Tuma sms for free airtel to airtel

Tuma sms for free airtel to airtel

T.K

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
345
Reaction score
75
Wadau kuna hii kitu inaitwa Sema na Airtel inakuwezesha kutuma sms free kwa mteja wa Airtel aliyejiunga kwenye hiyo service (yes ni 0Tsh/SMS)

Kujiunga
Kujiunga unatuma sms neno Jiunge unaacha nafac unaandika jina unalotaka kutumia halafu unatuma kwenda namba 2011.
ikiwa successful utapata SMS ya kuthibitishwa kujiunga. Kwa hiyo kama mimi ndo najiunga naandika sms JIUNGE TK then natuma kwenda 2011.

Namna ya kutumia
Kutumia sharti huyo unayechat nae nae awe amejiunga, unaandika sms kwa kuanza na jina lake analotumia unaacha nafasi unaandika maneno yako then unatuma kwenda 2011.

Kwa mfano kama Malaria sugu kajiunga so nita sms Malariasugu habari yako? then natuma kwenda 2011​....yeye MS ataona tu Maneno habari yako na kuendelea. Kwa kweli haka kahuduma ni kazuri hasa kama ni denti maana madenti wanapenda sana chatting sasa na vocha zenyewe wakati mwingine ni mtihani!

Ni hayo tuwadau
 
Kweli JF mwisho wa matatizo.ila kuna swali najiuliza ikitokea watu zaidi ya mmoja wanatumia jina hilo hilo inakuaje?
 
Kweli JF mwisho wa matatizo.ila kuna swali najiuliza ikitokea watu zaidi ya mmoja wanatumia jina hilo hilo inakuaje?

Hapo naamini system itakujulisha kuwa jina lliko occupied nafikiri ni kama vile email zilivyo
 
Thank kwa info aisee...hata mimi nimejaribu sasahivi,imekubaali....😛oa
 
Wadau kuna hii kitu inaitwa Sema na Airtel inakuwezesha kutuma sms free kwa mteja wa Airtel aliyejiunga kwenye hiyo service (yes ni 0Tsh/SMS)

Kujiunga
Kujiunga unatuma sms neno Jiunge unaacha nafac unaandika jina unalotaka kutumia halafu unatuma kwenda namba 2011.
ikiwa successful utapata SMS ya kuthibitishwa kujiunga. Kwa hiyo kama mimi ndo najiunga naandika sms JIUNGE TK then natuma kwenda 2011.

Namna ya kutumia
Kutumia sharti huyo unayechat nae nae awe amejiunga, unaandika sms kwa kuanza na jina lake analotumia unaacha nafasi unaandika maneno yako then unatuma kwenda 2011.

Kwa mfano kama Malaria sugu kajiunga so nita sms Malariasugu habari yako? then natuma kwenda 2011 ....yeye MS ataona tu Maneno habari yako na kuendelea. Kwa kweli haka kahuduma ni kazuri hasa kama ni denti maana madenti wanapenda sana chatting sasa na vocha zenyewe wakati mwingine ni mtihani!

Ni hayo tuwadau

Sasa mbona tunatuma kwenda namba 2011,au hii ni kwa mwaka huu tu? Hii imeanza lini? Asante lakini ya ukweli pia.
 
Naweza kubadilisha jina?kama ndiyo how?msaada tafadhali
 
Naweza kubadilisha jina?kama ndiyo how?msaada tafadhali

Ndio,mfano: mimi jina langu ni yeboyebo watu wengi wanaitwa hvyo,nilijaribu kujiunga ikaniambia jina limeshatumiwa,nikabadilisha mara tatu ndo ikakubali. Hivyo unaweza kubadili.
 
Mi naitumia hiyo huduma muda mrefu kweli..ila kujitoa nimeshindwa so kama unajua namna ya kujitoa nijuze tafadhali.
 
isije ikawa wanakata kwenye huduma ingine hawakawii hawa!
 
Back
Top Bottom