GE2025 Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC): Polepole hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wa uchaguzi unaotumika na Tume hiyo umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na chama cha siasa, hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na madai kwamba zoezi la upigaji kura tayari limefanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa INEC, Ramadhan Kailima kupitia taarifa ya INEC ya Agosti 23, 2025, amesema taarifa hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kupotosha umma na kuibua taharuki.

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa Serikali au wa Taasisi binafsi kwa madhumuni ya upigaji kura”, amesema Kailima na kuongeza,

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi”.

Kailima amebainisha kuwa Tanzania haitumii mfumo wa kielektroniki katika kupiga kura, kuhesabu kura, au kutangaza matokeo. Badala yake, zoezi hilo hufanyika kwa kutumia utaratibu wa kawaida (manual).

“Ifahamike kuwa, Kitambulisho cha Taifa hakitumiki kupigia kura, bali Kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuhakikiwa ndiyo inayotumika wakati wa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura”, amesisitiza.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa vilishapewa Daftari la Wapiga Kura baada ya zoezi la uboreshaji kukamilika, na mawakala wa vyama watatumia daftari hilo kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi.

Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo, ikisisitiza kuwa zinasambazwa na watu wasiokuwa na uelewa wa mfumo wa uchaguzi nchini.

Tume imewasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kuupuza uongo na upotoshaji huo, na anayesambaza ana lengo la kuzua taharuki na upuuzwe kama wapotoshaji wengine.

Taarifa hii imetolewa kutokana na madai yaliyotolewa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, usiku wa tarehe 22 Agosti 2025, ambapo alidai kuwa mifumo ya CCM imeunganishwa na ya INEC na NIDA kwa madhumuni ya kudhibiti matokeo ya uchaguzi.

1755952401111.png

1755952442758.png
 
View attachment 3450151

Source: Jambo TV
Tunaomba huo mfumo ukaguliwe na independent CIT expert kama ilivyoshauriwa wawe clean
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHAJI WA KUUNGANISHWA KWA MFUMO WA UCHAGUZI NA MIFUMO MINGINE

Kumekuwepo na taarifa za upotoshaji na uongo zinazozunguka katika mitandao ya kijamii zikieleza kuwa mfumo wa Data za Uchaguzi unaotumiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi umeunganishwa na mfumo wa NIDA na chama kimoja cha siasa, na kwamba zoezi la upigaji kura (uchaguzi) limeshamalizika.

Napenda kufafanua kwamba taarifa hizo si za kweli, ni upotoshaji na uongo kwa sababu zifuatazo:

1. Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinasambazwa na mtu asiye na uelewa wala ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi.

2. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa Serikali au taasisi binafsi kwa madhumuni ya upigaji kura.

3. Mfumo wa upigaji kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo hautumii mfumo wowote wa kielektroniki.

4. Mfumo wa upigaji kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo hutumia utaratibu wa kawaida (manual).

5. Baada ya kukamilika kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari, vyama vya siasa vilikabidhiwa daftari husika linaloonyesha idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika kila kituo.

6. Mawakala wa vyama vya siasa wanaoshiriki uchaguzi hutumia Daftari husika kuwatambua wapiga kura wanaofika vituoni kupiga kura.

7. Katika mfumo wa uchaguzi wa Tanzania, mpiga kura aliyeandikishwa hufika kituoni na kuonyesha kadi yake ya mpiga kura iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Jina lake husomwa kwa sauti na msimamizi wa kituo ili kuruhusu mawakala kuthibitisha iwapo yupo kwenye Daftari. Baada ya uhakiki huo, mpiga kura hupewa karatasi ya kura ili kuendelea na utaratibu wa kupiga kura.

8. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) hakitumiki kupigia kura. Kadi pekee ya mpiga kura iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo hutumika na huhakikiwa wakati wa upigaji kura katika vituo husika.

---
Tume inawasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kupuuza taarifa hizo za uongo na upotoshaji. Lengo la kuzisambaza ni kuleta taharuki, hivyo zinapaswa kupuuzwa kama upotoshaji mwingine.

Aidha, kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025, taarifa zote sahihi kuhusu Tume zitapatikana kupitia vyanzo rasmi vikiwemo:

Tovuti ya Tume: www.inec.go.tz

Kurasa rasmi za Tume kwenye mitandao ya kijamii
---

“KURA YAKO HAKI YAKO, JITOKEZE KUPIGA KURA”

Imetolewa leo tarehe 23 Agosti 2025 na:
Kailima, R. K.
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Screenshot_20250823-151634.png

Screenshot_20250823-151656.png
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wa uchaguzi unaotumika na Tume hiyo umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na chama cha siasa, hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na madai kwamba zoezi la upigaji kura tayari limefanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa INEC, Ramadhan Kailima kupitia taarifa ya INEC ya Agosti 23, 2025, amesema taarifa hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kupotosha umma na kuibua taharuki.

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa Serikali au wa Taasisi binafsi kwa madhumuni ya upigaji kura”, amesema Kailima na kuongeza,

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi”.

Kailima amebainisha kuwa Tanzania haitumii mfumo wa kielektroniki katika kupiga kura, kuhesabu kura, au kutangaza matokeo. Badala yake, zoezi hilo hufanyika kwa kutumia utaratibu wa kawaida (manual).

“Ifahamike kuwa, Kitambulisho cha Taifa hakitumiki kupigia kura, bali Kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuhakikiwa ndiyo inayotumika wakati wa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura”, amesisitiza.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa vilishapewa Daftari la Wapiga Kura baada ya zoezi la uboreshaji kukamilika, na mawakala wa vyama watatumia daftari hilo kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi.

Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo, ikisisitiza kuwa zinasambazwa na watu wasiokuwa na uelewa wa mfumo wa uchaguzi nchini.

Tume imewasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kuupuza uongo na upotoshaji huo, na anayesambaza ana lengo la kuzua taharuki na upuuzwe kama wapotoshaji wengine.

Taarifa hii imetolewa kutokana na madai yaliyotolewa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, usiku wa tarehe 22 Agosti 2025, ambapo alidai kuwa mifumo ya CCM imeunganishwa na ya INEC na NIDA kwa madhumuni ya kudhibiti matokeo ya uchaguzi.

View attachment 3450151

Source: Jambo TV
Waandishi waliuliza kwa nini matokeo ya kura za urais 2020 hayapo kwenye tovuti ya Tume hadi leo?
 
Ngoma inatakiwa ingia kati kila chama kilete ma IT wake
 
Polepole kasema ukweli, ndiyomaana Chama Cha Mashetani(ccm) hawataki tume huru ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom