Tumalize utata bingwa wa uhasibu kati ya TIA,CBE na IAA(Arusha)

Kama ni ubora,basi kwa tanzania chuo kinachotambulika sana ni uhasibu yaani TIA,IAA(Vyuo vya serikali vinavyotoa uhasibu),na quality yake inatofautiana kulingana na matawi husika ya vyuo,mfano.mtu aliyesoma uhasibu ya dar,ni tofauti na anayesoma uhasibu ya IAA,hii ni kulingana na mifumo ya uongozi,
Ila nikuhakikishie tu yakuwa,kwa kipindi hiki cha sasa,serikali imetumia nguvu kubwa sana kuviinua vyuo vya serikali,inawezekana ukapata shahada ya uhasibu chuo cha private lakin atakayekuwa na soko sana katika ajira ni yule anayetoka chuo cha serikali,.
Tatu:
Kuhusu ubora wa mwanafunzi ni yeye mwenyewe,kama ulienda chuo na haukuwa mtu unayejar kusoma na kujenga career yako basi utaishia kuitwa graduate pekee,yaan kama ni mhasibu,ni mhasibu wa makaratasi,
Na hili ni tatizo kubwa sana kwa vijana,anazan akienda chuo ndio mda wakula bata badala yakujenga professional yake,,
Ni vyema zaid kutambua chuo ni mahali sahihi pakujenga professional..soko la ajira kwa sasa linahitaj vijana walio na uwezo zaid ya elimu ya darasan,wenye uwezo wakutatua changamoto mbali mbali,
umenena
 
Kama ugumu ndio ubora basi IAA ni nux, chuo kilikuwa hakinaga carry ukipata sup ukishindwa kuchomoa yan hata kama ulikuwa na A nane na sup 1 fu unarudia mwaka mzima zile A zote zinafutika unaanza mwanzo, watu walikuwa wako makini sana na wengi walikuwa wakifeli wakija CBE NA TIA wanamaliza vizuri tu.

Kwa infrastructure na mazingira ya kusomea CBE na TIA hazifikii hata robo ya IAA...

CHUO RAIS NA LAIN KUSOMA KULIKO VYOTE NI CBE, ukiona mtu kafeli CBE manake ana hali mbaya sana KIAKILI KICHWANI

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sina jibu la uhakika zaidi ila nikijuacho ni hiki.

Kwa CBE ya sasa, ngoma sio ya kitoto kama watu walivyokizoea, sana sana ya Dar.

TIA Mkuu kwa sasa imeshuka sio kama zamani.

Watu wanaweza wakaja hapa wakapinga ila uliza kwa wanafunzi waliomaliza vyuo karibuni.

Kuna mdau aliweka hapa kuhusu koz za uhasibu ACCA, Kuwa ndio Bodi inayohusika na wahasibu dunia nzima, mitaala yake inayoitoa, kwa hapa Tanzania kuna vyuo vichache sana ambao wanaendana nao ktk fani ya uhasibu, moja wapo ni CBE na MZUMBE.

So mwanafunzi anayemaliza hapo kwa uhasibu huwa ana credit flani kufanya mitihani ya hao jamaa.

Mwisho Mkuu mimi siamini kama kuna uhusiano mkuubwa kati ya kozi uliyosoma na chuo, unaweza ukatoka na GPA hata ya 4 na bado kwenye field ukaburuzwa na mtu aliyepata 3.0 kutoka MUCCOBS.

Hiko chuo kingine sina taarifa zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
CBE kozi zinaendana na ACCA? You must be kidding
 
IAA,TIA vingine status ni kawaida sana pia Nenda Muccobs kipo sijui kule Moshi..Chuo balaa sana naona mifumo wanayotaka kutumia pale ni kama SUA kwa sababu zamani kilikuwa chini ya SUA saivi kinaitwa MUCU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila cbe ni chuo cha kuombewa kwakweli, hapa campus ya mbeya miaka ya 2015 eti ukiwa na D mbili unajiunga certificate kwa kupigishwa tuition ya mwezi, upuuzi mtupu, Sio ivo tu chuo kilikuwa na madarasa kule Bar ya b.o.t, yani huku ndio kuliiaibisha cbe nakumbuka walevi waliwaparamia sana mabinti wa cbe. Kitu kingine mdogo Wangu alisoma hio campus nikabaki nashangaaga eti kuna topic maalum kwajili ya individual assignment, group assignment, test na final nikabaki mdomo wazi tu maana navyojua vyuo vingi final na test ni kuanzia topic ya kwanza hadi ya mwisho, nakumbuka walio disco Tia walikuwa wanaenda cbe maana hata usipofikia coursework unapewa mark up test hata 2 za kuongezea maksi, Hiki chuo wawe serious kwakweli.

Kuhusu IAA nawapa maksi zote, TIA nao nawapa zote, pia IFM ila wapunguze kudahili wanafunzi wengi..kiufupi IAA, IFM na TIA ni familia moja zote zipo wizara ya fedha, ila CBE ipo chini ya wizara ya viwanda na biashara na kimelenga sana elimu ya biashara na sio uhasibu.

Nimezungumzia elimu tu, Kuhusu kazi kwakweli watu wamerundikana mtaani maana hakuna ajira.
 
ahsante sana Cbe campus ya dar vp?
 
Back
Top Bottom