RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 3,590
- 8,475
Nguruka, nyangabo,bweru, itebula,mganza, Nguruka Kati,lugongoni A&B hapawezi pakatoa mtu mwenye Mawazo kama wewe. Unawaaibisha wana MAGEUZI wa Nguruka.Mimi ni Mwananchi mwenzako ila nakiri hapa unatulisha tango pori. Naweza kusema ndugu yangu Kijana katika hoja yako umekurupuka maana Aliyetia neno kuhusu uchumba wa CHADEMA na ACT wala sio Time bali ni Msajili wa Vyma vya Siasa ambaye ndie msimamizi wa hivyo vyama.
Hebu itafute barua waliyoandikiwa ACT au Chadema Kisha usome anuani imetoka wapi.
Lakini pia, Sheria za Uchaguzi zipo wazi nadhani Tume Kama ingesema kitu katika hilo ingetaka tu Mgombea aliyetangaza kujitoa katika ulingo wa Uchaguzi kuandika barua ambayo ingethibitishwa na Chama chake na Kisha kuiwasilisha tume kabla ya Saa 12 jioni.
Ila sina hakika Kama Benard Kamilius Membe hadi Sasa amesha toa taarifa Tume ya Uchaguzi na Kama wamesha toa Basi Mkurugenzi wa Tume ataitaarifu umma juu ya hilo Kama alivyofanya kwa wagombea wa majimbo ya Chalinze na Madaba walioingia mitini.
Hivyo ndugu yangu hili andiko lako umelikosea na umelenga kuwapotosha wasomaji wa JF na kuwaaminisha kuwa Time ya Uchaguzi ndiyo inakosea. Ilhali ni taasisi nyingine.
Lakini Mbona unauhakika gani Kama TLP na UDP hawakufuata utaratibu wa kutoa taarifa mapema ya kuunga mkono Mgombea wa CCM? Je unavithibitisho? Kumbuka TLP na UDP wao hata Tume hawakusogea kuchukua Fomu lakini ACT alifika na kuchukua Fomu na akateuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais, hivyo mimi nadhani tunadili pia huo utofauti wa Ambaye hajachukua Fomu na aliyechukua na kuteuliwa kuwa Mgombea.