Tume ya ajira Utumishi yashindwa kusaili waomba kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya ajira Utumishi yashindwa kusaili waomba kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Jul 17, 2012.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Haya ndo matokeo ya kuhodhi kila nafasi ya kazi ipitie tume ya ajira utumishi. Ni kuanzia mhudumu hadi profesa!

  Hivi karibuni baada ya utumishi kutangaza nafasi za kazi za aina hii, wengi tulitegemea watakusanya maombi na kuzipa taasisi husika kuendesha zoezi la usaili. Hali imekuwa kinyume na sasa hivi Utumishi wanajiandaa kuendesha usaili huo.

  Taarifa niliyoipata toka chuo kikuu (UD), wamepelekewa barua toka utumishi eti chuo kitunge maswali na majibu kwa ajili ya nafasi walizoomba kuajili. Yaonekana hawana uwezo wa kusaili ngazi hizo za elimu sasa wanaifanya tume ya utumishi kama baraza la mitihani.

  Ukisha shindwa kujua nini uulize muomba kazi, maoni yangu ni kwamba umeshindwa kumusaili muomba kazi. Na kwa hali tuliyo nayo lazima washindwe. Siamini kama mwalimu anayefaa atapatikana kwa maswali ya kuandikiwa halafu atumwe kwenda kufundisha chuoni baada ya kupitishwa kwa mtindo huo.

  Kwa kuwa wanaendesha usaili kwa maswali na majibu yaliyotungwa hakika sasa tutakuwa na wallimu wabovu vyuoni na hata sekta zingine za serikali. Hatutaweza kukwepa uvujaji wa maswali (au mitihani) hayo.

  Hata hivyo, lengo la utumishi kuhodhi mamulaka ya kuajiri ni nini? Nini wanakiondoa? Nini wanakiweka? Au ni haya mambo tunayoyasikia mitaani? Yaani ku-balance dini, kabila, ukanda, n.k.
   
 2. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Utaratibu wa siku mingi
   
 3. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,967
  Likes Received: 37,520
  Trophy Points: 280
  Liwalo na liwe!
   
 4. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,015
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  Hii ni nchi ya majaribio.

  Ukishindwa kuongoza nchi hii, huwezi kuongoza nchi yeyote duniani.

  Embu tazama mitaala ya elimu ienzi za Kapuya mpaka leo ilivyochakachuliwa!!
  Huyu akija anasema hakuna michezo, huyou mara history ichanganywe huku,,pyuu!!
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi nashangaa sana kuhusiana na hawa watu wanaojiita wa utumishi, inakuwaje wanatangaza kazi hadi zinazohitaji maprofessor, kwani kwenye tume hiyo kuna maprofessor wangapi na waajiliwa wengine wenye PhD? Yaani huwa nafikilia sana na naona katika Tanzania sehemu iliyosheheni wasomi itakuwa ni kwenye hiyo tume ya ajira la sivo kitakuwa kiinimacho.

  Inakuweje waweze kuwafanyia interview watu wa kada zote wao wana wafanyakazi waliosomea mambo yote hayo.Naamini kabisa kuna taasisi za serikali zinapoelekewa wafanyakazi wa ajabu kwa sababu ya huu ukiritimba wa kutumia tume ya ajira. What is the point ya kila idaya na wizara ya serikali kuwa na HR Officers ambae hawezi kuajili au kufanyisha interview? Tukiendelea kutegemea hii tume eti iwe mwajiri mkuu tumeliwa
   
 6. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Wewe unafikiri watawapatia vipi kazi "Ma- Dokta" wao feki. Huu ndio mwendo wa kwenda kuwapa "Uprofesa" hao waliojipa udaktari. Sasa hivi udaktari hauna mashiko, ni uprofesa tu ambao haununuliki. Kwa hiyo kesho Nchimbi akishindwa uchaguzi wanampa ualimu wa Mzumbe, etc,

  Kama hujui, vyuo vukuu vya Tanzania sasa vinatekeleza sera kama ile ya UPE. Nafikiri tuiite "Universal University Education" au UUE.
   
 7. Andy1

  Andy1 Senior Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ilibid wao tume waalike mtaalamu toka katika taasisi husika inayohitaji kuajiri ajumuishwe katika hiyo panel yap.
   
 8. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  wamezidi kubana viallowance, yaani hata kuwaita watendaji kutoka chuo husika wakawa chini ya mtu mmoja wa tume wakawafamnyia usaili watu wao wanaona kazi. hizo allowance zitawatokea puani waacheni na wenzenu wafaidi. mkihodhi kila kitu wenzenu watakula wapi?
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kaka mie nimependa avatar yako tu
   
 10. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Usinikumbushe hayo mkuu.
  Ile mitaala ya Mungai! Nadhani tumefikia hatua ya kujaribia kila kitu. Baadhi wanajaribia kuwa Rais
  Mawaziri ni tatizo kubwa kabisa. Ni viongozi wa kisiasa lakini bahati mbaya wanajiingiza kuchukuwa maamuzi ya kiserikali.
   
Loading...