Mradi wa Bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania sasa kuendelea, mahakama Ufaransa yatupilia mbali kesi ya kuupinga

F16 Falcon

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
750
1,632
Mahakama moja nchini Ufaransa, imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa kupinga mradi wa Kampuni ya TotalEnergies wa uchimbaji na usafirishaji wa mafuta nchini Uganda na Tanzania.

Kesi hiyo iliwasilishwa na kampuni sita za ufaransa na makundi ya wanaharakati kutoka Uganda ambayo yaliishutumu kampuni hiyo ya Total ya Ufaransa kwa kukosa kuwajibika kuwalinda raia na mazingira wakat iwa utekelezaji wa miradi hiyo ya ya uchimbaji na usafairishaji wa mafuta kupitia mradi wa bomba la mafuta wa Tilenga.

Kampuni ya TotalEnergies na waliowasilisha kesi hiyo hawajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo wa mahakama.

Wanaharakati hao walikuwa wameiomba mahakama hiyo kuagiza kampuni ya TotalEnergies kusitisha miradi hiyo katika mataifa ya Uganda na Tanzania, kuambatana na sheria ya Ufaransa ya mwaka wa 2017, ambayo inashurutisha kampuni kuwajibika kwa adhari zitakazotokea kwa mazingira na raia wakati wa utekelezaji wa miradi yao.

Lakini mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi hilo, ikisema kuwa jaji ambaye angelichunguza kesi hiyo kwa kina ndiye anayeweza kuamua ikiwa madai dhidi ya kampuni ya Total Energies yanaweza kuchunguzwa mbali na kuidhinisha uhakiki wa operesheni za kampuni hiyo nchini Uganda na Tanzania.

BBC

Hapa wale wanaharakati UCHWARA WA KENYA tumewashinda
 

Attachments

  • Screenshot_20230228-190305_Facebook.jpg
    Screenshot_20230228-190305_Facebook.jpg
    127.6 KB · Views: 3
Safi sana,hata mheshimiwa makamba aliyaonya mabeberu yaache kutupangia cha kufanya, nadhani yamesikia,mungu ni mwema
 
Back
Top Bottom