Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Jamani ifike wakati sasa tuache kuilaumu CCM kizembe.

Granted. CCM ina makosa nengi sana. Siitetei.

Naomba nieleweke kwamba mimi si mtetezi wa CCM wala Magufuli. Ni mtetezi wa haki na mantiki, ni mtetezi uchambuzi wa kina usio na uvivu wa kufikiri.

CCM ina makosa mengi.Mengi sana. Magufuli namsema kila siku hapa.

Lakini, hivi CCM ina nguvu gani kiasi cha kulazimisha mambo nchi nzima?

Hao watu waliofanikisha wizi wa kura nchi nzima wote ni CCM?

Na baada ya wizi wa kura kujulikana wazi, wasiokuwa CCM nchi nzima wamefanya nini?

Tumeona hao wanawake wa CHADEMA waaliodai uchaguzi haukuwa wa haki na huru, wamekubali kuapishwa kupata vyeo vya ubunge. Mpaka wameadhibiwa kwa aibu.

Je, kweli tatizo letu ni CCM tu?

Hawa wataalamu watumishi wa umma, wasio na nyadhifa za kisiasa au hata uanachama wa vyama vya siasa, wanaoburuzwa kwa amri kutoka juu, tushasikia hata mmoja kaamua kujiuzulu kazi yake kwa kufuata maadili ya kazi na kukataa maamuzi ya kulazimishwa kisiasa?

Mimi naona hapa kuna jambo la utamaduni limepita siasa, tuache kujidanganya kulaumu CCM tu kila siku.
Nakubaliana na wewe ndugu kwa sehemu kubwa. Ila Tatizo linakuwa sehemu moja tu. Haya yote yanasababishwa na sera mbovu za ccm
 
Kuna watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi, walikua wanatumia ndugu zao hela za matumizi USD 1,000/=, USD 2,000/= na wengine mpaka USD 5,000/=. Ila kwasasa hivi wamesitisha kwasababu ya ujinga huu.

Ni mtihani mkubwa sana taifa kuongozwa na "WATU AMBAO HAWANA EXPOSURE YA DUNIA". Fikra zao zinakua hazifikirii "OUT OF THE BOX".


Shida ni washamba kushika madaraka kwa nguvu, hawajui Uchumi kabisa.
 
Wazanzibar wengi walio nje wameshachukua urai katika Nchi wanazoishi sasa wakija kuwekeza wanawekeza kama Watanzania au wageni? Je, Zenj pia itaruhusu dual citizenship tofauti na Bara?
Kuteleza sio kuanguka. Bara tumeanguka ila Zenji waliteleza tu na sasa wanachapa mwendo.
 
Tuliwahi ksema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Duniani kote, nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ya haraka ya kiuchumi na ambazo zinachukuliwa kama nchi zenye uchumi mkubwa duniani (Malyasia, Singapore na Thailand) hata siku moja hazikuwai kuwa na sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.

Nchi hizi hata siku moja hazikuwai kuweka sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala hasa mikubwa ya kifedha jambo lililopelekea watu wengi kupeleka fedha kwenye nchi hizi na hatimaye fedha hizi zikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha ya wanadamu na uchumi kwa ujumla.

Hapa Tanzania watu wanaojiita kuwa wazalendo, kuanzia mwaka 2015 walianzisha taratibu za kukamata fedha za watu na kuzitaifisha na pia kuweka sheria kali za kudhibiti miamala ya kifedha na matokeo yake tukayaona ndani ya miaka mitano ambapo hela ikawa adimu na watu wengi kupoteza ajira na kukosa fursa za kukopa kwa masharti nafuu kwenye mabenki.

Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.

Tulipoongea kukemea uporwaji ule wa fedha za wananchi watafutaji watu walituita majina mabovu kuwa nyie wapigaji na wezi Ila baada ya madhara yake kuonekana, leo hii huko Zanzibar wamekuja na hili👇

View attachment 1637873
Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa KWA UTARATIBU MZURI
Hili ndilo sasa wanafanya, - KWA UTARATIBU MZURI
 
Wazanzibar wengi walio nje wameshachukua urai katika Nchi wanazoishi sasa wakija kuwekeza wanawekeza kama Watanzania au wageni? Je, Zenj pia itaruhusu dual citizenship tofauti na Bara?
Yaani hiyo dual citizenship ndo inazibeba nchi kama Somalia, India, Israel na hata Nigeria kiuchumi ila hapa kwetu mijitu hadi leo haijaruhusu. Wakiulizwa majibu yao eti changamoto za kiusalama.
Kituko ni kuwa tangu lini Tanzania ikawa na changamoto za kiusalama kuliko Israel??! Sasa Kwa nini Israël wana dual citizenship na sisi hatuna???
 
Ni vitu vya kushangaza sana Mkuu. Kibunga kumbakumba AKA Membe alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje alijitahidi sana kupigia debe hii issue ya uraia pacha lakini akakosa support ya Kikwete kwani alishaona maccm hayaungi mkono na yalikuwa na dhana POTOFU ya kwamba Watu wataiba au kufanya ufisadi Tanzania kisha kuikimbia Nchi kwenda huko walikopata uraia, lakini ukweli ni kwamba majizi na mafisadi wala hayana uraia pacha yanakwiba pesa chungu nzima huku yakingiana vifua hivyo kutochukuliwa hatua za kisheria.

Yaani hiyo dual citizenship ndo inazibeba nchi kama Somalia, India, Israel na hata Nigeria kiuchumi ila hapa kwetu mijitu hadi leo haijaruhusu. Wakiulizwa majibu yao eti changamoto za kiusalama.
Kituko ni kuwa tangu lini Tanzania ikawa na changamoto za kiusalama kuliko Israel??! Sasa Kwa nini Israël wana dual citizenship na sisi hatuna???
 
Back
Top Bottom