Mtu Asiyejulikana
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 1,694
- 3,982
Hali ya Maisha inazidi kuwa ngumu. Why jamani, why? Kila siku watu wakiamka afadhali na jana. Serikali yetu kwa sasa haijielewi kabisa. Haieleweki kuna watu wanampotosha Rais.
Kuna watu wanamshauri vibaya makusudi. Wanamshauri vibaya nchi ionekane imemshinda. Maisha haya hatukutegemea. Kila kitu kimepanda bei upandaji bei wa Petrol wa safari hii ni wa kishetani. Haya yote yanafanyika watu hata hawamwambii Rais.
Wamechukulia Ubusy wa Rais vibaya. Wanaamua kukomoa wananchi. Nchi imekuwa ngumu maradufu. Hakuna anayewatetea wananchi wasio na uwezo.
Mafuta yanapanda kwa tsh 300 nzima? Tunaenda wapi ndugu Watanzania? Ni wapi tunakwenda? Hawa watu wanaofanya hizi biashara watatuumiza mpaka lini?
Rais jamani aambiwe maana najua wanamficha hii michezo yao michafu. Wanapandishia humo humo kwa kisingizio cha soko la Dunia. Tunajua hii mipango hasa ikiratibiwa na watu ambao awamu iliyopita walikuwa wanapora maeneo na kuanzisha vituo vya mafuta.
Tunajua watu ambao wamerudishwa kwa ajili ya kuja kumalizia ngwe nyingine ya upigaji. Jamani mkila na kipofu msimshike mkono.
Watu wanakula mpaka wanavuka urefu wa kamba zao. Na haya yote Mhe Rais haambiwi. Na watu wanamshauri vibaya sana. Wanamshauri kwa nia ya kumwaribia.
Ionekane nchi imeshamshinda. Kila kitu kinaenda kiholela holela. Hadi Panya road wanafunga mitaa polisi wamejazana barabarani wakisidiana na traffic. Kwa sasa traffics wamekuwa wengi kuliko askari wa kulinda usalama wa raia .
Kwa kweli kwa hali hii tumedondokewa na kitu kizito chenye ncha kali utosini.