Tume ya Uchaguzi itafanya maboresho daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia BRV

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Kama kuna wakati upinzani uliusubiri kwa hamu sana nadhani ni huu. Tume ya uchaguzi imetangaza kuja na mfumo mpya wakaundikisha wapiga kura kwa BVR ( Biometric Voters Registration) ambapo viparata vya zamani vitatupiliwa mbali na kuwa na vitambulisho electronic. Kazi imebaki kwa upinzani kuhamasisha wapiga kura wapya kujiandikisha maana inakadiliwa wapiga kura zaidi ya milioni saba hawajajiandikisha na waliojiandikisha wengi wamepoteza vitambulisho vyao au kuhama maeneo walikojiandikisha.
====================================

Jaji%20mstaafu%20Damian%20Lubuva%2C%20mwenyekiti%20wa%20tume%20ya%20taifa%20ya%20uchaguzi%20NEC.jpg

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi chini Tanzania (NEC) jaji mstaafu Damian Lubuva

VITAMBULISHO vya kupiga kura nchini, vitatolewa upya kwa wananchi wote, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuboresha daftari la kudumu la wapigakura. Mchakato huo wa kutoa vitambulisho upya, utakaotekelezwa Septemba mwaka huu, utagharimu Sh bilioni 293 .

Tofauti na vitambulisho vya awali vya karatasi vilivyotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2004, vipya vitakuwa vya plastiki. Vimebadilishwa kutokana na matumizi ya teknolojia mpya katika uandikishaji.

Teknolojia itakayotumika ni ya Biometric Voter Registration (BVR), ambayo inachukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika Kanzidata (database) kwa ajili ya utambuzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema hayo jana wakati akifungua mkutano kati ya tume na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura.

Alisema katika uboreshaji huo, wapigakura wa zamani, kwa maana waliokuwa kwenye daftari la sasa, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole, picha na saini zao katika mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho vipya.

Alisema vitambulisho hivyo vipya, vitatolewa papo hapo uandikishaji ukikamilika na vitakuwa vya plastiki ngumu na namba ya mpigakura itakayoonekana kwenye kitambulisho hicho, itakuwa ni ya kudumu na pekee kwa mpiga kura husika.

"Vitambulisho hivi vitatumika kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na kura ya maoni ya Katiba mpya na kuhitimisha matumizi ya vitambulisho vya wapiga kura vya awali," alisema Lubuva.

Akiwasilisha mada katika mkutano huo kuhusu maandalizi hayo kwa kutumia mfumo wa BVR, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema wapigakura watakaokuwa na kadi za zamani, watatakiwa kwenda na kadi hizo katika kituo cha kujiandikisha kurahisisha kuhamisha taarifa zao za awali katika mfumo mpya.

"Hata hivyo, kupotea ama kuharibika kwa kadi ya awali, hakumzuii mpiga kura kwenda kituoni kujiandikisha na kupewa kadi mpya," alisema.

Wenye umri miaka 17 Alisema kundi lingine litakalohusika katika uboreshwaji huo ni watu ambao ifikapo siku ya uchaguzi mkuu mwakani, watakuwa wametimiza umri wa miaka 18.

Pia, wale ambao hawakuwahi kujiandikisha katika madaftari yaliyopita kwa sababu mbalimbali, watahusika katika uboreshaji wa daftari.

Alisema baada ya kukamilika kwa uboreshwaji huo, daftari la awali litawekwa wazi katika maeneo husika na tarehe za ukaguzi, zitatangazwa ili kila aliyejiandikisha kwenda kukagua na kuona kama taarifa zake, zimeandikwa na kuchukuliwa kwa usahihi.

"Kipindi hicho pia kinatoa nafasi kwa wapigakura waliojiandikisha katika kata kuweka pingamizi kwa wale watakaoonekana wameandikishwa katika daftari lakini hawana sifa kama wasiokuwa raia au wasiotimiza umri unaotakiwa kisheria," alisema.

Alisema matumizi ya mfumo wa BVR, yataweza kutoa majibu kwenye changamoto zilizojitokeza katika mifumo mingine iliyotangulia na kuwezesha kuondoa wapigakura, waliojiandikisha zaidi ya mara moja, kutambua wapigakura siku ya uchaguzi na kuhamisha wapigakura waliohama.

BVR ni uandikishaji tu Hata hivyo, Lubuva alisema mfumo huo wa BVR utatumika kwa ajili ya kuandikisha wapigakura pekee na si kwa ajili ya kupiga kura kielektroniki au vinginevyo.

Alisema matumizi ya mfumo huo, yametokana na changamoto zilizojitokeza katika matumizi ya Optical Mark Recognition (OMR) na kufanya daftari la kudumu la wapigakura kuwa na kasoro na kusababisha wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Lubuva alisema vifaa kwa ajili ya kazi hiyo vimekwishaagizwa. Tume itavipokea Agosti mwaka huu ili kuanza uboreshaji huo huku vifaa vichache kwa ajili ya mafunzo kwa watendaji vitapokewa mwezi Julai na kuanza mfunzo hayo.

