ni nani hakuwepo Jambo, au BUsinessTimes. "Kumkoma Nyani Giledi", mbona ni juzi hapa na lile dude la Malicela!
Nasema unayo matatizo, kwa sababu hapa unajifanya kumkubali Magufuli; kwa sababu tofauti kabisa na hizo ulizotaja wewe. Magufuli alikuwa na "itikadi" zipi za kusema zilikuvutia. "Maadili? kwa magufuli?
Magufuli alikuvutia kwa sababu zilezile nilizozitaja walizo nazo akina Ritz na watu wa aina hiyo.
ACT na CUF najuwa huna habari navyo kabisa vyama hivyo. Hukuhitaji hata kuvitaja kabisa. ulaghai wote huu hasa ni wa nini?
Ni hivi: kama hunijui, mimi huwa sina simile na watu wanafiki. Siwezi kamwe kusema nyeusi ni nyekundu. Nitaisema vilevile ilivyo.
Kutompenda kwako Lissu, inawezekana ikawa ni kwa sababu hizo hizo za yeye kutopindisha mambo.
Vipi, unamwonaje Samia, maana hujamzungumzia kabisa.
Waambie waTanzania kwa umoja wao na wingi wao washirikiane na chama kufanya kazi hiyo. Inawezekana sana.Umenena vyema! Wa kututoa hapa tulipo ni kichaa mmoja tu atakayejitokeza kutoka JWTZ. Tusitegemee viongozi wa vyama vya siasa kwamba ndio watatuondoa kwenye huu mkwamo! Bahati mbaya tumekuwa na Jeshi ambalo nalo linaongozwa na machawa! Shenzi kabisa!