Tume yakatiba mpya imechoka kazi?

Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
396
65
Ndugu Watanzania na ndugu wana jamvi Tume yetu ya katiba imeanza kupoteza mwelekeo. Hivi majuzi Tume ameandika barua kwenye wizara na Taasisi za serikali ikitaka Wakuu wa Taaisisi hizo wasaidie kukusanya maoni ya watumishi sehemu za kazi.Hivi maoni yatakayokusanywa na waajiri yatakuwa ya aina gani? na ni mtumishi yupi atakuwa na ujasiri wa kutoa maoni bila woga? Tume imewezaje kuchukua maoni ya wananchi mikoani ishindwe kutengeneza utaratibu madhubuti wa kuchukua maoni kwenye Taasisi za Serikali? Hivi huo ndio uhuru wa kutoa maoni? Wamechoka nini? Tunasema hivyo kwa sababu tunaona sasa mwelekeo wa kutaka maoni ya mkondo mmoja kwa kutumia nguvu ya watumishi. Inawezekana Tume imepitiwa kwenye hili lakini tunajua wana fedha za kutosha, magari, wanaishi mahali pazuri na kila kitu wanapata. Tunataka wafanye kazi waliyotumwa na Mhe. Rais siyo kuwapa watu wengine mzigo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom