Mimi ni mmojawapo wa watu wasiopenda kusikia mvutano wetu na Kenya eti kuhusu bomba la mafuta tokea Uganda. Tumekuwa na bomba la mafuta la TAZAMA tulishaambiwa linachangiaje uchumi wa nchi yetu zaidi ya ile migomo ya reli ya TAZARA ambayo haishi?
Lakini tuna bomba la gesi ambayo mikataba na ujenzi wake bado unahitaji kuchunguzwa kutokana na kunuka uvundo wa ufisadi. Sisi tumeuza madini yetu na kubaki na mashimo eti ndo tunashutuka sasa hivi na kuuona mradi wa wenzetu ndiyo mkombozi!