Uandikisha kwenye vitongoji Alisema kwa sasa uandikishaji utafanyika katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa, tofauti na awali ambapo vilikuwa katika ngazi ya mtaa. Sasa vituo vya kujiandikishia, vimeongezeka kutoka 24,919 hadi 40,015 ili kuwa karibu na wananchi na kuongeza mwamko wa kujiandikisha na kupiga kura. Mchakato wa uandikishaji ukianza, huduma zitakuwepo kwa siku 14 kituoni.

Maandalizi Alisema maandalizi ya awali yamekamilika, kinachofuata ni mafunzo na kuanza uboreshwaji wa daftari utakaogharimu Sh bilioni 293 wanazopata kutoka serikalini na tayari sehemu ya fedha, wameshapokea na kutumika kukagua vituo .

Naibu Katibu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Tehama, Dk Sist Cariah, akizungumzia suala la vitambulisho vya taifa na hivi vya wapigakura, alisema vitambulisho hivyo ni tofauti kwani wao wanatoa kwa ajili ya kukamilika kwa muda maalumu lakini vile vya taifa ni endelevu.

Alisema kwa sasa, vitambulisho vya taifa hawajakamilisha kutoa hata Dar es Salaam pekee hivyo ni vigumu kutumika kwa uchaguzi ujao na kura ya maoni kwa Katiba mpya lakini wakikamilisha vitambulisho vya taifa , vitatumika katika uchaguzi.

Alisema katika mfumo huo mpya, watawasiliana na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuweza kuwaondoa wote waliofariki kwa kutumia takwimu za hospitalini na vyeti vya vifo vitakavyotolewa.

Chanzo;Habari leo
 
Kama kuna wakati upinzani uliusubiri kwa hamu sana nadhani ni huu. Tume ya uchaguzi imetangaza kuja na mfumo mpya wakaundikisha wapiga kura kwa BVR ( Biometric Voters Registration) ambapo viparata vya zamani vitatupiliwa mbali na kuwa na vitambulisho electronic. Kazi imebaki kwa upinzani kuhamasisha wapiga kura wapya kujiandikisha maana inakadiliwa wapiga kura zaidi ya milioni saba hawajajiandikisha na waliojiandikisha wengi wamepoteza vitambulisho vyao au kuhama maeneo walikojiandikisha.

Hilo nalo ni "tatizo" ambalo linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi; binadamu kuhama ni suala la kawaida na naamini ndani ya miaka mitano maelfu kama sio mamilioni ya watu watakuwa wamehama vituo walivyojiandikisha/kupiga kura awali.

Mfano ulio dhahiri ni wanafunzi wa elimu ya juu ambao katika kipindi cha miaka mitano kuna waliohama huko walikokuwa na kujiunga na vyuo na pili waliomaliza vyuo (maeneo waliyojiandikisha) na kwenda kuishi sehemu tofauti pengine na walikokuwa wamejiandikisha kabla ya kuingia vyuoni.

Huo ni mfano mmoja, ila kiuhalisia binadamu tunahamahama sana. Ni jukumu la mamlaka zilizokabidhiwa haya majukumu kutafuta ufumbuzi.
 
Athanthe kwa taarifa, naomba usiishie hapa tu, ukienda na kwenye ghahawa na bao hakikisha unawafikishia ujumbe huu wa ukombozi, kazi ya kutoa elimu ni yetu sote kamwe tusiwaachie wapinzani.
 
Tusaidiane wote kuhamasishana na wala c kuwaachia wapinzani peke yao, jama wenzetu wa India, Zambia, malawi n.k waliweza kuziondoa Serikali zilizoko madarakani c kwa kutegemea Wapinzani ndo wafanye jitihada peke yao bali wanyonge wote wa Mataifa hayo walishikamana na wala c kuwaachia eti Viongozi wa Upinzi peke yao.

Tafakari na chukua hatua.
 
Shukrani kwa taarifa mkuu,tupo pamoja na ni wajibu wa kila mmoja wetu kusambaza elimu ya uraia kwa kila mtanzania.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepanga kutumia sh bilioni 293 kuandaa vitambulisho vipya vya wapigakura. Huu ni ufisadi. Hii kitu ilitakiwa iwe ktk mfumo mmoja na leseni za udereva, vitambulisho vya taifa n.k
Kifupi, haya yote yalipaswa yawe ktk kadi moja tu. Gharama zingepungua sana. Tungeokoa hizo bilioni 293 na bilioni nyingine nyingi zilizotumika kwenye leseni za udereva. Nasisitiza, haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Hii pesa ingejenga kilometa 300 za lami.
 
Leo nimemuona jamaa mmoja Mlimani TV anazungumzia jambo hilihili nikaanza kuona mantiki yake. Tumetumia kweli mabilioni kuandaa vitambulisho vya utaia (vya taifa), kwanini visiwe na taarifa pia kuhusu kupiga kura badala ya kuanzishwa tena vitambulisho kwa ajili ya kura peke yake? Hili li nchi aisee linaliwa na wenye meno
 
wewe MANYERERE ni sehemu ya utawala huu wa kifisadi umesahau mwaka 2005 ulivyozunguka nchi nzima kumpigia kampeni JK na EDO wakati huo? waandishi na viongozi wa dini mkawa mnawapotosha wananchi kuwa JK ni chaguo la MUNGU!yako wapi leo majigambo yenu?badala yake mmebaki kulalamika tu kwenye mitandao ya kijamii.KWA TAARIFA NA BADO NCHI ITALIWA MPAKA "KIELEWEKE" MZARAMO ANAONGEZA MUDA MPAKA 2020 MTAKOMA KURINGA!
 
maoni yako haya ni ya kitaalamu au unayatoa kadri unavyoona. Hebu dadavua kitaalam vipi, kitambulisho uraia, lesseni na kitambulisho cha kupigia kura kiwe kimoja?
 
Leo nimemuona jamaa mmoja Mlimani TV anazungumzia jambo hilihili nikaanza kuona mantiki yake. Tumetumia kweli mabilioni kuandaa vitambulisho vya utaia (vya taifa), kwanini visiwe na taarifa pia kuhusu kupiga kura badala ya kuanzishwa tena vitambulisho kwa ajili ya kura peke yake? Hili li nchi aisee linaliwa na wenye meno

Tuwasikilize na tume ya uchaguzi, wanaweza kuwa na mantiki ya kufanya hivyo
 
wewe MANYERERE ni sehemu ya utawala huu wa kifisadi umesahau mwaka 2005 ulivyozunguka nchi nzima kumpigia kampeni JK na EDO wakati huo? waandishi na viongozi wa dini mkawa mnawapotosha wananchi kuwa JK ni chaguo la MUNGU!yako wapi leo majigambo yenu?badala yake mmebaki kulalamika tu kwenye mitandao ya kijamii.KWA TAARIFA NA BADO NCHI ITALIWA MPAKA "KIELEWEKE" MZARAMO ANAONGEZA MUDA MPAKA 2020 MTAKOMA KURINGA!

sijaona sababu ya kumshambulia Manyerere. binafsi siungani naye kwa maada yake hii ila siyo kwa mtindo huu wa kumshambulia, tujiridhishe tu sababu za pande zote tume ya uchaguzi na wadau kama akina Manyerere, kila upande unaweza kuwa na sababu za kuvutia kwake. Jk hana uwezo kuwa kujiongezea muda wa kuongoza, Katiba ya nchi iko wazi mawazo kama ya kwako ni mawazo ya watu ambao hawajui misingi inayoliongoza taifa la Tanzania na tunaweza kuyaita mawazo ya kimipasho tu.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepanga kutumia sh bilioni 293 kuandaa vitambulisho vipya vya wapigakura. Huu ni ufisadi. Hii kitu ilitakiwa iwe ktk mfumo mmoja na leseni za udereva, vitambulisho vya taifa n.k
Kifupi, haya yote yalipaswa yawe ktk kadi moja tu. Gharama zingepungua sana. Tungeokoa hizo bilioni 293 na bilioni nyingine nyingi zilizotumika kwenye leseni za udereva. Nasisitiza, haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Hii pesa ingejenga kilometa 300 za lami.

Sasa "ufisadi" hapo uko wapi?

Unafikiri kila mpiga kura ana leseni ya gari?

Halafu hizo pesa ni bajeti nzima ya gharama za kuwezesha wapiga kupiga kura Tanzania nzima na si za vitambulisho pekee, wacha kudanganya umma.

IQ za Watanzania zina walakin mkubwa sana.

Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Mkuu Leseni ya udereva wewe ulipewa bure?
 
Sasa "ufisadi" hapo uko wapi?

Unafikiri kila mpiga kura ana leseni ya gari?

Halafu hizo pesa ni bajeti nzima ya gharama za kuwezesha wapiga kupiga kura Tanzania nzima na si za vitambulisho pekee, wacha kudanganya umma.

IQ za Watanzania zina walakin mkubwa sana.

Kwi kwi kwi teh teh teh!

Naona ni kama amekurupuka, anataka watanzania wote wawe na leseni za kuendeshea, pia amesahau leseni ya udereva haitolewi bure.
 
Inawezekana kabisa, lingeingizwa kwenye mradi wa vitambulisho vya taifa lingekuwa ni gharama zaidi ukilinganisha kuwa peke yake.
 
unagopa mipasho? kwa taarifa yako mi ni MZARAMO. we ni mgeni masuala ya siasa nadhani, ukipiga hesabu uchaguzi unawezaje kufanyika?kwa Katiba ipi?ya zamani au mpya ambayo mchakato wake umekwama?unadhani mchakato wa Katiba mpya kukwama unafanyika kwa bahati mbaya? Brother THINK,THINK THINK!!!!!!
 
Back
Top Bottom